Mufti Mkuu asema "Punguzeni dhambi mvua zinyeshe"

Mwenyezi Mungu atunusuru na balaa hili la viongozi wa awamu ya tano kipindi Cha mpito.
 
Akili ndugu yangu, akili!
 
Your browser is not able to display this video.
 
Mashekhe waache kula kiboga kwanza, na pia waache kumfananisha Mwanasiasa na Mungu.
 
Mufti watu wameanza kutenda dhambi mwaka huu?
 
Hali ya hewa ya Dunia inaendana na Kanuni.
Usipo fata Kanuni unavuruga mzunguko wote.
Mfano tuu..Uwaribifu wa vyanzo vya maji.
 
Mimi kama Muislam ambaye Dini yangu inanifundisha kwamba dhambi huondoa baraka na kusababisha majanga na matatizo nimemuelewa Sheikh Zuberi (Allah amuongoze yeye na sisi). Ila ndio hivyo watu wanaleta ujuaji mwingi, wanajifanya wasomi sana nk.
 

41. Ufisadi umedhihiri bara na baharini kwa iliyo yafanya mikono ya watu, ili Mwenyezi Mungu awaonyeshe baadhi ya waliyo yatenda. Huenda wakarejea kwa kutubu

(Qur'an 30:41)
 
Mvua za kuomba mara nyingi huleta mafuriko...
 
Asiwe mwongo muda wa mvua bado.
 
Burundi tu nmekaa sijawahai ona shida ya maji na maji wanayatoa lake tanganyika

Ova
 
Muft wa mchongo..kwahiyo saudia ni wametenda maasi sana hadi hakunyeshi mvua huko..elimisheni mwanachi wapande miti kwa wingi haya ni madhara ya uharibifu wa mazingira.

Na mvua zitakuja tu mana msimu ndio umekaribia..acheni kudanganya watu kwenye ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Mwezi mtukufu ufike tena! Kama kwa mwezi mmoja unaweza kujidhibiti, kwa nini isiwe ndio jinsi unavyoishi maisha yako yote?
 
Mufti namheshimu sana ila angekemea pia uharibifu wa mazingira hasa ukataji miti hovyo. Utakuta hao wazinzi, wezi, wasengenyaji, wauaji na watenda dhambi wengine sio waharibifu wa mazingira kabisa lakini wanaoonekana wacha Mungu ndo hao wakawa wakata mito hovyo na kufanya shughuli za kilimo na ufugaji kwenye vyanzo vya maji. Ifike sehemu viongozi wa dini wasiwe kama vile hawakwenda kabisa shule. Kukemea dhambi peke yake haitoshi kukabiliana na hili tatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…