Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
hoja yangu ni ndogo sana. je? tunatakiwa kuwaenzi familia hizo tu zilizohusika, au waislam wote hata wale waliokuwa wanacheza tu bao? yeye au baba yake au babu yake walitoa mchango gani? (kama walitoa, tutamuenzi yeye na sio waislam wote), kwanini waislam wooote nchini waenziwe kwa jasho lililotolewa na familia kadhaa tu? na kwani, ni waislam pekee ndio walitoa jasho? hakuna mkrisot hata mmoja, na je, kwenye familia hizo za wakristo tuenzi familia hizo tu au tuenzi wakristo wote?Yesu Anakuja hujui kuwa Mohamed Said amepewa tuzo na JF, hujui kuwa ameandika vitabu kadhaa vinavyotumika na vyuo vikuu duniani? hujui kuwa umma wa kiislamu umefanyiwa madhila? tegemea mzee kuyasema haya katika utetezi wake kwa hoja ulizotoa🙂
Yesu,Nadhani ingekuwa fair kama familia zile tu zilizohusika na mchango wa uhuru zithaminiwe, kwasababu sio waislam wote walipigania uhuru na sio wakristo wote walipigania uhuru. kwahiyo tuseme wakati waislam wanapigania uhuru wakristo walikuwa hawapiganii uhuru? na hata kama ni hivyo, kwanini tusienzi familia hadi wajukuu wa hizo familia kuliko kuwaingiza watu ambao pengine hawakupigania uhuru kabisa?
mfano, mzee wangu mdini kuliko wote Mohamed said, siku zote umetamani kula matunda ya waislam waliopigania uhuru, wewe babu yako alipigania uhuru? baba yako au wewe mwenyewe ulitoa mchango gani? kwanini mnapendaga vya bure sana? pia, kwa shehe zuberi, kama anasema kulikuwa na mchango wa waislam, ni waislam wepi? ndugu zake, baba zake, wajomba zake? kama ana connection nao kifamilia, anastahili yeye na familia yake wakumbukwe. hiyo ni haki. si ukute wakati waislam kadhaa wa DSM wanashirikiana na nyerere kupigania uhuru, baba yake huyu shehe alikuwa huko anafanya yake, hakuna mchango wowote alitoa, lakini kwasababu kuna muislam alishawahi kufanya jambo basi wanataka wachume kupitia muislam huyo.
kwanini shehe leo hii asisimame kwenye jukwaa na kusema, tuenzi utajiri wa waislam kama kina bahresa na mo na wengine, kwasababu huo ni utajiri wa "waislam". hivi jitihada zangu mimi ni jitihada za wakristo wote? jitihada zako wewe ni jitihada za waislam wote hata wale wasiojishughulisha? kwanini huwa mnapenda vya bure na kulalamikalalamika, mnataka mpewe nchi yote muishi peke yenu? huwa hamuoni aibu? mzee Saidi hadi leo umezeeka unataka kufa bado mdomo wako umejaa udini na manung'uniko kwenye vitu ambavyo walifanya wenzio wewe haukutoa mchango wowote. ninyi ndio wale wanaoridhikaga kwa jitihada na utajiri wa jirani, fanyeni kazi, mtanung'unika hadi milele lakini hakuna mtu atakuja kusema chukueni pesa hizi hapa ni mchango wa familia binafsi za kiislam zilizochangia uhuru.
mimi mtu akija na wazo kwamba, waislam kiujumla waenziwe kwa mchango huo, kwasababu tu na yeye ni muislam na anataka kujivika kwenye joho la wale wazee wetu waliopambana, huwa namwona simwelewi.
Salari,Yesu Anakuja hujui kuwa Mohamed Said amepewa tuzo na JF, hujui kuwa ameandika vitabu kadhaa vinavyotumika na vyuo vikuu duniani? hujui kuwa umma wa kiislamu umefanyiwa madhila? tegemea mzee kuyasema haya katika utetezi wake kwa hoja ulizotoa🙂
Bila shaka utayasema tu kama sio katika uzi huu basi uzi mwingine🤣😂Salari,
Sikuyasema hayo.
Nimemweleza mchango wa babu yangu katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Salari,Bila shaka utayasema tu kama sio katika uzi huu basi uzi mwingine🤣😂
babu yangu Mzee Mohamed Said, mimi sio mgeni, tumeshabishana mengi sana hapa mimi na wewe directly, ninachopenda kukuambia ni kwamba, kama babu yako alipigania uhuru, babu yako anastahili kuenziwa. na tunashukuru Mungu kwa ajili yake. lakini hatuwezi kusema wewe hapo binafsi unatudai chochote, kwasababu sio babu yako tu aliyepigania. watoto wa nyerere hadi leo masikini, wewe hapo ulipo ni tajiri kuliko watoto wa nyerere. na watoto wa kawawa, na watoto wa wengine wengi tu. tunawashukuru wazee wenu kwa kupigania uhuru, lakini ninyi wajukuu hamtudai kitu.Yesu,
Inaelekea wewe ni mgeni katika jukwaa hili.
Itakuwa tabu kujibu yote uliyosema.
