Mudathir Yahya Abbas badilika kiuchezaji

CARDLESS

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2017
Posts
7,840
Reaction score
15,918
Nimeangalia mpira wa YANGA vs USM ALGERS nikiwa home SINZA VATICAN hapa.... Sikupata fursa ya kwenda Uwanjani hasa nikijua wazi kupata nafasi itakuwa ngumu + mvua.

Kwa nilivyoungalia mchezo huu kwa kina kabisa. Wachezaji muhimu

AZIZ KI STEPHAN na KENNEDY MUSONDA + MAYELE (Hasa First Half)

Hawa wote walikuwa na mchezo mbaya mno, na hapo AZIZ KI ndio hali kwake ilikuwa mbaya zaidi.

Kwa jicho la ushabiki ni rahisi kuona udhaifu wa Aziz Ki, na nimeona hata Bandiko la Ndugu yanga Edo Kumwembe na baadhi ya wachambuzi.

Yes nakubali AZIZ KI hakucheza vizuri kabisa leo, lakini je tumejiuliza kwanini? Tumejiuliza mazingira gani alikuwa anapokea pasi? Tumejiuliza wakati upi anapewa pasi?

Mpira ni mchezo wa USHIRIKIANO, hata ikitokea MAYELE amefunga magoli 5 lakini kama DIARRA ataruhusu magoli 6 kizembe then hakuna kitu cha maana kweny hiyo mechi.

Sasa basi, leo hii game aliyeiua ni MUDATHIR, ndio kwangu mimi na hata baadhi ya watu wanaoangalia game kwa jicho la 3, watakuwa pamoja na mimi.

MUDATHIR yuko slow kwenye maamuzi, kwenye kupiga pasi, kwenye kubadili upande au kuamua twende mbele kwa wakati, tupoze au tukimbie, yeye ndiye alipaswa awe anaiamua mechi hii.

Mpira mingi iliyowafikia MAYELE, AZIZ na MUSONDA ilitoka ama kwa BANGALA au Mabeki wa Pembeni.

Mudathir anatakiwa kuwa mchezaji mwenye akili, anatakiwa ajue kukaa na mipira kunafanya mabeki wa timu pinzani kujipanga na kublock njia zote, na hiki ndicho alichokifanya leo hii. Bahati mbaya lawama zinakwenda kwa Aziz Ki, bila ya kujali usharp wake wa kufunga pindi amuonapo Mudathir awapo na mpira. AUCHO one of the best midfielder kuwahi kuwa nayo TZ, hana mambo mengi, anapokea na kuacha kwa wakati, magoli mengi ya Yanga, Build up inaanzia kwake kutoka na ubongo wake kuwa unatafsiri nafasi muhimu kwa haraka.

Muda anakaa na mipira bila sababu, na anapoachia pasi mara zote anaachia sehemu ambayo huwa ni 50/50 kwa mwenzake na Wachezaji wa timu pinzani hali inayopelekea mipira mingi kuwa blocked.

Sikuona sababu yoyote ya msingi ya kumbakisha Mudathir kwenye hii game, badala yake alipaswa kwenda nje mapema na Sureboy akae pale namba 8 ili kubalance mechi.

Kumbuka kwenye Mpira uzembe wa mtu mmoja unaharibu shepu nzima ya timu.

Muunganiko wa YANGA leo uliishia kwa Mudathir, kila akipata mpira alishindwa sasa kuuvusha na kuwafikia AZIZ, MUSONDA na MAYELE.

MWISHO KWAKO NABI.
GAME IJAYO USIJARIBU KUANZA NA MUDA DIMBA LA JUU (NO.8). HUYO MCHAZAJI UBONGO WAKE NI WA KONOKONO yuko slow sana.
Game inahitaji mtu mwenye uwezo wa kutafsiri nafasi kwa haraka sana.

Badala ya kukata matawi basi TUKATE MIZIZI ya huu uzembe.
 
Ukimsema Aziz unaonekana mchambuzi wa mchongo😅.(in edo kumwembe's.....)

Sidhani kama Nabi alikuwa mpuuzi kiasi hicho asione icho unachookiita jicho la tatu kwa dakika zote hizo 90

Azizi miyeyusho bwana😅😅😅🙌
 
Ukimsema Aziz unaonekana mchambuzi wa mchongo[emoji28].(in edo kumwembe's.....)

