Mufti ataka Waislamu kuwekeza katika elimu zaidi

Status
Not open for further replies.

Huyu sheikh Mufti tunamjua kwamba ni moja ya idara ya serikali inayowakilisha mtazamo wa serikali kuhusu waislamu. wewe pamoja na mufti nawaomba niwaulize :-

a. Utaendeleza shule kwa michango ya waumini? Ni kiasi gani unataka walipe kama waislamu kuchangia elimu ya watoto wao?

b. Kodi na vifaa vya endeshaji pesa utazipata wapi?

c. Uwezo wa kifedha kwa waislamu wengi unajulikana ni wa kusikitisha kama sio kuhuzunika (Kwa ufupi wengi ni maskini) sasa hizo pesa za ujenzi wazitoe wapi wakaibe???

d. Sawa tunaweza kupata ufadhili wa kujenga shule kutoka kwa waarabu au matajiri wa kiislamu nchini? Ila kama ilivyo misikiti mingi Tanzania kuendesha misikiti na mashule sio kama kuiendesha nyumba yako Mtu wa Pwani ni kwamba inahitajika a stable working capital kuhakikisha msikiti au shule inaendeshwa kwa umakini.

Hivyo ijapokuwa umesoma fikiria vilevile waislamu hawalalamiki kama wajinga bali to promote fairness na equality the government needs to subsidies them. MOU ya Kanisa na Serikali ndio iliyoleta shule nyingi za wakristo, kama mnakumbuka shule za seminari ziliibuka kama uyoga miaka ya 90s. Sasa jiulize kwanini, siamini na kwasababu najua kuwa si michango ya waumini pekee imechangia kukua kwa hizi shule bali na kwa msaada wa serikali pia.

Nyerere anachukiwa na waislamu kwasababu mojawapo ya sababu alichangia kwa kiasi kikubwa kuvunjika kwa EAMWS. EAMWS ilikuwa ni jumuiya yenye kuwaunganisha waislamu sunni, shia, ismailiya na wengineo kwa lengo la kuwaendeleza waislamu kielimu. Kumbuka kipindi kile waislamu wengi walikuwa ni wafanyabiashara ya kilimo, utumwa, meli waliona kuna haja ya jumuiya ya kiislamu nayo iendelee kielimu. Hivyo basi wakawa wameanzisha jumuiya hiyo kuleta maendeleo kwa waislamu. Vilevile kumbuka kipindi cha miaka 1945 wakoloni walikuwa wakifanya kazi kwa kupitia missionaries kusambaza dini na elimu. Waislamu walikuwa wanatakiwa kubadili dini ili waweze kusoma shule za wamisionaries (kama huamini waulize watu kutoka Tanga babu zao na bibi zao watakuambia ndio maana Tanga utakuta mtu mdogo wake muislamu kaka mkristo na kuendelea).

EAMWS ilikuja kama mbadala wa wamisionaries kwani ilikuwa na network Tanzania nzima kupitia waalimu wa vyuo,tariqa na jumuiya za kiithnasheri ambao walitapakaa Tanzania nzima. Hivyo wakaweka mikakati ya kuwa na elimu ya kidunia na ya kidini ili kuwanyanyua waislamu ambao wengi walikuwa hawapati huduma kutoka shule za missionaries. Mikakati hii ilifanikiwa na mwaka 1964 Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan Bin Ameir Al-Shirazi alienda Lebanon, Egypt, Iraq, Syria na kufanikiwa kupata grant ya karibu pound milion 55 za kiegypt wakati ule kuja kuanzisha CHUO KIKUU cha kwanza Tanzania. Ilipofikia hapo Nyerere akaona ni tishio na vilevile tishio kwa wakristo kwa vile waislamu wataanzisha chuo kikuu.

Hivyo basi tunaifahamu wengine vizuri Bakwata na ni bora tu tuiache itangaze inavyojisikia ila inajulikana kama taasisi ya serikali kwani akina Sheikh Abdallah Chaurembo, Sheikh Adam Nasibu, na wengineo wengi kwa msaada wa serikali (kwani serikali iliwaona ni waislamu walioelimika mpaka wakasifiwa katika magazeti ya Uhuru na Radio Tanzania) ndio walioshiriki kuiua hii jumuiya.

Hivyo Mtu Pwani soma historia vizuri kwani through history you can define your future. Usifikirie waislamu wanalalamika tu kama wendawazimu, chunguza kwanza.
 

Kwa wenye akili watapaza sauti ya Sheikh, that is smartest thing Sheikh has said.
 
kuna mengine kwa kweli wala hayana uonevu wowote ni sisi wenyewe tuache kulalamika.
 
