SoC04 Muamala kukosewa

SoC04 Muamala kukosewa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Pendragon24

Member
Joined
Aug 8, 2018
Posts
68
Reaction score
97
Ni kitendo cha aibu sana kama nchi tunajisifu kwa usalama wa mtandao lakini bado watumiaji wengi wa huduma za kifedha kidijitali wanapoteza mabilioni ya fedha eeti kwa sababu mpokeaji aliyepokea pesa kimakosa amekwisha kutoa pesa hizo katika akaunti yake.

Serikali kupitia waziri wa habari, mawasiliano na teknolojia ya habari pamoja na TCRA kwa pamoja wanathibitisha kwamba watumiaji wengi wa huduma za mawasiliano nchini hawana uelewa na matumizi sahihi ya simu za mkononi na dhana nzima ya mabadiliko ya kidigitali. Wananchi wengi wanapitia changamoto nyingi hasa wanapofanya malipo kupitia mifumo ya kidigitali kama vile simu za mkononi ua mabenki.

Wapo wananchi wanakabidhi simu zao kwa mawakala ili aweze kutolewa pesa saa nyingine wakala anapewa hadi namba ya siri ili aweze kumtolea hela. Hali hii ni mbaya sana kwa watumiaji wa mijini lakini ni mbaya zaidi kwa watumiaji waliopo vijijini.

Watumiaji wakati wote wamekuwa wakipata hasara katika kutuma na kupokea pesa, kununua muda wa maongezi, uingizaji wa vocha, kulipia luku na malipo mengine ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali kupitia simu za mkononi na mabenki ambapo watumiaji wengi wanapoteza pesa nyingi kwa kukosea kosea baadhi ya namba wakati wa kukamilisha malipo.

Labda alikuwa atume pesa kwa mtu X ghafla amekosea baadhi ya namba ametuma kwenda kwa mtu YZ. Alikuwa anunue salio la shilingi 1,000 ghafla amenunu la shilingi 10,000. Alikuwa atume pesa kwenye akaunti JJJO1 amekosea ameweka akaunti JJJ01. Alikuwa alipie huduma fulani kwa control namba 991091442608 namba zimemchanganya kalipa kwenda 9910091442680.

Mara nyingi mtoa huduma anathibitisha ni kweli muamala wako tumeuona umekwenda kwa YZ lakini muamala huo umeshatolewa tumeshindwa kurudisha. Na hapo ndipo pesa yako inakuwa imepotea rasmi na hakuna uwezekano wa kuipata tena. Huu ni uonevu mkubwa kwa watumiaji.

Hivi kweli zama hizi za kidigitali mitandao ya simu imeshindwa kabisa kutengeneza mfumo ambao utasaidia muamala huo uliotumwa kwa makosa kurudishwa? au mtu kurudishiwa shilingi 9,000 yake baada ya kukosea kununua salio?

Saa nyingine mtoa huduma anathibitisha kwamba ni kweli umetuma pesa kwenda kwa mtu YZ tumefanikiwa kuuzuia na ndani ya masaa 24 au 48 utarudishwa.

Sasa kwa muda huu wote wa kusubiri je huyu mwananchi anawezaje kumudu maisha yake kama hiyo pesa ndiyo ilikuwa tegemeo lake? Kwanini watoa huduma wasiwajibike kwa wakati huo kisha baada ya hayo masaa hizo pesa zirudi kwao?

Je, vipi kama kwa wakati huo huyo mtu alikuwa alipie gharama za hospitali au alikuwa anunue dawa kwa ajili ya mazao au mifugo yake au kama alikuwa apate hela ili anunue chakula au hata kwa matumizi yake binafsi atafanyaje?

Vitendo hivyo vinawaumiza sana wananchi hasa wa hali ya chini ambao ni ngumu sana kupata hela nyingine kwa wakati huo ili kufidia kile kilichopotea. huku wadau wengine kama vile watoa huduma wakikwepa kuwajibika katika kusaidia walau sehemu ya hasara hiyo.

Hakuna mtu anayedhamiria kukosea inatokea labda kwa sababu ya haraka za hapa na pale, uelewa mdogo, bahati mbaya bila kujua na saa nyingine uwepo wa namba namba nyingi zinamchanganya mtu (control number) pia udhaifu wa mifumo ya kidigitali ya watoa huduma.

Ndio maana ndani ya mabenki na simu kuna fedha nyingi sana zinaelea hewani hazina mwenyewe miamala imeingia kimakosa na wameshindwa kurudisha kwa wahusika kwa hiyo miamala mingi imebaki inaelea hewani bila mwelekeo wowote,pia njia zilizopo (manually) ili kurudishiwa pesa hizo ni ngumu sana na saa nyingine hazijulikani, hivyo wengi huamua kuacha tu.

Tungekuwa tunapewa takwimu cha kiasi cha pesa kilichotumwa kwa makosa bila kurudishwa kwa wahusika na zile zinazoelea tu hewani tungepata picha halisi ya mabilioni ya fedha za watumiaji zinazopotea kizembe ambapo kama mwananchi asingalitumia mfumo wao angeweza kuziepuka hasara hizo.

