BAKIIF Islamic
JF-Expert Member
- Jul 11, 2021
- 600
- 1,843
السَّلاَمُ عَلَيْكُمْ وَرَحْمَةُ اللهِ وَبَرَكَاتُهُ
Kama mjuavyo uislamu sio dini ngumu, thamani ya Biriani, Pilau na Ubwabwa, viliwe katika mjumuiko wa kheri ambao MUNGU anauridhia, hivyo tunachukua fursa hii kuwatangazia waislamu wote wa JamiiForum kwamba Tare 12/12/2022 siku ya Jumamosi saa mbili kamili usiku tutakuwa na Mawlid ya kumuadhimisha mtukufu wa Umma, Nabii Muhammad S.a.w hapa BAKIIF ISLAMIC, Kimara-Korogwe Dar es salaam, Tanzania.
Nachukua fursa hii kukukaribisha ufike bila kukosa, tusherehekee kwa pamoja khafla hii ya Mazazi ya Mtume Muhammad s.a.w, na pia unaweza kuchangia kufanikisha shughuli hii adhwim kwa kuwakilisha mchango wako au swadaka yako hapa BAKIIF ISLAMIC. Katika siku hiyo tutapata wasaa wa kuwarehemu ndugu zetu walio tangulia mbele za haki. Hivyo usikose kujumuika nasi katika viwanja vya BAKIIF.
Wabillahi taufiq walhidayah"
BAKIIF ISLAMIC
P.O.BOX 55185
Kimara Korogwe,
KAM College Road, Kivulini Street
House no 36
Phone +255 755 351 262
Hapa chini Waeza burudika na Qasida (Annayu Watwaru)