Muda mwafaka wa kuanza Kliniki

Muda mwafaka wa kuanza Kliniki

IlangiKwetu

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
85
Reaction score
33
Heshima mbele wadau,

Naomba kujua muda mwafaka wa mama mjamzito kuanza kuhudhuria kiliniki, hasa mimba ya kwanza. Coz wa mama watoto ana wiki kumi na nne (14) hajaanza kuhudhuria.

Na anasema mtoto hajacheza kwa wiki mbili sasa, pia tatizo hili linasababishwa na kitu gani MziziMkavu watu8 msaada wenu tafadhari.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kawaida inatakiwa akijua tu ana ujauzito anatakiwa aanze kliniki kwani kuna DAWA anatakiwa atumie ambazo na huduma nyingi nyingi ukiangalia watu wengi ambao watoto wao walipata matatizo ya kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa ni wale ambao either walichelewa au hawakwenda kabisa clinic . mwambie kuna tu DAWA rule wanatoa clinic TWA kuongeza damu na pia vinasaidia mtoto asizaliwe na uzito MDOGO pia inazuia mtoto asipate spine bifida. Matatizo ya brain na uti Wa mgongo
 
Ni muda muafaka.... Chini ya wiki 16
Aanze
 
Wangu amamizi 7 bilabila sijui aanze lini wadau
 
Mkuu heshima yako,

Mwanamke mjamzito hushauriwa kuanza kuhudhuria kliniki pindi tu anapokuwa na uhakika wa kunasa ujauzito.

Kuna mambo mengi ambayo hushauriwa ahudhuriapo kliniki yenye kuzingatia afya yake pamoja na ya kiumbe/viumbe waliopo tumboni.

Ukiacha hilo pia huwa kuna vipimo hufanywa na wahusika wa afya kuzingatiana na umri wa ujauzito.

Naomba kujua muda mwafaka wa mama mjamzito kuanza kuhudhuria kiliniki, hasa mimba ya kwanza. Coz wa mama watoto ana wiki kumi na nne (14) hajaanza kuhudhuria.

Huwezi kusema moja kwa moja hilo ni tatizo pasipo kuthibitisha kwa vipimo ikizingatiwa kuwa huo ni ujauzito wake wa awali.

Kwa umri wa ujauzito alionao ndio wakati ambapo mtoto huanza movements lakini huwa kwa nadra si kama movements dhahiri za trimister ya tatu...

Tafadhali msisitize mkeo afanye hima kuhudhuria kliniki mapema iwezekanavyo...

Na anasema mtoto hajacheza kwa wiki mbili sasa, pia tatizo hili linasababishwa na kitu gani MziziMkavu watu8 msaada wenu tafadhari.
 
Last edited by a moderator:
wakwangu alianza kwenda clinic baada ya kufikisha miezi 3, kuhusu mtoto kucheza ni mapema sana,wangu alianza kucheza akiwa na miezi 6 kwa hiyo ondoa hofu!
 
Kuna vipimo anatakiwa pia apimwe mfano syphilis a.k.a kaswende kwani kama mama ana ugonjwa huo wale spiralcates Wa kaswende wanauwezo Wa Ku cross placenta barrier na kumdhulu mtoto anaeza zaliwa kipofu, kuna kipomo cha kundi LA damu blood group mfano kama mama ana resus factor tofauti na mtoto reaction inaeza kutokea kwa mtoto yan haemolytic disease of new born hivo mama akiwahi clinic akapimwa akikutwa rhesus negative atapewa ant d ya kuzuia hdn na kipimo chengine ni cha h.I.v akikutwa mama ana maambukizi atapewa DAWA ( ART) ili kuzuia maambukizi toka kwa mama kwenda kwa mtoto .
 
Kwa kawaida inatakiwa akijua tu ana ujauzito anatakiwa aanze kliniki kwani kuna DAWA anatakiwa atumie ambazo na huduma nyingi nyingi ukiangalia watu wengi ambao watoto wao walipata matatizo ya kuzaa watoto wenye vichwa vikubwa ni wale ambao either walichelewa au hawakwenda kabisa clinic . mwambie kuna tu DAWA rule wanatoa clinic TWA kuongeza damu na pia vinasaidia mtoto asizaliwe na uzito MDOGO pia inazuia mtoto asipate spine bifida. Matatizo ya brain na uti Wa mgongo
Alitakiwa aanze alipojigundua au kujihisi mmjamzito.
Mengi yatokanayo yatatokana na majibu ya vipimo.
 
Back
Top Bottom