The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Sheikh Mkuu na Mufti wa Tanzania, Sheikh Dkt. Abubakar Zuber Bin Ally ametumia mashindano ya kusoma na kuhifadhi Qur-an Tukufu kumuombea msamaha mwalimu wa Madrasa, Mussa Bashiri, aliefikishwa mahakamani akikabiliwa na mashtaka ya kuwafanyia ukatili wa kuwachapa viboko watoto wawili wenye umri wa miaka 6 na 9 na kuwasababishia madhara.
"kiukweli nilisikia kuna mwalimu wa madrasa amefikishwa mahakamani kwa kosa la kuchapa watoto wa madrasa hivyo nitumie nafasi hii kuwaomba wazazi na umma wa Watanzania msameheni tuchukulie alipitiwa lakini nitoe wito kwa walimu wote kuacha kuwa wakali kwa watoto wa madrasa hata hivyo sisi kama mabaraza la Waislamu tumekuwa tukitoa semina kwa walimu kuhusu namna yakuwafundisha watoto wetu"~Abubakar zuber mufti wa Tanzania