Mufti Abubakari Zuberi ahimiza uharaka kesi ya mashehe wa Uamsho

🤣🤣🤣 Niliona dalili! Serikali na BAKWATA wanavyotuchezea akili, yaani serikali inaitaka BAKWATA itoe tamko ikiwa tayari imekwishaamua kuwaachia!
Hahahaahaa hata mimi nilishtuka. Ndo Utajua ni kias gani BAKWATA wako "well connected"
 
Yaani Bakwata inatoa tamko tu watu wanaachiwa,

Naiona hatari ya mambo kama haya kama taasisi za kidini zinakua na nguvu namna hii katika mihimili yetu ya dola.

Tunatengeneza mfumo ambao kila dini itakua inapambana kuweka viongozi wa juu wa nchi ili kunufaika na mfumo.
 

Unafiki tu anataka kuchukua credit sasa, huyu alikuwa wapi miaka yote mbona hatukumsikia akiongea na Mwendazake, wakati siku zote walikuwa wanakutana kwenye mialiko mbali mbali.

Hongera Mama Samia.
 
Baada ya kugundua kuwa DPP amesha sain hati ya kuwafutia mashtaka watuhumiwa kilichobaki ni utekelezaji (kuachiwa) ndio unaamua kujitokeza kuomba swala la masheikh lifatiliwe! Kipindi chote ulikuwa wapi kusema? ulimuogopa nani na ulichoogopa hasa ni nini? na kama uliamua tu kukaakimya kwanini uliamua hivyo? Na kinachokufanya useme sasahivi ni nini? Kwani ungeendelea kukaakimya nini kingetokea?

Wakati wafuasi wako team Bakwata wakimshambulia sheikh Ponda Kwa issue hii ya kuachiwa Kwa hawa masheikh mbona hukujitokeza kutoa neno juu ya msimamo wako? Walichokuwa wakikisema wafuasi wako dhidi ya sheikh Ponda yalikuwa ni maelekezo kutoka kwako?

Katiba ya Bakwata inapaswa kufanyiwa marekebisho huu utaratibu wa Muft kutawala mapaka kifo uondolewe.

Uongozi ni uwajibikaji, hatuwezi kuwa na kiongozi ambae kazi yake ni kutangaza mwezi na kuomba dua kwenye majanga na sherehe za kitaifa, huku maadili kwenye jamii yanaporomoka, watu wanadhulumiwa haki zao, hakuna hospital, hakuna shule (madrasa) Migogoro ya miskiti mingi chanzo ni Bakwata, hata wanapopatikana wafadhili kujenga chule, hospital au mskiti mnawaletea zengwe wanaondoka, wale wanaoamua kufanya ufadhili mwisho wa siku mnageuza huo ufadhili kuwa vitega uchumi vyenu.

Nyumba za waqfu mmezigeuza vitega uchumi, watu mpaka wamekuwa wazito kutoa zaka maana wapokeaje (wasimamizi) ni nyinyi ili muwafikishie walegwa (jamii) Kwa utaratibu maalumu, matokeo yake nyinyi ndio mmekuwa wadau No1 kanakwamba hakuna wakundi mengine.

Badirikeni acheni mazoea.
 
Alikuwa wapi kipindi cha nyuma badala ya kusubiria movie iishe ndipo atoe sauti
 
msumari wa mwisho kabisaa katika jeneza.
 
..Nadhani Mufti " alitonywa " kuwa serikali inatarajia kuwaachia huru Mashekhe wa Uamsho, ndipo na yeye akajitokeza kuigiza kuwatetea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…