Kuna ka uongo mwandishi hapo juu kaandika.

Waislaam inawezekana hawana shule wengi ila kwenye biashara wao ndiyo wametawala.

Waislaam wengi ndiyo wenye hela nzuri na mitaani wengi tunapanga kwenye nyumba zao.

Sasa kusema ETI HAWANA HELA, mhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!

Waanze tu kujifunza kuzipanga vizuri hela zao. Ila kwa hela, wao ndiyo wako juu ya WASTANI.

Ukichunguza watu wenye maisha ya wastani, wengi ni WAISLAAM.
 

Mkuu nadhani unawazungumzia waislamu wa mijini. ukienda vijijini mkuu ni aibu hali ya maisha ni mbaya sana. Kuna msikiti mmoja nilienda vijijini huko nikakuta wameufunga na kufuli kwasababu wameshindwa kuuendesha. sasa uwingi wa waislamu unaosema wewe hebu fafanua zaidi.
 

ni kweli kabisa sisi waislamu inabidi tubadilike badala ya kuendelea kulalamika kwa kuwa haitotusaidia lolote!!
 
ni kweli kabisa sisi waislamu inabidi tubadilike badala ya kuendelea kulalamika kwa kuwa haitotusaidia lolote!!

Hebu tuanze mimi na wewe kwa kujiuliza ni kiasi gani tumetoa kusaidia waislamu?
 
Utaendesha shule kwa nguvu ya gesi only a fool will agree with what Sheikh has said!!!

Mkuu i would like to believe that only a foll will disagree with Sheikh. Kukazania elimu means that you have to do what ever you can to be educated. Kama ukitegemea misaadam kutoka nje ya nchi ndio usome, unaweza kusubiri kwa miaka mingi sana. I believe Sheikh has seen what is happening on the ground. By the way ametoa wito tu, wataoitikia waitikie watakaoona haufai na wauache.
 
Katika harambee hiyo jumla ya shilingi milioni17321300, zilikusanywa, fedha taslimu zikiw a milioni 4881300 na milioni 12,404,000.
Im shocked with the figure huyu mwandishi arekebishe namna ya kuandika hiyo figure ni pesa nyingi sana kwa uandishi huu
 

Mdondoaji,

..binafsi naamini Waislamu wangejikita zaidi kwenye QUALITY na siyo QUANTITY.

..inawezekana kabisa kwa kutumia resources za ndani, matajiri wakubwa Waislamu, kuanzisha walau shule 6 as centers of excellence. hiyo iwe short term measure ya kujenga uwezo wa kuanzisha na kuhudumia shule nyingi zaidi.

..labda hata taasisi za Kiislamu zingeachana na miradi mingine yote ya kijamii kama huduma za afya na zahanati, na kujielekeza kwenye ELIMU peke yake.

..vilevile badala ya kuipiga vita Bakwata angalieni uwezekano on how best it can be used to serve the Muslim community. nimewahi kusikia kwamba Bakwata wana mtandao nchi nzima unaofika mpaka wilaya na hata kata.

..pamoja na historia yake ambayo Waislamu wanaona ina walakini, lakini it is better kusahau yaliyopita, na kuangalia jinsi gani Bakwata inaweza kuboreshwa na kuwezeshwa.

NB:

..siyo kweli kwamba MOU ndiyo imewezesha makanisa kujenga shule nyingi zaidi.

..kilichotokea ni kwamba serekali ya Mzee Mwinyi ilifungua milango ktk masuala mengi ikiwemo hili la utoaji elimu.

..kama huna habari Mwalimu alipiga marufuku waalimu toka nje kufundisha ktk shule za msingi. hilo lilikuwa pigo la kwanza ktk shule za makanisa ambazo nyingi zilikuwa zinaaza na primary schools. baada ya hapo likafuatia zoezi la kutaifisha shule binafsi na shule za madhehebu ya dini.

..kuna shule nyingi sana za Kanisa ambazo zina mazingira mabaya, zinatoa elimu ya kiwango cha chini na kufanya vibaya ktk mitihani ya taifa. mara nyingi ubora wa shule za kanisa uko directly related na uwezo wa kifedha na kitaalamu wa shirika la kidini[maryknoll,white fathers,capucini,...] linalofadhili shule husika. kama MOU ingekuwa inazibeba shule hizo basi kusingekuwa na academic disparity katika shule za makanisa.

..kwa upande mwingine ni kitu gani kinazuia taasisi za Kiislamu kusaini MOU na serikali ili mpate ushirikiano kama ule wanaopata taasisi za Kikristo? Waislamu sasa hivi wanahitaji viongozi/activists ambao wanaweza ku-negotiate na serikali na siyo kuilalamikia na kuishutumu siku zote.
 
