Muelekeo wa ajira na maendeleo ya teknolojia kwa miaka 10 ijayo

Bolotoba

JF-Expert Member
Joined
Apr 24, 2024
Posts
3,424
Reaction score
7,706
MWELEKEO WA AJIRA NA MAENDELEO YA TEKNOLOJIA MIAKA 10 IJAYO.

Kwa miaka takribani 10 Sasa tangu mnamo mwaka 2014 katika awamu ya mwisho ya Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete matumizi ya mitandao na TEHAMA kwa ujumla yamekuwa chachu katika kuongeza pato la taifa, naiona Tanzania yenye vijana wenye weledi, hali ya kujitegemea na kujitengenezea fursa miaka 10 ijayo hivo kupunguza utegemezi wa serikali katika sekta ya ajira. Mimi ni kijana niliyebahatika kufika ngazi ya elimu ya juu yaani shahada ya usimamizi wa biashara nimebahatika kuona changamoto kubwa wanafunzi wengi wa zama za sasa wamekuwa wakisoma programu inayoitwa "computer application" ambayo kiukweli wanafunzi wanaishia kujifunza darasani kwa nadharia zaidi kuliko vitendo hali inayopelekea kuishia kujibia mtihani lakini wanamaliza na kuingia katika mifumo ya ajira bila kujua kiufasaha kompyuta hali ambayo inapelekea kwa vijana wengi kunyimwa fursa za kazi kwa hofu ya waajiri kuwa vijana hawa wanaweza kushindwa kutumia vizuri mifumo mbali mbali ya kielektroniki. kwa maono yangu sasa yatakapofanyika yafuatayo miaka 10 ijayo yanaweza kuzalisha taifa shindani, kazi kufanyika kielektroniki zaidi na kuweza kuvumbua mifumo mbali mbali ya kiutendaji kazi endapo serikali itaweka mkazo katika maeneo haya:

Kompyuta kuwa somo la lazima
Kompyuta iwe somo la lazima na kufanyika kwa vitendo kuanzia shule ya msingi na sekondari, ambapo kwa darasa la nne kufanyika katika mtihani wa taifa, ingawa Tanzania kumekuwa na uhaba wa madarasa, madawati na pia kuwepo kwa changamoto ya umeme ukiachilia mbali ongezeko la wanafunzi endapo baraza la mitihani likiweka mtihani wa taifa utakaofanyika kwa awamu ya makundi makundi kwa vitendo kama vile inavofanyika mitihani ya vitendo ya kemia, biolojia pamoja na fizikia vijana hawa watakuwa na ule utambuzi wa kompyuta. Pia kwa pamoja wazazi na vijana kwa ujumla tubadilijitihada za kujitafutia maarifa yao wenyewe kupitia mitandao ya kijamii na tovuti mbalimbali kupitia simujanja angalau kupata ule ujuzi wa awali wa matumizi ya teknolojia ya kompyuta.

Mda wa mafunzo ya kazi kwa vitendo vyuoni uongezwe
Kwa miaka kumi ijayo kama mda wa mafunzo wa vitendo(field practical training) hautaongezwa tutegemee kuzalisha wasomi wa karatasi na kukariri masomo zaidi kuliko vitendo hivyo ubunifu mpya kukosekana. Hali inapelekea vijana wengi kukoswa fursa za kazi sababu ya kutokua na ujuzi juu ya kazi wanazoomba japo wanakwenda katika mafunzo ya kazi kwa vitendo. Kuna haja sana ya wizara ya elimu pamoja na vyuo mbali mbali kupitia sera, sheria na kanuni za mda wa wanafunzi kufanya mafunzo ya kazi kwa vitendo na walengwa wakuu haswa ni wanafunzi wa sayansi ya kompyuta, uhandisi wa umeme, uhandisi mitambo, magari pamoja na ndege wanafunzi hawa wanafanya mafunzo hayo kwa miezi mitatu mda huu hautoshelezi kutengeneza wazalishaji wazuri wa baadae na ni swala ambalo halijapewa kipaumbele Kikubwa ingawa ni kweli taasisi za kujifunzia kwa vitendo ni chache huku idadi ya wanafunzi ni kubwa zaidi, swala hili litizamwe kwa umakini kwa tija ya taifa na wasomi wa miaka 10 ijayo kutokana na kwamba pia idadi ya wasomi inaongezeka.
Kuajiriwa na kuongezwa kwa mishahara.

