Wakuu jioni hii hapa Newala(Mtwara) limetokea tukio la Jambazi mwenye silaha
Kuvamia kituo cha mafuta Kiduni na kupora fedha. Wakati anaondoka eneo la tukio
kaua Raia mmoja, hata hivyo wananchi wenye hasira walimfuatilia jambazi huyu
ambaye alishindwa kutoroka baada ya mtu mwenye pikipiki ambaye anasadikiwa
kuwa ni mwenzake kuwahi kukimbia baada ya kuona mazingira yameshakuwa magumu.
Mpaka hivi sasa bado polisi wako msituni wakimsaka jambazi huyo ambaye anaonekana
kuwa na ujuzi wa hali ya juu katika kutumia silaha, askari mmoja ameshapigwa risasi eneo la
makalio na amekimbizwa hospitali, Pia kuna tetesi kuwa askari wawili wameuwawa.
*************
RAIA KUUWAWA............ Hili ni la uhakika kwani nimeiona maiti kwa macho yangu
ASKARI KUPIGWA RISASI.. Huyu aliyejeruhiwa nimemuona kwa macho yangu akikimbizwa
hospitali pia namfahamu ni dereva wa gari za polisi.
SINA UHAKIKA NA HABARI ZA KUUWAWA KWA POLISI INGAWA ZINAZUNGUMZWA SANA NA
WATU MBALIMBALI.
TUWAOMBEE MUNGU ASKARI WETU WAPATE USHINDI KATIKA MPAMBANO HUO MGUMU UKIZINGATIA
KUWA KUNA HALI YA MVUA NA GIZA
WAKUU HAKUNA UMEME NITAREJEA BAADAE KAMA KUTAKUWA NA TAARIFA ZA UHAKIKA.