Mufti Mkuu asema "Punguzeni dhambi mvua zinyeshe"

Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaasa Watanzania kupunguza na kuacha kabisa kutenda dhambi na badala yake wamrudie Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na adha ya ukame ulioikumba nchi. Amesema kukosekana kwa mvua, uwepo wa ukame na kukauka kwa maji ardhini ni ishara kwamba watu wanatenda maasi.

Hata hivyo mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuwa ni sababu ya ongezeko la joto, mvua zisizotabirika pamoja na ukame. Mufti ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 5, 2022 alipokuwa akiongoza dua maalum ya maadhimisho ya miaka 26 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

“Tunapoomba mvua tuendelee kuacha maasi na mambo mengine yasiyofaa, watu waache dhuluma, mambo mabaya yanayosababisha sisi Mwenyezi Mungu atunyime mvua,” amesema Mufti Zuberi. Amesema tayari viongozi wa dini wameanza kuomba dua kwa ajili ya kuiombea mvua.

“Mwenyezi Mungu atuletee mvua yenye kheri isiyo na maafa kwetu Tanzania na nchi zingine zilizopakana na sisi. Tunajipanga kuomba dua kwa Watanzania kwa ujumla na wenzetu wengine watafanya dua siku ya Jumatatu.

“Wananchi wote kila mmoja kwa nafasi yake aombe dua ili tupate mvua isiyo na maafa tushirikiane katika kumuomba Mwenyezi Mungu hii itakaribisha baraka na itatuondoshea huu wasiwasi viongozi wote wa dini, mashekhe wote tushirikiane,” amesema Mufti Zubeir.

Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Denis Bwigira amesema Mungu amejalia vitu vingi vya asili binadamu aweze kuvitumia kwa akili lakini wakati huu kwa pamoja viongozi wa dini wapo katika kuomba kwa sala makanisa yote.

“Naamini kutakua na maombi ya kitaifa. Tanzania tuna utajiri mkubwa wa maji ardhini na kwenye maziwa tumuombe Mungu atuzidishie uwezo wa kiteknolojia tuvute maji yaliyopo ardhiri tunaamini Mwenyezi Mungu hawezi kutuacha tuangamie kwa kiu,” amesema na kuongeza;

“Tunaamini tutapata maji ya kutosha na hii itukumbushe tunapo mtumainia Mwenyezi Mungu kuna njia za kujiwekea imani ya kuwa makini kwa majanga mbalimbali.”

Sala hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za tiba pamoja na viongozi wa kidini ambao kwa pamoja wameitaka taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa upendo, na kufuata maadili ya utumishi wa umma.

MWANANCHI
Mwenyezi Mungu atunusuru na balaa hili la viongozi wa awamu ya tano kipindi Cha mpito.
 
Madhara unayoona leo yaliongelewa sana na watu wa mazingira lakini wakadharauliwa, watu wanakata misitu wanapanda mazao, moshi wa viwanda

Rate ya deforestation ni 10 million hectares per day

Kila mwaka sehemu ukubwa wa Portugal linakatwa miti

Kiwango cha bafafu kuyeyuka kinaongezeka, kina cha maji baharini kinaongezeka, ocean currents zinabadilika

Haya ni matokeo ya uharibifu wa muda mrefu,

mvua zipo lakini majira yamebadilika. Inaweza kunyesha mvua kubwa moja ikaharibu na isirudi tena.

Bado kuna vichwa maji watakuambia tumuombe Mungu, Mungu anahusikaje?
Akili ndugu yangu, akili!
 
Mashekhe waache kula kiboga kwanza, na pia waache kumfananisha Mwanasiasa na Mungu.
 
Mufti watu wameanza kutenda dhambi mwaka huu?
 
Hali ya hewa ya Dunia inaendana na Kanuni.
Usipo fata Kanuni unavuruga mzunguko wote.
Mfano tuu..Uwaribifu wa vyanzo vya maji.
 
Mimi kama Muislam ambaye Dini yangu inanifundisha kwamba dhambi huondoa baraka na kusababisha majanga na matatizo nimemuelewa Sheikh Zuberi (Allah amuongoze yeye na sisi). Ila ndio hivyo watu wanaleta ujuaji mwingi, wanajifanya wasomi sana nk.
 
30_41.gif

41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu

(Qur'an 30:41)
 
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaasa Watanzania kupunguza na kuacha kabisa kutenda dhambi na badala yake wamrudie Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na adha ya ukame ulioikumba nchi. Amesema kukosekana kwa mvua, uwepo wa ukame na kukauka kwa maji ardhini ni ishara kwamba watu wanatenda maasi.

Hata hivyo mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuwa ni sababu ya ongezeko la joto, mvua zisizotabirika pamoja na ukame. Mufti ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 5, 2022 alipokuwa akiongoza dua maalum ya maadhimisho ya miaka 26 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

“Tunapoomba mvua tuendelee kuacha maasi na mambo mengine yasiyofaa, watu waache dhuluma, mambo mabaya yanayosababisha sisi Mwenyezi Mungu atunyime mvua,” amesema Mufti Zuberi. Amesema tayari viongozi wa dini wameanza kuomba dua kwa ajili ya kuiombea mvua.

“Mwenyezi Mungu atuletee mvua yenye kheri isiyo na maafa kwetu Tanzania na nchi zingine zilizopakana na sisi. Tunajipanga kuomba dua kwa Watanzania kwa ujumla na wenzetu wengine watafanya dua siku ya Jumatatu.

