Mualiko kwa wana JamiiForum: Tarehe 12/12/2022 tutakuwa na Mawlid ya Mtume Muhammad (S.A.W) hapa BAKIIF ISLAMIC

Madhehebu ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani. Ni makundi ndani ya dini fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja umoja wa msingi. Madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana vita. Kwa kifupi madhehebu ni mapokeo ya ufahamu kunako dini husika. Wakati alipoishi

Yesu Kristo, dini ya Uyahudi ilikuwa na madhehebu yaliyoshindana sana, hasa Masadukayo, Mafarisayo na Waeseni lakini wote walibakia kuwa ni dini ya uyahudi japokuwa walikuwa wanatofautiana kwa mengi.

Wafuasi wa dini ya Ukristo, kutokana na wingi wao katika urefu wa historia na upana wa jiografia, wamegawanyika katika madhehebu mengi, kuanzia Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki hadi makundi elfu kadhaa ya Uprotestanti na ushirika wa Anglikana na yanazidi kuongezeka siku kwa siku lakini wote wanabakia katika njia kuu ya UKristo ispokuwa mapokezi yao yametofautiana kwa baadhi ya vitu.

Sasa katika uislamu kuna mikondo mitatu mikubwa ambayo ni Sunni-Waljamaa, Shia na Wahabiyya ambao ni Answar Sunna. Shia ndani yao wamegawanyika katika makundi mengi zaidi.

Sunni-waljamaa kuna madhehebu au madhhab manne yanayokubaliwa rasmi. Wahabiyya wao walianza kujiita Answar Sunna' ni dhehebu ndani ya Sunni lililo vuka mipaka katika sheria za dini. Sunni wote wanafanya Mawlid ispokuwa hao 'Wahabiyya au Answar sunna' ambao kwasasa nao wamegawanyika ndani yake kuna dhehebu la 'Salafy Swaleh' ambalo lina misimamo mikali zaidi na sheria zao ni kali zaidi wao wanajihusisha na mambo ya itikadi zaidi (Tawhid).

Kwa hivyo Mawlid hupingwa na Wahabiya na sio Sunni.
Ahsante sana kiongozi,umenipa somo ambalo hapo kabla nilikuwa silijuhi,ubarikiwe sana

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Madhehebu ni mafundisho, maadili na matendo ya ibada yaliyo ya msingi katika dini fulani. Ni makundi ndani ya dini fulani ambayo yanatofautiana bila ya kuvunja umoja wa msingi. Madhehebu mbalimbali ya dini ileile yanaweza kushindana hata kupigana vita. Kwa kifupi madhehebu ni mapokeo ya ufahamu kunako dini husika. Wakati alipoishi

Yesu Kristo, dini ya Uyahudi ilikuwa na madhehebu yaliyoshindana sana, hasa Masadukayo, Mafarisayo na Waeseni lakini wote walibakia kuwa ni dini ya uyahudi japokuwa walikuwa wanatofautiana kwa mengi.

Wafuasi wa dini ya Ukristo, kutokana na wingi wao katika urefu wa historia na upana wa jiografia, wamegawanyika katika madhehebu mengi, kuanzia Kanisa Katoliki, Waorthodoksi na Waorthodoksi wa Mashariki hadi makundi elfu kadhaa ya Uprotestanti na ushirika wa Anglikana na yanazidi kuongezeka siku kwa siku lakini wote wanabakia katika njia kuu ya UKristo ispokuwa mapokezi yao yametofautiana kwa baadhi ya vitu.

Sasa katika uislamu kuna mikondo mitatu mikubwa ambayo ni Sunni-Waljamaa, Shia na Wahabiyya ambao ni Answar Sunna. Shia ndani yao wamegawanyika katika makundi mengi zaidi.

Sunni-waljamaa kuna madhehebu au madhhab manne yanayokubaliwa rasmi. Wahabiyya wao walianza kujiita Answar Sunna' ni dhehebu ndani ya Sunni lililo vuka mipaka katika sheria za dini. Sunni wote wanafanya Mawlid ispokuwa hao 'Wahabiyya au Answar sunna' ambao kwasasa nao wamegawanyika ndani yake kuna dhehebu la 'Salafy Swaleh' ambalo lina misimamo mikali zaidi na sheria zao ni kali zaidi wao wanajihusisha na mambo ya itikadi zaidi (Tawhid).

Kwa hivyo Mawlid hupingwa na Wahabiya na sio Sunni. Mawahaby pia hupinga kupiga dufu, hupinga watu kusoma dua kwa pamoja, hupinga muandamo wa mwezi wao wanafuata mwezi wa Saudia arabia, hupinga kuwasomea Maiti Qur'an na dua ya Kaburini, hupinga mwanaume kuvaa kanzu ndefu, wanahimiza ufugaji wa ndevu kama sunna ya mtume s.a.w, wao ndio hujihusisha na uchezaji wa kareti, na makundi mengi ya kigaidi yamehusishwa na Uwahhaby kwasababu wao hufundisha zaidi itikadi (Tawhid) katika kumpwekesha Mwenyezi MUNGU. Kwa ufupi ni watu wenye misimamo mikali katika dini, na mambo mengi katika uislamu wameyakanusha.
Hao sunni ndo nawaonaga wako smart Wana hoja wanaeleweka
Nyie waislamu BAKWATA hamna kitu
Mpo kimaslahi tu
Mwezi unaweza uandame watu wauone isiwe eid Hadi mufti atangaze
Madufu kibao
Sunni ndo real muslim
Me sio Muislam lakin napenda mtu asimamie anachokiamini sio kufata upepo na matakwa ya binadamu
 
Hao unao wazungumzia sio Sunni, wao huitwa Wahabiyya au Answar Sunna. BAKWATA sio dhehebu bali ni taasisi ni Baraza kuu la Waislamu Tanzania ambalo lipo chini ya Madhehebu ya Sunni.
Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Ambao Mawahabby wamejiegemeza eneo hili.

Kundia la pili wanasema kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii. Ambapo Sunni waljamaa wameegemea eneo hili

Na hiyo ndio maana ya Madhehebu katika dini. Upokeaji tofauti na rai tofauti. Kila mmoja anafuata kule anako kuona kunafaa bila kuwatusi na kuwadhihaki wengine.
 
Back
Top Bottom