GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,286
- 6,736
Wakuu jioni hii hapa Newala(Mtwara) limetokea tukio la Jambazi mwenye silaha kuvamia kituo cha mafuta Kiduni na kupora fedha. Wakati anaondoka eneo la tukio kaua Raia mmoja, hata hivyo wananchi wenye hasira walimfuatilia jambazi huyu ambaye alishindwa kutoroka baada ya mtu mwenye pikipiki ambaye anasadikiwa kuwa ni mwenzake kuwahi kukimbia baada ya kuona mazingira yameshakuwa magumu.
Mpaka hivi sasa bado polisi wako msituni wakimsaka jambazi huyo ambaye anaonekana kuwa na ujuzi wa hali ya juu katika kutumia silaha, askari mmoja ameshapigwa risasi eneo la makalio na amekimbizwa hospitali, pia kuna tetesi kuwa askari wawili wameuwawa.
RAIA KUUWAWA: Hili ni la uhakika kwani nimeiona maiti kwa macho yangu
ASKARI KUPIGWA RISASI: Huyu aliyejeruhiwa nimemuona kwa macho yangu akikimbizwa, hospitali pia namfahamu ni dereva wa gari za polisi.
Sina uhakika na habari za kuuwawa kwa polisi ingawa zinazungumzwa sana na watu mbalimbali.
Tuwaombee mungu askari wetu wapate ushindi katika mpambano huo mgumu ukizingatia uwa kuna hali ya mvua na giza
Wakuu hakuna umeme nitarejea baadae kama kutakuwa na taarifa za uhakika.