Mtwara: Mwanamke ajeruhiwa kwa kukatwa mapanga kisa simu ya 24,000/=

Mtwara: Mwanamke ajeruhiwa kwa kukatwa mapanga kisa simu ya 24,000/=

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1643369441603.png

Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Lyowa Mkoani Mtwara, Josephine Boniface (30) amejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kwenye miguu yake yote miwili na mumewe baada ya kupoteza simu ndogo (Kiswaswadu) yenye thamani ya Tsh. 24,000.

Josephine anasema wakiwa kwenye sherehe za ngoma za jando na unyago usiku kijijini hapo, Mumewe alimkabidhi simu hiyo ndogo ili amhifadhie lakini baadaye alipokea taarifa ya kushtukiza ya kuunguliwa moto nyumba ya Mdogo wake kijijini jirani na kujikuta anapoteza simu bila kujua "tuliporudi nyumbani, nilimwambia Mume wangu ambaye alipata hasira na kisha kuchukua panga kuanza kunipiga nalo sehemu mbalimbali za mwili na kunijeruhi miguuni"

“Mume wangu alipofika nyumbani hapa kwa Mama, tukampa taarifa za tukio la kuunguuliwa kwa moto nyumba ya Ndugu zetu na Mimi ndio nikamwambia kwamba nimedondosha simu, akasema 'aah haiwezekani kudondosha simu yangu Mimi nataka simu yangu, sijui habari za moto, wala habari za nini, sitaki chochote, nataka simu yangu, akaanza kunipiga" anasema Josephine
Hassan.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Lyowa, Mohamed Mmunda amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema Mwanaume huyo ametoroka baada ya tukio.

Chanzo: Millard Ayo
 
Mwanamke mmoja Mkazi wa Kijiji cha Lyowa Mkoani Mtwara, Josephine Boniface (30) amejeruhiwa kwa kukatwa na mapanga kwenye miguu yake yote miwili na mumewe baada ya kupoteza simu ndogo (Kiswaswadu) yenye thamani ya Tsh. 24,000...
Haya matukio yanazidi kukithiri katika jamii yetu.

Kuna haja kubwa sana ya watu kutubu dhambi na kumrudia muumba wetu. Inaumiza, kila siku matukii kama siyo ya mauaji basi itakuwa majeruhi.

Huenda watu wanaishi kwenye msongo wa mawazo wanahitaji Psychological therapy wakae sawa.!!
 
Kisa sio Simu; Kisa ni Uchizi wa aliyefanya hayo majambo..., Au ndio pale the Last Straw which broke the Camels Back
 
Watasema haya matukio yanazidi kukithiri, mara legasi za mwendazake
 
Mapenzi ni ugonjwa wa akili

Ukichanganya na umasikini ndio kabisaaaa ni Wehu...

Inahitaji nguvu ya ziada kumaliza matatizo ya namna hii
 
  • Thanks
Reactions: nao
Uchizi wanaupata ndani ya Ndoa

Unapima ukimwi kabla ya ndoa lakin baada ya ndoa ndio unakuwa kwny risk zaid maana unaeenda nae kavukavu hujui yeye huwa anaendaje?
Mimi naona kabla ya ndoa watu wakapimwe akili kwanza
 
Back
Top Bottom