Muda wa kuwa juani usiishi kama vile upo kivulini, elewa nyakati

Muda wa kuwa juani usiishi kama vile upo kivulini, elewa nyakati

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
MUDA WA KUWA JUANI USIISHI KAMA VILE UPO KIVULINI,ELEWA NYAKATI ✍️

Katika siku za kuishi Duniani kwa mwanadamu kuna mpaka kufikia kifo cha asili kuna zama nyingi tunapitia ambapo zama moja inakuandaa kuishi zama nyingine inayofuatia.

Ukizembea zama moja tambua utasumbuka zama inayofuata kwa mfano Zama unayotakiwa utumie nguvu zako vizuri wewe ukipumzika tambua zama inayofuata utasumbuka kwa sababu utakuwa mwenye nguvu ndogo sasa ili kufidia itakugharimu utumie nguvu kubwa sana kufanya jambo ambalo lilihitaji nguvu za kawaida kwenye zama ukiwa na nguvu.

Umri wa miaka 45 wengi hukimbizana na shughuli za kusomesha na kuboresha miradi yao ambapo maandalizi yalianza kwenye miaka ya 20-40 hivyo kama ukicheza hapo basi utatumia nguvu kubwa sana kwenye miaka ya 45 ili kufidia uzembe uliofanya kwenye zama iliyopita.

Kila jambo likifanywa kwenye zama yake linakuwa rahisi kulinganisha na likifanywa nje ya zama zake


KIPINDI CHA KUJITAFUTA USIISHI KAMA VILE TAYARI UMEJIPATA

#Mwanasayansi Saul kalivubha
#Fikia Ndoto ZAKO
 
Uninishauri Nini kijana wa miaka 25 kutoka katika familia duni kuhusu mahusiano ya kimapenzi?? Je nijipe Muda mpaka nijipate mana binafsi mahusiano ya kimapenzi ndio yananirudisha nyuma Sana katika Maisha yangu kwasasa nipo Single kila nikijaribu kutongoza naambulia patupu

Karibu
 
Back
Top Bottom