Mualiko kwa wana JamiiForum: Tarehe 12/12/2022 tutakuwa na Mawlid ya Mtume Muhammad (S.A.W) hapa BAKIIF ISLAMIC

Ahsante sana kiongozi,umenipa somo ambalo hapo kabla nilikuwa silijuhi,ubarikiwe sana

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Hao sunni ndo nawaonaga wako smart Wana hoja wanaeleweka
Nyie waislamu BAKWATA hamna kitu
Mpo kimaslahi tu
Mwezi unaweza uandame watu wauone isiwe eid Hadi mufti atangaze
Madufu kibao
Sunni ndo real muslim
Me sio Muislam lakin napenda mtu asimamie anachokiamini sio kufata upepo na matakwa ya binadamu
 
Hao unao wazungumzia sio Sunni, wao huitwa Wahabiyya au Answar Sunna. BAKWATA sio dhehebu bali ni taasisi ni Baraza kuu la Waislamu Tanzania ambalo lipo chini ya Madhehebu ya Sunni.
Kundi la kwanza ni la wale wanaosema kuwa mwezi ukionekana katika mji mmoja au sehemu moja, basi Waislamu wengine popote walipo ulimwenguni watalazimika kufunga au kufungua. Haya pia ni maoni ya Imamu Hambali, Ambao Mawahabby wamejiegemeza eneo hili.

Kundia la pili wanasema kama kuna masafa marefu kati ya mji ulipoonekana mwezi na mji watu walipopata taarifa juu ya kuonekana kwake haitajuzu kwao kufuata mwandamo huo, lakini endapo mji huo utakuwa umekaribiana basi watu waliopata taarifa ya kuandama mwezi kutoka mji wa karibu watawajibika kufunga au kufungua, mwanachuoni mashuhuri anayeshikilia rai hii ni Imamu Shafii. Ambapo Sunni waljamaa wameegemea eneo hili

Na hiyo ndio maana ya Madhehebu katika dini. Upokeaji tofauti na rai tofauti. Kila mmoja anafuata kule anako kuona kunafaa bila kuwatusi na kuwadhihaki wengine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…