Mufti Abubakari Zuberi ahimiza uharaka kesi ya mashehe wa Uamsho

Ulitaka aingie kwenye mzozo na serikali halafu mwisho wake utakuaje? huko jela kuna zaidi ya masheikh 170 ukiacha hao uamsho na kesi ni hizo hizo tu za ajabu ajabu wanapewa.
Hakuyasema haya wakati wa kipindi cha mwendazake na alikua very close naye,why now?President Samia ni msikivu mno but NOT take her for fool or granted,sheikh mkuu asimpe unnecessary pressure,alikua in a good position kuongea na mwendazake na hakutake advantage hiyo kwa uoga wake,aache unafiki now President Samia katupa uhuru wa kuongea na tuutumie vema otherwise she can silence all of us
 
Asingeongea mngemuhukumu.

Ameongea mmemuhukumu


Mnataka afanyeje?
Sheikh Abubakr Zuberi ni mnafiki kiwango cha Tanzanite. Yeye ndiye alikuwa anamsomea Dua Mwendazake kila akianguka. Miaka yote 5 hakuthubutu kumuomba mgonjwa wake Magufuli awaachie hawa Mashehe au kushinikizwa kesi isikilizwe.

Ameona mchakato unarndelea, kaamua kudandia treni kwa mlango wa Dreva. Ni MNAFIKI TU
 
Wamuache mama aamue inavyofaa maana for 5yrs hamkupigia hizi kelele yule jamaa na hata kule nyuma kwa JK hamkumpigia kelele pia...leo mnataka mvimbishe vifua kwa mama....enzi za yule jamaa mlikuwa busy kwenye zinduzi, tafrija nk.....tusimsumbue mama, tumuache huru afanye sehemu yake naye kadili atakavyojaaliwa na mwenyezi Mungu mwingi wa rehema....
 
..Wazungu wana msemo wao , " too little too late. "

..Mufti amechelewa mno kulizungumzia suala la Mashekhe wa Uamsho.

..Vilevile kauli ya Mufti ina msaada kidogo sana kwasababu imechelewa kutolewa.
Lakeni hao hao wazungu wana kamsemo kangine kanasema better late than never. Kwahiyo Mufti atakuwa kakafuata hako kamsemo!
 
Dini Hizi zimegeuka kuwa sehemu Ya fursa tu...Hawa wanaojiita Viongozi wa Dini wote wanajulikana mambo yao..Jamii wala haiwaheshimu hawa..
 
Lakeni hao hao wazungu wana kamsemo kangine kanasema better late than never. Kwahiyo Mufti atakuwa kakafuata hako kamsemo!

..wazungu pia wana kamsemo, " justice delayed is justice denied. "

..mashekhe wamekaa mahabusu muda mrefu sana.
 
Hivi alikua wapi enzi za mwendazake, hakuwahi hata kuwataja masheikh wa uamsho
 
Huyu mnafiq alikuwa wapi siku zote?
 
Mnafiq sana huyu Sheikh Ubwabwa
 
Haya sasa Farid na Mselemu wameachiwa baada ya DPP kuwafutia mashtaka. Huu ni mpango uliopangwa na serikali kuonyesha kuwa inaheshimu mawazo au hoja za viongozi wa dini!
 

Wee ngoma ya Isoko. Tayari kule wameshatolewa. Wako huru mtaani.
 
Wee ngoma ya Isoko. Tayari kule wameshatolewa. Wako huru mtaani.
🤣🤣🤣 Niliona dalili! Serikali na BAKWATA wanavyotuchezea akili, yaani serikali inaitaka BAKWATA itoe tamko ikiwa tayari imekwishaamua kuwaachia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…