Sasa TANZANIA TUITAKAYO ni lazima mtumiaji arudishiwe pesa yake aliyotuma kimakosa na kwa wakati hata kama mpokeaji amekwisha kutoa pesa hizo katika akaunti yake. tunataka uwajibika wa wadau wote wa mawasiliano hasa mitandao ya simu ili kwa pamoja tutokomeza utapeli huo ambao ni mateso makubwa kwa watumiaji, hizi ni baadhi tu ya njia ili kuleta uwajibikaji.

  • Uwepo wa namba maalumu ya kupiga ili mtu aliyekosea kutuma muamala aweze kusaidiwa kwa haraka badala ya namba mia moja ambayo menyu yake inamlolongo mrefu ili kuongea na mtoa huduma, maana kama watoa huduma wangekuwa wanapokea simu kwa haraka pangekuwa na uwezekano mkubwa wa kuzuia miamala hiyo pasipo kutolewa.
  • Pawepo na mfumo thabiti wa kidigitali ili kufuatilia miamala iliyokosewa kwa haraka hata kama mhusika amekwisha toa hiyo pesa iliyoingia kwenye simu yake kimakosa kama ameshindwa kutoa ushirikiano afuatiliwe kwa karibu ili aweze kurejesha, maana taarifa zake zote zipo kupitia ile namba kipi kinatushinda kumfuatilia?
  • Mtumiaji aliyekosea kutuma muamala anatakiwa arejeshewe pesa kamili punde tu inapothibitika kwamba alituma kimakosa sio mpaka kusubiri masaa 24 au 48 au mpokeaji amekwisha kuitoa katika akaunti yake.katika hili watoa huduma hawawezi kukwepo kuwajibika katika kubeba hasara ilitokana na uwepo wa mfumo wao.
  • Pawepo na designing au option itakayompeleka mtumaji wa pesa moja kwa moja kwenye contact list ili aweze kuchagua jina au namba anayokusudia kutuma pesa au kulipia huduma fulani kwa njia ya simu au benki moja kwa moja.
  • Na kwa wakala pia pawepo na mfumo maalumu wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya scanning hata kwa kutumia bar code, tutoke kwenye mfumo wa analogia wa kutaja taja au kuandika namba katika ulimwengu huu wa kidigitali ni vyema kila kitu kiende kidigitali pia.
Wakati wa kuchangia bajeti ya Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari katika mwaka wa fedha 2024/2025 mbunge mmoja alichangia kwa msisitizo mkubwa sana kwamba nchi yetu sasa inapaswa kuingia kwenye mfumo wa cashless economy ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato ya serikali. Kama hatutahakikisha usalama katika mifumo ya kidigitali hasa katika huduma za kifedha wananchi wengi hawatakubali kutumia mifumo hiyo kwa hofu waliyonayo ya kupoteza pesa pasipo refund yeyote. Ni lazima kwanza tutengeneze uwajibikaji wa wadau wote ili watumiaji wasije kupoteza imani na watoa huduma.
 
Upvote 5
Sasa kwa muda huu wote wa kusubiri je huyu mwananchi anawezaje kumudu maisha yake kama hiyo pesa ndiyo ilikuwa tegemeo lake? Kwanini watoa huduma wasiwajibike kwa wakati huo kisha baada ya hayo masaa hizo pesa zirudi kwao?
Watoa huduma, wajitahidi kuwajibika. Na wapokea huduma pia wawajibike.

Ninaamini mifumo yote ina kipengeke cha kuuhakiki muamala kabla haujatuma kuthibitisha. Pia kuandika majina ya watu na taasisi zinazotumiwa pesa. Hivyo ni rai tu kila upande ufanye "due diligence" wazungu walisema.

Mtumiaji aliyekosea kutuma muamala anatakiwa arejeshewe pesa kamili punde tu inapothibitika kwamba alituma kimakosa sio mpaka kusubiri masaa 24 au 48 au mpokeaji amekwisha kuitoa katika akaunti yake.
Nakubaliana, arejeshewe lakini ni lazima alipie huduma. Ikatwe kwenye pesa yake. Jamani haki itawale bila kumuumiza mtu. Fikiria mitandao iajiri mtu standby wa kushughulikia miamala iliyokosewa halafu asiliowe kweli? Na kama analipwa fedha itike kwa nani?
Pawepo na designing au option itakayompeleka mtumaji wa pesa moja kwa moja kwenye contact list ili aweze kuchagua jina au namba anayokusudia kutuma pesa au kulipia huduma fulani kwa njia ya simu au benki moja kwa moja.
Hii itasaidia, nzuri.

Na kwa wakala pia pawepo na mfumo maalumu wa kutuma na kupokea pesa kwa njia ya scanning hata kwa kutumia bar code, tutoke kwenye mfumo wa analogia wa kutaja taja au kuandika namba katika ulimwengu huu wa kidigitali ni vyema kila kitu kiende kidigitali pia.
Ewaaaaaah! Haya ndio maboresho sasa. Ahsante.
Kama hatutahakikisha usalama katika mifumo ya kidigitali hasa katika huduma za kifedha wananchi wengi hawatakubali kutumia mifumo hiyo kwa hofu waliyonayo ya kupoteza pesa pasipo refund yeyote. Ni lazima kwanza tutengeneze uwajibikaji wa wadau wote ili watumiaji wasije kupoteza imani na watoa huduma.
Hakika
 
Back
Top Bottom