Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 8,870
- 14,258
Wafalme wa nchi zote za kiislamu ikiwemo mashariki ya kati ni marafiki wa maadui wa Mwenyezi Mungu.Wameweza kuwatawala watu wao kwa njama na ujanja ila wakati wao wa kuondolewa umefika.
Kampeni ya kuwaondoa madarakani inaonekana kama ni ndoto lakini inawezekana kwa kasi ya kushangaza na itatokea miaka sio mingi mbeleni.
Uwezekano wa aina hiyo hutokea panapokuwa na hasira za Mungu baada ya makosa ya muda mrefu waliyoyafany huku Mungu akiwaangalia tu kama wangeweza kuzinduka na ubaya wao.
Wamechangia kuuliwa kwa wingi na kulemazwa kwa wenzao wa Afghanistan,Iraq,Libya na Syria na mbaya kuliko yote hayo ni kuachia kuuliwa kwa wapalestina wanaoishi kuuzunguka msikiti mtakatifu wa Alaqsa bila kutoa upinzani wowote.
Marekani ilitamani sana kumuondoa Bashar lakini hawakuweza kufanya hivyo mpaka Mwenyezi Mungu alipowapa nguvu,,mbinu na kuwachagulia muda wasyria wenyewe kumuondoa bila Marekani kujua kitakachotokea tena kwa mikono ya mtu waliyewahi kumtangazia pesa kubwa kwa atakayemuua.
Urahisi walioupata Hizbu Tahrir ni kutokana na udhaifu walioingia Urusi na Iran waliokuwa wakimlinda Bashar Al Asad.Walikuwa wameshughulishwa na vita kila mmoja upande wake mpaka wakashindwa kumsaidia Bashar kuwapiga wapinzani wake waliokuwa wakimkaribia kwa kasi ya ajabu.
Marekani ambayo ndio mlinzi mkubwa wa wafalme wa mashariki ya kati kwa sasa iko hoi kiuchumi ndio maana inapunguza wafanyakazi mpaka wa mashirika nyeti kama ya CIA na kila siku inakatisha michango yake kwa mashirika ya misaada ya UN na ya kwake yenyewe ambayo yamekuwa kama nembo ya nguvu zake duniani kote.
Mpango uliotangazwa na Trump kuichukua Gaza na kuwahamisha wapalestina japo hautawezekana kutokana na udhaifu wa kiuchumi wa Marekani lakini ni matamshi mabaya ambayo hayapaswi kupuuzwa na yanayohitaji kujibiwa kivitendo na wafalme wote wa mashariki ya kati.
Baada ya wapalestina kuumizwa,kuuliwa na kuvunjiwa majumba yao ingepaswa jaribio lolote la kuendelea kuwaumiza lizuiliwe papo kwa papo.Ni fursa ya mwisho waliyopewa watawala hao kujitetea kwa makosa yao.
Wafalme hao wakishindwa kutumia vyema fursa yao ya mwisho basi Allah aliye na nguvu za juu atawatolea watu kama Taliban na Ahmed Alsharaa awaporomeshe chini bila uwezo wa kujitetea.
Siku hazikubaki nyingi kabla kumuona Mohammed Suleiman wa Saudi Arabia akiomba ukimbizi kwenye nchi maskini za kiafrika. Au mflame Haitham wa Oman akiomba ukimbizi nchi za Afrika Mashariki.