Muendelezo wa Masoko Kuungua ni Sahihi kuwa Bado hatujapata Suluhisho?

Muendelezo wa Masoko Kuungua ni Sahihi kuwa Bado hatujapata Suluhisho?

Mdundwa

Member
Joined
Dec 5, 2018
Posts
19
Reaction score
28
Siku za hivi karibuni kumekuwa na Ongezeko na kasi isiyokawaida ya Kuungua kwa Masoko Nchini hasa Nyakati za Usiku Jambo linalozua Maswali mengi zaidi.

Sio kwamba kama Nchi ndio tumeanza kupata kuyaona Majanga haya kwa Mara ya Kwanza hapana, yamekwisha kutokea huko Nyuma lakini mtindo ndio unaoleta utofauti na Maswali, Matukio ya Sasa yanafanana na kufuatana, Tulianza na Tukio la Kariakoo, likafuata la Karume, Kule Mwanza, Pale Mbuyuni Moshi na Sasa tena Mbagala haya yote yameungua kwa Nyakati Moja yaani usiku pekee, swali kwanini Usiku pekee?

Zimekuwa zikundwa Kamati kuchunguza na kuripoti, zipo ripoti tumewahi kuambiwa ya Kama ile ya Karume na Mshumaa wa Mateja lakini pia mpaka sasa Jamii hajaelezwa juu ya Uchunguzi wa Soko la Kariakoo, lakini Kamati ilipeleka ripoti yake, Sasa kwanini hawaweki wazi kama hizi nyingine?

Je, tutaunda Kamati kila Mara kwa matukio yale yale yenye kufanana kwa Matukio na Nayakati? Hizi Kamati si hutumika gharama kuzianda na kufanya Uchunguzi wake? Vyombo vya Dola si vina interejensia yake ya kufuatilia jambo kabla na baada? Kwani kipi kilichobora tuzibiti yasitokee au tusubir yatokee tuunde Kamati tuchunguze? Kama ni Watu (Kama inavyosemekana mtaani) wako Nyuma ya haya Matukio, ni kwamba Vyombo vya Usalama vimeshindwa kuwatambua na kuwadhibiti?

Je, Wafanyabiashara hawa wataendelea kupata hizi Hasara hadi lini? Kuna Mkakati gani wa kuyadhibit haya yasitokee tena?

Binafsi Naamin, Serikali ni kubwa na inamkono Mrefu (kwa Imani) haiwezi kushindwa kwani haikuwahi kushindwa na haitashindwa kufuatilia na kuyadhibit Matukio haya yasitokee tena, Kwani wanavyovyombo vinvyoweza kufanya hivyo, sitaki kuamini kuwa Matukio ya Moto yanavizid Vyombo vyetu vya Usalama na Weredi, Kama Vyama vya Siasa wakitaka kufanya Mikutano huzuiwa kwa kuwa kuna taarifa ya uhalifu unaoweza kutokea, sidhani Kama watashindwa kudhibiti Majanga haya tena, Mkuu wa Mkoa wewe ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Jukumu lako ni kuhakikisha Watu na Mali zao wanakuwa Salama, Mpaka sasa kwenye Mkoa wako zaid ya Maelf my Wafanyabiashara wa Masoko ya Kariakoo, Karume, Mwenge na Mbagala mali zao zimeteketea, Wamepoteza Mitaji na kupata hasara, Tumia Vyombo vyako vya Usalama kudhibiti haya Matukio.

Ahsante.

Pia soma: Soko la Kariakoo lateketea kwa moto
 
Back
Top Bottom