Mufti na Sheikh Mkuu Abubakar Zubeir: Mwezi haujaonekana, mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan utaanza Jumapili March 02,2025

Ni kila mwaka! Yani Bakwata huwa inakinzana na dunia nzima, ina mwezi wao wenyewe.

Mungu Mkubwa juzi juzi tu hapo Sheikh mmoja maneno yalimponyoka akasema huwa wanapokea maagizo watangaze au wasitangaze.

Mi kesho naamka na swaum, sifuati ujinga wa Bakwata.
Alishaomba anunulie Darubini, je amepata? isijekuwa sarakasi za makusudi ili aseme si niliwaambia?
 
Afrika mashariki wote wamekubaliana kuwa mwezi ukionekana popote katika hizi nchi 3 basi wafunge na kufungua pamoja.

Hiyo taarifa haipo ndugu yangu kuwa Kenya au Uganda mwezi umeandama.

UK kwa nini tuufuate mwezi wao?
Ikiwa hii ni hoja yafaa kufahamu kuwa ibada za kiislamu ni za kimaumbile. Zinafuata maumbile ya mwezi na jua kwa maana ya nyakati.

Vipi napo kwenye nyakati za swala inatubidi tufuate mwenendo wa Jua la UK? Kwamba kule ikiwa adhuhur tutangaziwe sisi tuswali adhuhur pia

Unajua haki si kumwangalia mtu!

Haki ni kile anachokisema ni sahihi?

Inawezekana mtu akazungumza ukweli lakini haiondoi kuwa ana sifa ya uongo.

Bakwata ni wazunguaji kwenye mambo mengi tu!

Lakini kwenye suala la mwezi wanavyolisimamia ndivyo kwenye vitabu vya fiqh limeandikwa hivyo hivyo kama wanavyolisimamia.

Hivyo rai yangu, tusome dini na tuache mkumbo.

Kwa sababu kwenye mahakama ya Allah atusimamishwa wewe kama wewe na kuhukumiwa wewe kama wewe.
Ndugu zangu Aya mambo yanahutaji uchamungu na mazingira lkn kama elimu watu wanayo Sina hakika kama wote wanaopindisha ni kwasabb ni wapumbav isipokuwa wengi wao wanafanya kwasabb ya matumbo Yao na kuwafurahisha watawala
 
Hili suala limeshajadiliwa na wana wazuoni waliyopita na wa sasa na fatwa zilishatolewa.

Na kwa nini wana wazuoni? Kwa sababu adila za sheria zipo 4.

Qur'an na sunna ndiyo asili. Ijmaa na Qiyas ni ncha zake.

Mkutano wa wana wazuoni uliyofanyika Saudia Majmaal Fiqh Al Islam ulishatoa mwongozo kwa zama zetu kuwa kila nchi ifuate mwandamo wa kwake.

Na fatwa zipo nyingi sana! Ukibahatika kwenda hija pitia kwenye vibanda vya fatawa watakupatia hukumu hizo hizo kwani kuuliza ni ruhusa.

Tena kongamano la wana wazuoni likahitimisha kuwa; maamuzi ya mwandamo wa mwezi yanapaswa kufanywa na mahakama za kiislamu au Taasisi rasmi za kiislamu ndani ya kila nchi.

Kuna wengine wanajiamulia kufunga wao wenyewe kwa kufuata mwezi mwandamo wa kimataifa, hili suala halipo! Kwa sababu ikifuatwa kauli yenye nguvu ndiyo hiyo ya mwezi wa eneo lako.
 
Afrika mashariki wote wamekubaliana kuwa mwezi ukionekana popote katika hizi nchi 3 basi wafunge na kufungua pamoja.

Hiyo taarifa haipo ndugu yangu kuwa Kenya au Uganda mwezi umeandama.

UK kwa nini tuufuate mwezi wao?
Ikiwa hii ni hoja yafaa kufahamu kuwa ibada za kiislamu ni za kimaumbile. Zinafuata maumbile ya mwezi na jua kwa maana ya nyakati.

Vipi napo kwenye nyakati za swala inatubidi tufuate mwenendo wa Jua la UK? Kwamba kule ikiwa adhuhur tutangaziwe sisi tuswali adhuhur pia

Unajua haki si kumwangalia mtu!

Haki ni kile anachokisema ni sahihi?

Inawezekana mtu akazungumza ukweli lakini haiondoi kuwa ana sifa ya uongo.

Bakwata ni wazunguaji kwenye mambo mengi tu!

Lakini kwenye suala la mwezi wanavyolisimamia ndivyo kwenye vitabu vya fiqh limeandikwa hivyo hivyo kama wanavyolisimamia.

Hivyo rai yangu, tusome dini na tuache mkumbo.

Kwa sababu kwenye mahakama ya Allah atusimamishwa wewe kama wewe na kuhukumiwa wewe kama wewe.
Sawa ndugu wa Bakwata ccm
 
Back
Top Bottom