Mufti na Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir: Mwezi haujaonekana, mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza Jumapili March 02,2025

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir amesema mwezi haujaonekana leo Ijumaa February 28,2025 na hivyo amewatangazia Waislamu wote kwamba mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza keshokutwa Jumapili March 02,2025.

Akitangaza taarifa hiyo Jijini Tanga leo, Mufti Zubeir amesema “Ndugu Waislamu leo February 28,2025 tumekusanyika sehemu zetu za Kamati ya Mwezi kwa ajili ya kuangalia mwezi wa mwandamo kwa ajili ya Mwezi wa Ramadhan lakini haijapatikana habari yoyote ya mwezi Ramadhan, Tanzania Bara na Tanzania Visiwani, hata wenzetu wa Kenya vilevile hawajaona mwezi mahali popote”

“Kwa maana hiyo mwezi haukuonekana,
nawaelekeza Waislamu wote na kuwatangazia kwamba tunakamilisha Shaaban siku 30 na tunatarajia InshaAllah mwezi Ramadhan kuanza keshokutwa March 02,2025”
 
Ni Tanzania tuu mwezi huonekani

Uganda tayari

Kenya tayari

UK tayari

Anyway

Mfunga mwema.
Ni kila mwaka! Yani Bakwata huwa inakinzana na dunia nzima, ina mwezi wao wenyewe.

Mungu Mkubwa juzi juzi tu hapo Sheikh mmoja maneno yalimponyoka akasema huwa wanapokea maagizo watangaze au wasitangaze.

Mi kesho naamka na swaum, sifuati ujinga wa Bakwata.
 
🙏🙏🙏🙏✅✅✅✅

Bakwata Kama ccm tuuu,
 
Nimehadithiwa mpaka mwezi uonekane arabuni ndio ramadhan itaanza.

nimeanza zoezi lakini, nakula jioni tyu
 
Ni kila mwaka! Yani Bakwata huwa inakinzana na dunia nzima, ina mwezi wao wenyewe.

Mungu Mkubwa juzi juzi tu hapo Sheikh mmoja maneno yalimponyoka akasema huwa wanapokea maagizo watangaze au wasitangaze.

Mi kesho naamka na swaum, sifuati ujinga wa Bakwata.
Ni vizuri kuwa na msimamo lakini ni vizuri kuwa na elimu ya kile unachokisimamia.

Una ufahamu wowote juu ya fiqh ya funga?
 
Ni Tanzania tuu mwezi huonekani

Uganda tayari

Kenya tayari

UK tayari

Anyway

Mfunga mwema.
Afrika mashariki wote wamekubaliana kuwa mwezi ukionekana popote katika hizi nchi 3 basi wafunge na kufungua pamoja.

Hiyo taarifa haipo ndugu yangu kuwa Kenya au Uganda mwezi umeandama.

UK kwa nini tuufuate mwezi wao?
Ikiwa hii ni hoja yafaa kufahamu kuwa ibada za kiislamu ni za kimaumbile. Zinafuata maumbile ya mwezi na jua kwa maana ya nyakati.

Vipi napo kwenye nyakati za swala inatubidi tufuate mwenendo wa Jua la UK? Kwamba kule ikiwa adhuhur tutangaziwe sisi tuswali adhuhur pia?
 
Ni Tanzania tuu mwezi huonekani

Uganda tayari

Kenya tayari

UK tayari

Anyway

Mfunga mwema.
Afrika mashariki wote wamekubaliana kuwa mwezi ukionekana popote katika hizi nchi 3 basi wafunge na kufungua pamoja.

Hiyo taarifa haipo ndugu yangu kuwa Kenya au Uganda mwezi umeandama.

UK kwa nini tuufuate mwezi wao?
Ikiwa hii ni hoja yafaa kufahamu kuwa ibada za kiislamu ni za kimaumbile. Zinafuata maumbile ya mwezi na jua kwa maana ya nyakati.

Vipi napo kwenye nyakati za swala inatubidi tufuate mwenendo wa Jua la UK? Kwamba kule ikiwa adhuhur tutangaziwe sisi tuswali adhuhur pia
Najua kesho kufunga tusipangiane
Unajua haki si kumwangalia mtu!

Haki ni kile anachokisema ni sahihi?

Inawezekana mtu akazungumza ukweli lakini haiondoi kuwa ana sifa ya uongo.

Bakwata ni wazunguaji kwenye mambo mengi tu!

Lakini kwenye suala la mwezi wanavyolisimamia ndivyo kwenye vitabu vya fiqh limeandikwa hivyo hivyo kama wanavyolisimamia.

Hivyo rai yangu, tusome dini na tuache mkumbo.

Kwa sababu kwenye mahakama ya Allah atusimamishwa wewe kama wewe na kuhukumiwa wewe kama wewe.
 
IMG-20250228-WA0003.jpg

IMG-20250228-WA0004.jpg

Australia na Hong Kong wao Ramadhan itaanza Jumapili inshaallah!
 
Afrika mashariki wote wamekubaliana kuwa mwezi ukionekana popote katika hizi nchi 3 basi wafunge na kufungua pamoja.

Hiyo taarifa haipo ndugu yangu kuwa Kenya au Uganda mwezi umeandama.

UK kwa nini tuufuate mwezi wao?
Ikiwa hii ni hoja yafaa kufahamu kuwa ibada za kiislamu ni za kimaumbile. Zinafuata maumbile ya mwezi na jua kwa maana ya nyakati.

Vipi napo kwenye nyakati za swala inatubidi tufuate mwenendo wa Jua la UK? Kwamba kule ikiwa adhuhur tutangaziwe sisi tuswali adhuhur pia

Unajua haki si kumwangalia mtu!

Haki ni kile anachokisema ni sahihi?

Inawezekana mtu akazungumza ukweli lakini haiondoi kuwa ana sifa ya uongo.

Bakwata ni wazunguaji kwenye mambo mengi tu!

Lakini kwenye suala la mwezi wanavyolisimamia ndivyo kwenye vitabu vya fiqh limeandikwa hivyo hivyo kama wanavyolisimamia.

Hivyo rai yangu, tusome dini na tuache mkumbo.

Kwa sababu kwenye mahakama ya Allah atusimamishwa wewe kama wewe na kuhukumiwa wewe kama wewe.
Mkuu tusipangiane unajua nilipo mpaka useme hivyo nilipo nimeona mwezi
 
Uko wapi na kwanini umepinga tangazo la mwezi kutoonekana Afrika Mashariki?

Kama uko Papua New Guinea kuna haja gani ya kudai "tusipangiane" kwani Mufti kapangia dunia nzima?
 
Subiri jioni majibu mtapata na mufti
 
Back
Top Bottom