RingaRinga
JF-Expert Member
- Jul 10, 2015
- 1,047
- 521
Tatizo la ajira serikalini limekuwa sugu sana.
Ajira ni mojawapo ya keki ya taifa inayofaa kufaidiwa na wote wanaostahili.
Sasa nashangazwa na utaratibu wa serikali wa kuwang'ang'ania watumishi wa serikali hadi watimize umri wa miaka 60 ya kuzaliwa.
Kuna baadhi ya kada kwa kuzingatia wingi wa mahitaji na udogo wa athari ya kustafu mapema zinafaa kurekebishiwa umri wa kustaafu.
Ntataja moja tu,
UALIMU WA SHULE ZA MSINGI
Kada hii ina wahitimu wengi sana ukilinganisha na kada yoyote. Lakini pia haina athari kubwa ikiwa watumishi wake watastaafu kwa hiari au lazima kwa umri wa miaka 45.
Hii itawapa fursa pia kutumia walichochuma kuwekeza kny ufugaji, kilimo au mambo mengine wakiwa bado na nguvu.
Sheria ya pension irekebishwe ili hao watakaohiari kutoka wakiwa na umri huo iwahusu.
Makato yao ya pensheni yanaweza kuwa makubwa ili yawasaidie wakati wowote watakapostaafu, ni swala la makubaliano tu.
Liwe ni chaguo la ama uende na mkataba wa sasa au huo mpya.
Lakini nafasi za ajira zitolewe nyingi kny mikataba ya muda mfupi.
Sidhani kwa hali ya sasa kwa vijana waliosubiri kuajiriwa kwa miaka 5 au zaidi haitawafaa.
Wengine wanalazimika kujitolea kwa kulipwa laki mbili kwa mwezi bila increment wala nyongeza.
Hii itasaidia kundi kubwa lililoko nje kuajiriwa kwa idadi kubwa kuliko ilivyo sasa.
Muda wa kusubiri ajira utakuwa mdogo ukilinganisha na sasa.