Naunga mkono kauli ya Shehe mkuu sio yule wa kambi isiyo rasmi (Basaleh) ambaye kazi yake kubwa ni kulalamika tu na kupandikiza chuki dhidi ya ukristu.
Waislamu wenye akili tafakarini kisha chukueni hatua.
 

Mkuu,

Personal effort ni muhimu kufanikiwa kimaisha hakuna mtu atakuletea maendeleo. Ila waislamu usifikiri wamebweteka hawajihangaishi. Kumbuka kama nilivyokuambia zamani wazee wa kiislamu walikuwa wakipeleka watoto wao shule za wamissionaries wakaambiwa lazima wawe wakristo. Sasa hilo likawa kikwazo kwao. Kwanini Nyerere kama kweli alikuwa mwadilifu asiwaruhusu waislamu wawe na wao na jumuiya za kimissionaries za kwao?

Ni kweli umesema Sheikh ametoa wito lakini asiseme waislamu wanalalamika kwani kuna mambo yako nje ya uwezo wa waislamu kukwamuka kielimu na kimaendeleo. Mfano Bakwata kulikuwa na ufisadi wa kutisha huyu sheikh alikuja kubadilisha mazingira hayo mazingira na kuweka mambo katika mipangilio ya kueleweka (hapa nampa pongezi). Ila shule, zahanati zinahitaji msaada wa waislamu na serikali kwa pamoja. Either mmoja asaidie kuanzisha au asaidie kuendeleza venginevyo inakuwa ngumu.
 
Mi nadhani pia miongoni mwao hawaambiani ukweli, kuna baadhi yao walienda kusoma shule za seminari wengine hata majina walibadili ili wasigundulike na walipomaliza elimu walipata kazi nzuri sana serikalini, sasa sijui kwa nn hawakutaka kuwaonyesha njia wenzao au wao kuwa chachu ya kujenga na kuendeleza elimu dunia kwa sana. Heko Mufti kwa kujitoa kimasomaso.
 

Mkuu ,

Ushauri mzuri ila Quality huja baada ya kuweka misingi mizuri mie nafikiria kwanza waanze na quantity ili waislamu wengi ambao hawajapata the so called elimu dunia wasome. Zijenge shule nyingi za kisecular waislamu wasome kwa wingi zaidi kupunguza wingi wa waislamu wasiosoma (kumbuka haya pia yalikuwa malengo ya EAMWS). Quality itafuata halafu baada ya kupata vijana wengi waliosoma.

Kujenga shule sio kazi Joka Kuu bali kuendesha shule ndio kazi ndugu. Fikiria shule mmoja ya msingi ina waalimu kama 100 kila mmoja analipwa mshahara wa laki 4 tuseme, hiyo ni jumla ya milioni 40 kwa mwezi, na jumla ni milioni 400 kwa mwaka. Sasa serikali inaweza kutusaidia kuwalipa mshahara walimu (kama walivyofanya katika ile MOU na kanisa ili kuweza kusomesha vijana shule). Ila litasaidia sana.

Umepinga kuwa ile MOU ya Kanisa haijachangia kustawisha shule za kanisa na hospitali, nikuulize shule za seminari zimeanza kustawi lini? Mzee mwinyi ndio alifungua uhuru wa kutoa elimu Lowassa akatumia kigezo hicho kuomba msaada wa serikali kusaidia katika kutoa elimu katika jamii. Sasa sio wazo baya ila figures zinazoonyesha shule za seminari zilikuwa kama uyoga miaka ya 90s.

Disparity ya kutoa elimu unaweza kuwa uko sahihi inatokana na utoaji wa elimu wa shule husika, mazingira na elimu hilo silikatai. Ila vilevile shule nyingi za seminari haziperform vibaya kama shule za serikali na shule za kiislamu. Mfano mmoja katafute matokeo ya shule ya Al-Haramain, Kinondoni ni aibu tupu kuyasema sasa kuna matatizo ya watoto wenyewe kutokusoma au uzembe but pia uendeshaji wa shule, kukosekana vifaa na ukata unachangia pia. Ukienda Al-Haramain kumezungukwa na maduka siku hizi imekuwa ghetto pale. Kinondoni pia jiulize mazingira yale mtoto atafaulu kweli??? Think mkuu think!!!
 
