PEMBA IJITENGE
CCM hawako serious waseme kabisa hakuna muhafaka mpaka baada ya uchaguzi wa 2010 kwani karume alishasema alishinda kihalali na hana mpango wa kugawana madaraka na mtu yeyote, kuwa wakweli kutawafanya CUF wajue wanafanya nini badala ya kuwambia kuwa watapewa nafasi za uwaziri wakati si kweli.
Majadiliano yasimamiwe na raisi mwenyewe kuonyesha kuwa yuko committed.
Mimi naona mambo ya muafaka yashashindikana. Sidhani kama kuna wakati ambapo CCM watakubali kushindwa kwenye uchaguzi wowote Zanzibar katika ngazi ya Rais, mpaka pale watakaposhindwa kwenye uchaguzi wa Rais wa Jamhuri ya muungano. Kitu ambacho kutokea siku za karibuni ni ndoto. Ni vigumu sana sehemu ya nchi kuendelea iwapo wananchi hawautaki uongozi uliopo, na kimsingi CCM wapo Pemba kimabavu (kama Bush Irak).
Sasa natamka rasmi kwamba endapo CCM hawataki serikali ya mseto Zanzibar basi ni bora Pemba ijitenge. Haina maana, tena ni upimbavu kulazimisha utawala katika karne hii. tujifunze kwa yaliyotokea sehemu mbalimbali za dunia kwenye hii miungano feki, iko wapi USSR, Yugoslavia, na nyinginezo? Maana ya kuwa na muungano ni kujenga nguvu ya kiuchumi pamoja na mambo mengine, kunatengenezwa nini Zanzibar kwenye umoja huo unaolazimishwa kama siyo chuki tu kwenye vizazi vinavyokuja?
Madhara ya chuki inayopandwa na CCM kati ya Waunguja na Wapemba itakujaonekana wakati akina kikwete na akina Karume hawapo tena duniani, ni itakuwa mbaya kuliko hata ya Wayahudi na Wapelestina huko mashariki gani sijui!
Kwa hali ilivyo sasa nadhani Pemba ingepata maendeleo ya haraka kama ingekuwa ni nchi inayojitegemea kuliko kuwa part ya Zanzibar. Kila siku muafaka muafaka, tumeshachoka sasa, kwanza muafaka gani huo usiopatikana kwa miaka yote hiyo? Maana yake ni kwamba huo muafaka haupo. Kuna nini wanacholazimisha hawa watu kwenye huo muungano? Kwa sababu ule mkataba wa muungano (TANGANYIKA NA ZANZIBAR) aliou-upload muungwana mmoja hapa JF hauna kipengele chochote kinachosema kuwa huu muungano ni wa milele!!! Sembuse Unguja na Pemba ambapo hata mkataba hamna!!!
KWANINI TUALAZIMISHA KUWA PAMOJA?? VISIWA VIPO TOFAUTI MUNGU ALITAKA VIWE HIVYO. SASA KWA NINI TUNALAZIMISHA WATU WAJE WAUANE BAADAE?? KWANINI? KWANINI? KWANINI? KWANINI? NA KWANINI????? SIPATI JIBU HATA NIKIJIULIZA MARA ELFU!!! MWEEE!!!
PS: Nachanganya muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar NA Unguja na Pemba kwa sababu ni yaleyale tu, msichanganyikiwe waungwana!!! Kama visiwa vipo tofauti lakini kunautawala mmoja kwangu ni muungano tu.