Muda huu kuna wazinzi wanamcheka Mwijaku kufanya uzinzi

Muda huu kuna wazinzi wanamcheka Mwijaku kufanya uzinzi

Right Marker

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
194
Reaction score
625
Kama ilivyokuwa kwa "Mwijaku wa zamani" aliwacheka wazinzi wenzake waliomtangulia kubumbuluka kwenye skendo ya uzinzi. Ndivyo ilivyo hata sasa kuna wazinzi wengine wanamcheka "Mwijaku wa sasa" kufanya uzinzi.

Kila mwizi ana siku yake ya arobaini. Hizo arobaini hazihesabiwi kama ulivyofundishwa kuhesabu tarakimu (namba) huko Chekechea. Arobaini ya mwizi ni hali ya hewa (haitabiriki), unaweza kuanza uhalifu asubuhi lakini jioni unakamatwa.

Usimcheke mwizi mwenzako aliyefikisha siku yake ya arobaini, dawa sahihi ya kuepuka uhalifu ni kutofanya uhalifu. Wezi wa mapenzi tupo wengi, kinachosubiriwa ni hiyo arobaini. Huenda hata yule shemeji yetu kuna mtu anamkaza kimya kimya.

Right Marker
Dar es salaam.
 
Back
Top Bottom