Naunga mkono kauli ya Shehe mkuu sio yule wa kambi isiyo rasmi (Basaleh) ambaye kazi yake kubwa ni kulalamika tu na kupandikiza chuki dhidi ya ukristu.
Waislamu wenye akili tafakarini kisha chukueni hatua.

kambi isiyo rasimi.duh anafukuzia Kadhi mkuu,njaa izi bwana
 

Mdondoaji,

..naona hili suala la MOU umeamua kulipotosha kwa makusudi.

..majadiliano ya MOU yalisababishwa pamoja na mambo mengine, hali mbaya ya shule na hospitali za Kikristo zilizokuwa zimetaifishwa. serikali ndiyo iliyo-approach mashirika ya kidini and not vice versa. pia mchakato wa MOU ulihusisha mpaka ofisi za ubalozi mfano Ujerumani, sasa hebu jiulize kwanini?

..suala la MOU ni pana na lina sababu zake za kihistoria. I am disspointed msomi kama wewe unapolizungumzia in a simplistic way kama wakina Maalim Basalehe na wenzake.

..kwa taarifa yako mchakato wa MOU ulianza wakati Anna Makinda akiwa ni waziri wa nchi ktk ofisi ya Raisi. Edward Lowassa alikuja kumpokea wadhifa huo na ndiyo maana unaona amesaini kwa niaba ya serikali.

..pia MOU imesainiwa wakati Raisi ni Muislamu, Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu, Waziri wa Fedha Muislamu, Waziri wa Afya Muislamu, Katibu Mkuu wizara ya Elimu Muislamu. pia suala zito kama hilo lazima lipitie vikao vya baraza la mawaziri.

..yeyote yule anayedai kwamba suala hili lilifanyika kwa "kificho" au "ghiliba" au "kutumia upenyo" anakuwa hatendi haki kwa kilichotokea.

..kuna hospitali na shule za Kanisa zina umri wa miaka zaidi ya 50. sasa wewe unadai zote zimeanza wakati wa Mwinyi baada ya kusainiwa MOU in 1992.

..leo hii kuna Hospitali zilizojengwa na Kanisa na kukabidhiwa kwa serikali na tayari zimeporomoka na kuwa na hali mbaya.

..kwanini serikali inashindwa kuendesha shule ilizotaifisha kama Pugu[St.Francis] na Minaki[St.Andrews]? katika mazingira hayo una uhakika kwamba shule za kanisa zinazong'ara ziko hivyo kutokana na msaada wa serikali na siyo michango ya waumini na mashirika wafadhili ya Kikristo?
 

Mkuu kuna mambo na mipaka ya waziri, Rais, katibu kata. Unapodai MOU hii ilisainiwa na Waziri Lowassa, na Rais Muislamu, Mkuu wa Usalama wa Taifa Muislamu hebu tupatie evidence kama kweli wamesign. Au nawewe unakuwa kama jamaa mmoja anayejiita katibu TEC. We are anxious to know what realy went there!!!!.

Mkuu kuanzishwa tangia zamani hakumaanishi ndio zitolewe favourable terms from the government JK. Kumbuka hawa viongozi walitakiwa wawe na weledi wa kujua hii nchi ina waislamu, wakristo, wapagani, wahindu sasa tukisema tuwape favorable terms wakristo tu wahindi nao wasemeje? Unadhani zile shule za upanga, muhimbili na kisutu walijenga serikali? Wamejenga wahindi kipindi cha mkoloni sasa basi nao wapewe favourable terms kusaidia jamii.

Mkuu huwezi kuepuka kwani data zinaonyesha hizi seminari zilishamiri miaka ya 90 sasa kama MOU ilisaidia au la nakuachia wewe umalizie ila sidhani kama ni mada. Swala ni je huyu mufti anachokisema kina msingi.

Binafsi silaumu kila kitu serikali ni vema waislamu nao wakawa na moyo wa kusaidia. Kuna waislamu matajiri mno Tanzania ila utajiri wao unatumika katika siasa, kujionyesha, kuhonga akina dada, na ni wachache sana hutumia utajiri wao kuendeleza jamii. Vile vile jamii za kiislamu ni vema zikawa na mwamko wa kusoma kwa serikali haitaweza kufanya kila kitu. Sio lazima aje tajiri kuja kusaidia waislam, wenyewe kwa wenyewe wanaweza kuchangishana kufanya kitu cha msingi. Ila jambo moja waislamu linawarudisha nyuma nalo roho ya kutoa, yaani wengi wana roho ya kwanini nitoe mie sasa mioyo ya kutoa hawana.

Hivyo JK silaumu kila kitu serikali ila there is a share serikali lazima ibebe katika haya mambo kwani ile divide and rule iliyoanzia kipindi cha nyerere inaendelea mpaka sasa.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…