Sidhani kama Nabi alikuwa mpuuzi kiasi hicho asione icho unachookiita jicho la tatu kwa dakika zote hizo 90

Azizi miyeyusho bwana[emoji28][emoji28][emoji28][emoji119]
Then baada ya yeye kutoka timu ilicheza tofauti na first half?

Hakuna siku Mudathir alicheza No 8 game ikawa easy kwa Yanga haipo.
 
Ukimsema Aziz unaonekana mchambuzi wa mchongo😅.(in edo kumwembe's.....)

Sidhani kama Nabi alikuwa mpuuzi kiasi hicho asione icho unachookiita jicho la tatu kwa dakika zote hizo 90

Azizi miyeyusho bwana😅😅😅🙌
Mudathir, sure boy wapo slow kuachia mipira,yanga wanatakiwa kutafuta namba nane wa maana
 
Mudathir sio advance middle ni mzuri sana akicheza kiungo wa chini na ndio maana unaona kama anazingiua ni wachezaji wachache sana wanaweza kucheza kiungo wa chini na juu wakotea performance Ile ile kutokana na postion labda ulaya tu Kwa Africa sijaona bado izo kazi wanaziweza kina Toni kroos,Pogba Thiago alcantra n.k
 
Mudathir, sure boy wapo slow kuachia mipira,yanga wanatakiwa kutafuta namba nane wa maana
Mashabiki bwana! Wanaocheza mpira ni binadamu. Makosa ni kawaida ktk baadhi ya games. Huo udhaifu mnaouona ni kwakuwa wapinzani walikuwa bora. Acheni kuwalaumu wachezaji kupitiliza.
 
Ifike wakati mkubali kuzidiwa nyie sio wa kwanza kufungwa... USMA jana wamekaba kila mchezaji ni meyele pekee ndo alionesha kauhai hao wengine wote walipigwa pini.
 
Mashabiki bwana! Wanaocheza mpira ni binadamu. Makosa ni kawaida ktk baadhi ya games. Huo udhaifu mnaouona ni kwakuwa wapinzani walikuwa bora. Acheni kuwalaumu wachezaji kupitiliza.
Hilo siyo suala la Jana,muda na sure boy wapo slow,pia fullbacks na wingers za yanga hazitoshi kupambana champions league
 
Ifike wakati mkubali kuzidiwa nyie sio wa kwanza kufungwa... USMA jana wamekaba kila mchezaji ni meyele pekee ndo alionesha kauhai hao wengine wote walipigwa pini.
Aziz kii alipewa mzungushoo mmoja hadi alilambaa nyasi chiniii [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Komeshooo n kwa Job hadi nlimuonea huruma, anajifanyaga anajua kukabaa alipewa zungushoo hadi alingukia makalio kwa kukaa chinii ndiiiiii
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Waarabu wabayaa waleeee [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Ifike wakati mkubali kuzidiwa nyie sio wa kwanza kufungwa... USMA jana wamekaba kila mchezaji ni meyele pekee ndo alionesha kauhai hao wengine wote walipigwa pini.
Makolokolo akitoa povu hivi napata raha saaana mimi Utopolo maana miaka ya 2022 na 2023 ni 0-0 kwa kombe lolote [emoji23]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Huyu jicho lake la 3 lina makengeza sio bure mudathir kacheza vzr janA
Kacheza vizuri vipi? Yy kazi yake ilikuwa kushambulia sio kuzuia, alipaswa kusambaza mipira kwa washambuliaji, ishu mnasahau majukumu yake.

Jana aliyesambaza mipira alikuwa Bangala, which is not good. Namba 8 ndio jicho la ushambuliaji na namba 6 ndio jicho la ulinzi.

Tunapojadili nafasi, Jana Mudathir hajacheza kama namba 8, muda wote anacheza kama mzuiaji, wakati alipaswa kufungua lock, kwa pasi za haraka.
 
Naamini Aziz Ki anachezeshwa zaidi kwa shinikizo la viongozi, kocha alishamchoka kitambo tu. Na akimuweka nje mashabiki mnapiga kelele.
 
Zungukeni weeeee, Mwiaho wa siku mtasema pengo la Fei toto linaonekana na limeiathili timu
 
Mzamiru Yasin mbona unamuacha kumtaja kwa makusudi tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…