Muda na vyeo ndio unawahadaa watawala wa awamu ya tano, wanadhani wanayoyafanya hayajulikani

Muda na vyeo ndio unawahadaa watawala wa awamu ya tano, wanadhani wanayoyafanya hayajulikani

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,291
Ni muda tu ndio unawapa kiburi ukichanganya na vyeo. Wanadhani wamejificha sana na pengine wanadhani wayafanyayo hayajulikani.

Kwanza hakuna jambo baya na zuri kama system. Matendo huhifadhiwa na kuwekwa rikodi. System inaendeshwa na binadamu ambao ni dhaifu vile vile.

Hawa viongozi wetu iwe kwa MAKUSUDI AU KWA BAHATI MBAYA WANAFUMBIA MACHO malalamiko tena mengine yapo kisheria na kikatiba.

Iweje leo watawala hawana habari kabisa kwamba watumishi hawajapewa stahiki zao za kisheria za kupandishwa madaraja na mishahara kila baada ya muda kwa zaidi ya miaka 3 hivi.

Iweje leo watawala kwa zaidi ya miaka minne wamezuiya mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa na maandamano halali ambayo yapo kisheria na kikatiba kama si kiburi tu na hadaa ya muda?

Iweje leo watawala wanafumbia macho wavurugaji wa haki za wananchi kwenye Chaguzi mbali mbali za marudio na ule wa Mitaa bila kuulizwa lolote kama si kiburi tu na kuhadaliwa na vyeo na muda?

Iweje leo serikali iamuwe kujitoa kwenye ile itifaki za uwazi na ukaguzi kwenye jumuiya ya kimataifa kama si nia ovu na kutaka isiwajibike? na sasa kuna huo mpango wa kutaka kujitoa kwenye Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Afrika? iweje kama si kiburi tu na nia mbaya?

Iweje srikali itumie nguvu za chama kutunga sheria ya kudhibiti habari, na kupata habari na kutumia kisingizio cha sheria hizo zilizotungwa kwa nia mbaya kudhibiti wakosoaji kama si kiburi cha watawala wakati wanajuwa KATIBA imetoa ruhusa ya kupata habari?

Kwamba kinachoendelea cha kuwatesa na kuwasumbuwa wapinzani wasifanye siasa na kukipendelea chama cha CCM wazi wazi bila kuchukuliwa hatua watendaji, kuwatesa kwa kuwakamata kupitia Polisi na Mamlaka za kiserikali nyengine eti iwe si kiburi na kuhadaliwa na muda tu ?

WASICHOJIFUNZA WATAWALA.

Hawajifunzi kwamba wao sio wa kwanza kufanya haya na kwamba wakati utawaumbuwa. Hawajifunzi somo la wakati na vyeo kuwa ni la kupita na muda utawaacha mkono baadae.

Hawajifunzi kuwa walikuwepo waliofanya haya kabla yao na historia iliwahukumu na leo tunasoma kwenye vitabu uchafu wa aina hio.

Hawajifunzi kuwa mwanadamu ana ukomo wa uvumilivu na ikifika huko hata hio sytem inayowapa kiburi huwageuka na kuanza kuwashughulikia.

Hawajifunzi kuwa Taifa linalindwa na KILA MMOJA WETU na sio system pekee yenye wajibu na uwezo wa kuilinda nchi. Nchi inalindwa na umoja wetu na mshikamano hili wanalijuwa kweli ?

Hawajifunzi kuwa nchi za wenzetu zilifanya makosa kama haya, watawala walidharau na kuyadogosha makosa yao, walijisahau kuwa makosa madogo ndio huzaa makosa makubwa na chuki hupandikizwa kwa kudharau na baadae huonekana kuwa mazoeya. Watawala hawajui kuwa watu wameumizwa kwa hii miaka minne na wana chuki wamezifundika kwenye nafsi zao. Wao wanahadaiwa na vyeo wakidhani watu wamesahau?

MWISHO.

Watawala mnayo nafasi ya kujifunza na mnayo nafasi ya kurekebisha bado. Kadiri siku zinavyokwenda ndio level ya ongezeko la tatizo inakuwa itafika wakati kujirekebisha kwenu itakuwa vigumu. Tambueni wanaoumia ni binadamu vile vile

Watawala tambuweni Watanzania wana vipaumbele vya kudumu vya umoja na mshikamano , Kamwe msithubutu kucheza na maeneo ambayo yatamongonyoa tunu hizo. Jitafakarini kama haya yanayofanywa na AWAMU YA TANO yanawakikishia WATANZANIA uwepo wa tunu hizo. Wataalamu wetu wa USALAMA fanyeni tafiti.