“Wananchi wote kila mmoja kwa nafasi yake aombe dua ili tupate mvua isiyo na maafa tushirikiane katika kumuomba Mwenyezi Mungu hii itakaribisha baraka na itatuondoshea huu wasiwasi viongozi wote wa dini, mashekhe wote tushirikiane,” amesema Mufti Zubeir.

Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Denis Bwigira amesema Mungu amejalia vitu vingi vya asili binadamu aweze kuvitumia kwa akili lakini wakati huu kwa pamoja viongozi wa dini wapo katika kuomba kwa sala makanisa yote.

“Naamini kutakua na maombi ya kitaifa. Tanzania tuna utajiri mkubwa wa maji ardhini na kwenye maziwa tumuombe Mungu atuzidishie uwezo wa kiteknolojia tuvute maji yaliyopo ardhiri tunaamini Mwenyezi Mungu hawezi kutuacha tuangamie kwa kiu,” amesema na kuongeza;

“Tunaamini tutapata maji ya kutosha na hii itukumbushe tunapo mtumainia Mwenyezi Mungu kuna njia za kujiwekea imani ya kuwa makini kwa majanga mbalimbali.”

Sala hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za tiba pamoja na viongozi wa kidini ambao kwa pamoja wameitaka taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa upendo, na kufuata maadili ya utumishi wa umma.

MWANANCHI
Asiwe mwongo muda wa mvua bado.
 
Burundi tu nmekaa sijawahai ona shida ya maji na maji wanayatoa lake tanganyika

Ova
 
Muft wa mchongo..kwahiyo saudia ni wametenda maasi sana hadi hakunyeshi mvua huko..elimisheni mwanachi wapande miti kwa wingi haya ni madhara ya uharibifu wa mazingira.

Na mvua zitakuja tu mana msimu ndio umekaribia..acheni kudanganya watu kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amewaasa Watanzania kupunguza na kuacha kabisa kutenda dhambi na badala yake wamrudie Mwenyezi Mungu ili kuwaepusha na adha ya ukame ulioikumba nchi. Amesema kukosekana kwa mvua, uwepo wa ukame na kukauka kwa maji ardhini ni ishara kwamba watu wanatenda maasi.

Hata hivyo mabadiliko ya tabianchi yanatajwa kuwa ni sababu ya ongezeko la joto, mvua zisizotabirika pamoja na ukame. Mufti ameyasema hayo leo Jumamosi Novemba 5, 2022 alipokuwa akiongoza dua maalum ya maadhimisho ya miaka 26 tangu kuanzishwa kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Muhimbili (MOI).

“Tunapoomba mvua tuendelee kuacha maasi na mambo mengine yasiyofaa, watu waache dhuluma, mambo mabaya yanayosababisha sisi Mwenyezi Mungu atunyime mvua,” amesema Mufti Zuberi. Amesema tayari viongozi wa dini wameanza kuomba dua kwa ajili ya kuiombea mvua.

“Mwenyezi Mungu atuletee mvua yenye kheri isiyo na maafa kwetu Tanzania na nchi zingine zilizopakana na sisi. Tunajipanga kuomba dua kwa Watanzania kwa ujumla na wenzetu wengine watafanya dua siku ya Jumatatu.

“Wananchi wote kila mmoja kwa nafasi yake aombe dua ili tupate mvua isiyo na maafa tushirikiane katika kumuomba Mwenyezi Mungu hii itakaribisha baraka na itatuondoshea huu wasiwasi viongozi wote wa dini, mashekhe wote tushirikiane,” amesema Mufti Zubeir.

Paroko wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Joseph, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Padri Denis Bwigira amesema Mungu amejalia vitu vingi vya asili binadamu aweze kuvitumia kwa akili lakini wakati huu kwa pamoja viongozi wa dini wapo katika kuomba kwa sala makanisa yote.

“Naamini kutakua na maombi ya kitaifa. Tanzania tuna utajiri mkubwa wa maji ardhini na kwenye maziwa tumuombe Mungu atuzidishie uwezo wa kiteknolojia tuvute maji yaliyopo ardhiri tunaamini Mwenyezi Mungu hawezi kutuacha tuangamie kwa kiu,” amesema na kuongeza;

“Tunaamini tutapata maji ya kutosha na hii itukumbushe tunapo mtumainia Mwenyezi Mungu kuna njia za kujiwekea imani ya kuwa makini kwa majanga mbalimbali.”

Sala hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa taasisi za tiba pamoja na viongozi wa kidini ambao kwa pamoja wameitaka taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma kwa upendo, na kufuata maadili ya utumishi wa umma.

MWANANCHI
Mwezi mtukufu ufike tena! Kama kwa mwezi mmoja unaweza kujidhibiti, kwa nini isiwe ndio jinsi unavyoishi maisha yako yote?
 
Mufti namheshimu sana ila angekemea pia uharibifu wa mazingira hasa ukataji miti hovyo. Utakuta hao wazinzi, wezi, wasengenyaji, wauaji na watenda dhambi wengine sio waharibifu wa mazingira kabisa lakini wanaoonekana wacha Mungu ndo hao wakawa wakata mito hovyo na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji kwenye vyanzo vya maji. Ifike sehemu viongozi wa dini wasiwe kama vile hawakwenda kabisa shule. Kukemea dhambi peke yake haitoshi kukabiliana na hili tatizo.
 
Back
Top Bottom