Mudathir Yahaya kukosa 'Dabi ya Kariakoo' baada ya kufungiwa mechi Tatu

Mudathir Yahaya kukosa 'Dabi ya Kariakoo' baada ya kufungiwa mechi Tatu

PAYE

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2025
Posts
459
Reaction score
644
Kiungo wa Young Africans SC, Mudathir Yahaya, atakosa mchezo wa dabi unaosubiriwa kwa hamu dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Simba SC, baada ya kupewa adhabu ya kufungiwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

1776690697664.png

Mudathir amefungiwa mechi tatu na kupigwa faini ya Shilingi milioni moja kufuatia tukio la kumpiga Ibrahim Abraham wa Pamba Jiji FC wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC.

Kulingana na ratiba ya ligi, Yanga itamenyana na Simba mnamo Mei 3 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, kabla ya kucheza na KMC mnamo Mei 6 na Coastal Union mnamo Mei 9. Kiungo huyo sasa atakosa mechi zote hizo tatu.

Uamuzi huo umethibitishwa kupitia taarifa rasmi iliyotolewa na Kamati ya Usimamizi ya ligi baada ya kikao chake cha Aprili 18, 2026, ambapo kesi kadhaa za kinidhamu zilifanyiwa mapitio.

1776689203544.png

1776689210358.png
 
Hawa Bodi ya Ligi hawana tofauti na askari wapenda rushwa wa barabarani. Ni mwendo tu wa kukusanya mapato, huku matumizi ya hayo mapato yakiwa hayajulikani.
 
Back
Top Bottom