Kasheshe
JF-Expert Member
- Jun 29, 2007
- 4,694
- 790
Profesa Lipumba, CUF wanatafuta ufalme gani?
Chama cha Wananchi (CUF), kupitia kwa mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba, juzi kilitoa tamko kali la kushutumu Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuhusu mwenendo wa mazungumzo ya mwafaka.
Mwenyekiti huyo alizungumza maneno mengi mno, hata akafikia wakati wa kuomba msaada wa jumuiya ya kimataifa, katika kuhakikisha kuwa mazungumzo ya mwafaka yanazaa matunda mazuri.
CUF wanaamini kuwa CCM ndio wanaokwamisha mwafaka huo, kwa maelezo kwamba wamefanya ghiliba kwa uhadaa ulimwengu.
Kwanza ni vema tukasema kwamba sisi hatufungamani na upande wowote katika suala hili, ilimradi tu pande zote- CUF na CCM - wanachotaka ni kuona Tanzania inaendelea kuwa nchi ya amani.
Kauli za Profesa Lipumba, si tu kwamba zinaamsha hisia za vurugu miongoni mwa wafuasi wa vyama hivyo, lakini ni kauli iliyojikita zaidi katika utashi wa propaganda za kisiasa.
Pengine CUF wanajua kwamba baada ya kuwepo mwafaka, hawatakuwa na jingine la kuwafanya wasikike.
Tunasema hivyo kwa sababu kwa muda wenyewe wa mazungumzo bado haujaisha. Profesa Lipumba kasema zimebaki siku saba. Ndiyo, siku hizo ni nyingi. Hata kama ingekuwa imebaki siku moja, bado siku hiyo ni muhimu.
Ndiyo maana tunaamini kuwa kabla ya kiongozi huyo kuzomoka na kuanza kutoa maneno ya kuwatisha wananchi, angesubiri kwanza aone hadi siku ya mwisho, kitu gani kitakuwa kimefanywa na CCM.
Profesa Lipumba amezungumza maneno makali, akitaka umma uamini kuwa Zanzibar ni kama Darfur.
Kwa kauli zake za kuomba msaada wa kimataifa, anataka kuonyesha kwamba Zanzibar sasa watu hata hawasaidiani chumvi. Hii si kweli.
Kwa kusema kwamba Rais Jakaya Kikwete amekuwa akitoa ulaghai, hasa kwenye hotuba yake ya Desemba, mwaka juzi, huko ni mkumvunja moyo kiongozi huyo aliyeapa kusimamia kidete upatikanaji mwafaka wa kudumu Zanzibar.
Kwa yeyote atakayesikiliza kauli ya Profesa Lipumba ya jana, atagundua kwamba hizi ni propaganda za kisiasa anazoeneza.
Hakuna anayezuia propaganda hizo, lakini zinapokuwa na mwelekeo wa kujenga au kuamsha hisia za chuki miongoni mwa Wanzanzibar na Watanzania kwa ujumla, hapo tutapinga.
Ni ukweli ulio wazi kwamba Zanzibar yapo matatizo ya kisiasa, lakini matatizo haya si ya kutisha kama Profesa Lipumba na chama chake wanavyotangaza.
Mazungumzo ya Mwafaka yanahitaji ustahimilivu, kuaminiana na kuweka mbele zaidi, maslahi ya nchi na wananchi.
Kwa hili tunapenda kumwambia Profesa Lipumba kwamba asilikuze mno. Mara zote Watanzania wamemaliza tofauti zao kwa njia ya mazungumzo. Kwa kuwa nia ya kumaliza matatizo ya Zanzibar ipo, na imeanza kuonyeshwa na viongozi wetu wa vyama viwili, basi tusubiri.
Kama Darfur wanakuja kwetu kutafututa mwafaka, hilo CUF hawalioni? kama kungekuwa na vita anyohubiri Lipumba, nani angekuja kuendesha vikao vya mwafaka hapa? Chonde Profesa Lipumba.
Maoni ya Mhariri: Mtanzania Agosti 8.