muda wa kula matunda

Acha Dhambi

Senior Member
Joined
Oct 19, 2010
Posts
145
Reaction score
41
naomba kujuzwa ni wakati gani mzuri kula matunda? Ni baada au kabla ya mlo na ni nini faida au hasara zake?
 
Ni before mlo na inatakiwa iwe @lst 1hr b4,faida zake ni kuongeza kinga za mwili na kuimarisha afya kwa ujumla
 
Kula kabla ni nzuri zaidi, ila ukila baada jitahidi angalau masaa mawili yawe yamepita.
 
Kula kabla ni nzuri zaidi, ila ukila baada jitahidi angalau masaa mawili yawe yamepita.

Kwahiyo siyo vizuri kula wali na ndizi kwa pamoja?. Najua wengi uwa wanafanya hivyo. Unakula wali kidogo uku unakata ndizi kidogo hadi unamaliza kula.
 
Kwahiyo siyo vizuri kula wali na ndizi kwa pamoja?. Najua wengi uwa wanafanya hivyo. Unakula wali kidogo uku unakata ndizi kidogo hadi unamaliza kula.

Tatizo ni kwamba chakula kinamong'onyeka taratibu kuliko matunda na ukila matunda kabla unapunguza uwezekano wa wewe kula chakula kingi kwasababu sehemu ya tumbo lako inakua imejaa tayari. Kama ukitaka kula matunda baada tu ya kumaliza kula unatakiwa ule ambayo yana enzymes zinazosaidia kuyeyusha chakula (maembe, mananasi,mapapai n.k) kuepuka tumbo kujaa gas na kujisikia vibaya.
 
Ningekushauri ule matunda katikati ya milo yako mitatu ya siku. Masaa mawili au matatu inategemea unakunywa chai saa ngapi; yaani masaa 2/3 baada kunywa chai ya asubuhi, alafu baada masaa 2/3 utakula chakula cha mchana, baada masaa 2/3 utapata matunda tena, baada masaa 2/3 utapata mlo wa jioni.

Hii tabia itakusaidia sana kuzidisha metabolism yako na kukuepusha na unene.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…