Wabobezi na wenye vipaji vya ubunifu, kutengeneza vifaa na vitu vya kielekitroniki wasiishie tu kufadhiliwa na kuachwa baada ya masomo kwenda kufanyia Kazi mataifa makubwa yaliyoendelea, vijana hawa wachukuliwe na waajiiriwe hapa Tanzania kwa mshahara unaokidhi thamani ya ujuzi wao ili kuwapa motisha zaidi ya kutumikia taifa letu Tanzania kwa ujuzi na ubunifu wao kama serikali itawaajiri katika vyuo vyetu hapa nchini na katika wizara za kisekta hii itasaidia kuzalisha vijana wengi wenye ujuzi kama wao hivyo kwa miaka kumi ijayo kuwa katika soko la ushindani zaidi.

Kupunguzwa kodi kwa wawekezaji
Katika kuelekea miaka 10 ijayo gharama za kodi zipunguzwe kwa wawekezaji, natizamia kusema kwamba endapo serikali itatengeneza mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji wakubwa kutoka mataifa yaliyoendelea itapendeza zaidi ikiwa ni pamoja na kutengeneza sheria itakayowapa fursa za ajira zaidi wazawa kwa asilimia 60% katika uwekezaji huo, Kimsingi ziwekwe sheria patanishi ambazo zitaleta faida kwa pande zote mbili serikali na wawekezaji katika teknolojia mfano mzuri ni taifa la Kenya wao wameruhusu muwekezaji Elon Musk kuwekeza kiasi cha dola bilioni thelathini za kimarekani mradi wake wa Starlink katika taifa hilo la kenya ambapo italeta ajira katika nchi hiyo pia kwa ujumla hii itasaidia vijana kujifunza na Kuja na vitu vipya kutoka kwa waliofanikiwa kiteknolojia huu ni mfano mzuri wa kuigwa na kuangaliwa kwa jicho la tatu. Na niseme tu kwamba si jambo baya viongozi katika sekta mbalimbali "kujifunza na kufanya baadhi ya yale mazuri" yaliyofanywa na mataifa mengine haswa katika suala la kwenda na kasi ya teknolojia. Vile vile ata baada ya wawekezaji hawa kuondoka baada ya mikataba yao kufika tamati wasiishie kuondoka na maarifa yao kuna haja ya kutunza kumbukumbu nzuri kwa namna makampuni hayo yalivokuwa yakifanya kazi na hii endapo itafanyika kwa kuwa chukua wafanyakazi wabobezi katika teknolojia waliomaliza mikataba katika makampuni hayo ili waweze kutoa mafunzo, semina na maarifa haya yapandikizwe kwa damu changa kwa hali itasaidia kuleta kizazi chenye weledi mkubwa miaka 10 ijayo.

Kuundwa kwa taasisi na tamasha la vipaji litakalofanyika kila mwaka
Ikiwa serikali itatenga bajeti na kuunda taasisi ya uvumbuzi, uchunguzi na ubunifu katika nyanja ya teknolojia kitaifa (Tanzania National innovation, research and creativity foundation, TNIRCF) ambayo itafanyika kwa Tanzania nzima angalau mara moja Kila mwaka ili kuonesha uvumbuzi, ugunduzi mbalimbali na mwisho wa siku kuwekwa katika maendelezo ya vumbuzi hizo pia wapunguziwe kodi na sheria kandamizi ambazo zinawapa nafasi wenye uwezo tu wa rasilimali fedha na kuwakandamiza vijana masikini hii itasaidia kuleta Tanzania yenye vijana wanaowaza kujitengenezea fursa za ajira kuliko utegemezi wa ajira za serikali kwa miaka 10 ijayo.

Mwisho wa yote, katika safari ya kuelekea miaka 10 ijayo napendekeza serikali kupunguza bajeti katika matumizi yao angalau asilimia 40% haswa katika ununuzi wa magari ya serikali kwa ajili ya watendaji mbali mbali, badala yake fedha hizo zielekezwe Katika miradi ya maendeleo haswa mikopo ya vikundi kwa vijana ili kusaidia vijana kujikwamua kiuchumi.

Mawasiliano
Namba za simu:0627635212, email:adrianalexnjile@gmail.com.
 
Umetoa mchango mzuri sana wa mawazo! Nashauri serikali yetu iuchukue na kuufanyia kazi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…