A
Anonymous
Guest
Fremu za Tegeta Nyuki zilijengwa na wananchi wakaambiwa wachukue kodi kwa miaka 10, kisha fremu zirudishwe Halmashauri wapewe wananchi wanaohitaji kupanga. Lakini mpaka sasa miaka 10 imeisha muda mrefu. Kwa nini mpaka leo hawajarudisha fremu hizo?
Nasema hivi kwa sababu wapangaji wanaumizwa sana. Leo Halmashauri wamepita wakafunga fremu zote zinazodaiwa. Ina maana mmiliki wa fremu analipa 42,000 Halmashauri huku mpangaji analipa 200,000 kwa mmiliki.
Unakuta mpangaji analipa pesa zote kwa mmiliki wa fremu, halafu mmiliki wa fremu halipii pesa Halmashauri. Halmashauri wakija kusaka pesa zao wanawafungia ofisi wafanyabiashara huku biashara zao zinasimama mpaka yule mmiliki alipie pesa Halmashauri.
Ni usumbufu na uonevu mkubwa. Tunaomba Mkurugenzi wa Kinondoni atusaidie kurudisha fremu kwa wahusika kwani muda wao wa mkataba uliisha zamani.