Tulipofika sipo mahali salama na kamwe msijaribu amani yetu kwa udhaifu wenu wa kutoona uhalisia.

MAAJABU

Maajabu ya awamu ya TANO ni kule kudhani kwamba yote yanayofanyika kwamba wananchi hawayajui, Dunia haijuwi, wasomi hawajui na kwamba eti wamejifungia kama kisiwa kwa hio watendayo eti hayajulikani.

Haya maajabu yasingemuweka Hitler kwenye kumbukumbu leo kwa uwezo aliokuwa nao.

Rejeeni makosa ya wakati na vyeo muone yalivyowagharimu waliopita kabla yenu.


Wakati wa kujirekebisha ni sasa.



Kishada.
 
Watawala wengi wanabweteka kwa kuacha kuwatumikia Wananchi

Waje Tanzania Wajifunze jinsi Rais Magufuli anavyowatumikia Watanzania

Kila kona ya nchi miradi mikubwa ya Maendeleo inafanyika
 
Watawala wengi wanabweteka kwa kuacha kuwatumikia Wananchi

Waje Tanzania Wajifunze jinsi Rais Magufuli anavyowatumikia Watanzania

Kila kona ya nchi miradi mikubwa ya Maendeleo inafanyika
Tunaiomba serikali iangalie uwezekano wa kuruhusu utoaji wa mimba ili kuepusha wazazi na aibu itakayoletwa na watoto wao wajinga
 
Hawajui kuwa watu sasa hivi wako kazini kuweka rikodi ya kila kifanywacho kwa msaada wa hio hio system ambao watawala wanaamini inawalinda.

Its a matter of Time. wao wanahadaliwa na muda na wengine wanasubiri huo huo muda ili ufike uwaumbuwe
 
Nimeshangaa sana kutumia wingi kwenye neno mtawala,aliyeikaba Kabali hii inji ni mmoja tu sio wengi,hivo ungetumia neno mtawala badala ya watawala
 
Wana macho lkn Hawaon,wana mackio lkn hawasikii wamepewa akili lkn hawazitumii ipasavyo bac hao n kama wanyama bali wao wamepotea zaid ktk njia ya haki
 
Nakubaliana na wewe muda ni rafiki mzuri....Muda utawahukumu kina Kabudi,Polepole na Wajasiliamali wa siasa...
 
Nakubaliana na wewe muda ni rafiki mzuri....Muda utawahukumu kina Kabudi,Polepole na Wajasiliamali wa siasa...
System inakuwa nawe kwa muda tu. Mambo yakiharibika tu ni rahisi kukuacha. Tatizo hatuna uhakika kama hao wanaoongoza system wanaweza kutofautisha maslahi mapana ya taifa au kikundi cha watu. Kwa mtazamo wangu jambo lolote linaloleta sintofahamu kwa wanajamii wengi halipaswi kufumbiwa macho hata kama linafanywa na wataala. huu uchafunzi wa mitaa , kuwabambikizia viongozi wa upinzani kesi ambao nao wana wafuasi wao nsi ya kuachwa bure. athari zake ni kubwa na ni hatari kwa afya ya mshikamano. Tatizo hao system ni zao la watawala na sio mfumo unaojitegemea.
 
Watawala wengi wanabweteka kwa kuacha kuwatumikia Wananchi

Waje Tanzania Wajifunze jinsi Rais Magufuli anavyowatumikia Watanzania

Kila kona ya nchi miradi mikubwa ya Maendeleo inafanyika

Maendeleo anayofanya Magufuli hayafiki hata 1% ya waliyofanya makaburu wa Afrika kidini, lakini bado weusi walitaka kuwa huru.
 
Hata sisi tulidai Uhuru kutoka kwa Mabeberu Mkuu, Mbona unajisahaulisha
Maendeleo anayofanya Magufuli hayafiki hata 1% ya waliyofanya makaburu wa Afrika kidini, lakini bado weusi walitaka kuwa huru.
 
Back
Top Bottom