Nitakueleza historia ya babu yangu Salum Abdallah:
BABU YANGU SALUM ABDALLAH POPO
Ikiwa umemsoma babu yangu Salum Abdalah na kigoma chake cha daku utakuwa umeona kuwa alipata kuwekwa kizuizini mwaka wa 1964.
Hayo hapo chini yatakusaidiwa kumwelewa mtu huyu.
Ilikuwa mwaka wa 1965 babu yangu Salum Abdallah katoka jela ya Uyui Tabora alikowekwa kizuzini mwaka wa 1964 baada ya maasi ya Tanganyika Rifles tarehe 20 Januari 1964 hana kazi yuko nyumbani.
Mwaka wa 1953 akiwa na taarifa kutoka Dar es Salaam kuwa kuna harakati za kuunda chama cha siasa yeye na wenzake Tabora wakawa wanafanya mikutano ya siri kila Jumapili Town School ambako Abubakar Mwilima alikuwa mwalimu na yeye Mwalimu Abuu kama walivyopenda kumwita ndiye aliyekuwa akiwafungulia darasa moja kukutana na kupeana habari kutoka New Street Dar es Salaam, Makao Makuu ya TAA.
Hii ailikuwa baada ya kumtuma Katibu wa TAA Western Province, Germano Pacha kwenda Makao Makuu ya TAA kuwapa taarifa kuwa Tabora inataka kuunda chama cha siasa.
Germano Pacha alipokelewa Dar es Salaam na Abdul Sykes na akamwambia arudishe salamu Tabora kuwa wafanye subira.
Tufupishe kisa kwani kuna mengi.
TANU ikaundwa mwaka wa 1954 babu yangu akiwa mmoja wa wanachama wa mwanzo.
Mwaka wa 1955 babu na Kassanga tumbo wakaunda Tanganyika Railway African Union (TRAU) babu akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary.
Babu yangu Salum Abdallah ana historia ya uzalendo ya kusisimua ambayo hutochoka kuisikiliza kila inapohadithiwa kwa kuwa mkasa una kuwa ndani ya mkasa mwingine visa vikiunganishwa kama ushanga katika uzi.
Mwaka wa 1965 baba akanifungia safari niende Tabora kumwangalia babu baada ya kutoka kifungoni.
Babu yangu jina lake alililopewa na baba yake Abdallah Mwekapopo (naweza kwenda vizazi saba hadi kwa waliokuwa Belgian Congo) ni Rashid lakini katika ujana wake akiwa mfanyakazi wa Tanganyika Railways katika miaka ya 1930 alimpiga Mzungu akafungwa na alipotoka jela akabadili jina lake akawa Salum Abdallah.
Kisa gani akampiga Mzungu?
Huyu Mzungu alikuwa mbaguzi, mnyanyasaji Waafrika kwa hiyo babu siku moja akaamua kumshughulikia.
Hili lilikuwa kosa kubwa sana wakati wa ukoloni.
Hukaa nikafikiri yule Mzungu alikuwa katika hali gani baada ya kuingia katika mikono ya babu kwani alikuwa kapanda juu futi sita ana kifua kipana ile mitambo, yaami maumbo makubwa ya Kimanyema.
Kwa ajili ya umbo hili akiwa kijana Waingereza walimfunza kazi ya kufua chuma, yaani ‘’foundry,’’ kazi ngumu katika moto na joto kali.
Hii ‘’foundry ’’ ilikuwa ndani ya karakana ya Tanganyika Railways.
Humo ndani ya karakana wanaume wako vifua wazi na nyundo nzito ni kelele za chuma kikigonga chuma cheche za moto zikiruka na miaka ile hakuna vifaa mfanyakazi atavaa kuzuia kelele.
Hii karakana ndiyo ilikuwa ikachonga spea za treni.
Wenyewe kwa wenyewe ndani ya karakana wakizungumza kwa sauti za juu.
Labda ndiyo sababu babu hata akizunngumza hata katika mazungumzo ya kawaida sauti yake siku zote ilikuwa juu.
Hii karakana ilikuwa ndani ya eneo la Tanganyika Railway lakini jirani na Arab Street hivi sasa Mtaa wa Nkrumah na ndiko lilipokuwa lango kuu la wafanyazi wa Tanganyika Railways wakiingilia na kutokea katika miaka ile ya 1930.
Babu akiishi Mtaa wa Kipata.
Nyuma aliyokuwa akiishi ilikuwa inatazamana na nyuma ya Kleist Sykes ambae yeye alikuwa Accounts Clerk (Karani wa Mahesabu) Tanganyika Railways.
Nafasi kubwa sana wakati ule kwani hio kazi wakifanya Wahindi.
Lakini babu yangu juu ya ubabe wake na haya yote alikuwa mtu karimu sana mimi nimeshuhudia kwa macho yangu na labda huu ukarimu alimrithisha baba yangu kwani mara nyingi nikipisha wageni chumbani kwangu nami kwenda kulala ‘’sitting room,’’hadi waondoke.
Hii Karakana ya Railway ikahamishwa Dar es Salaam mwaka wa 1947 kupelekwa Tabora na babu yangu akahamanayo kwenda huko.
Hakurudi tena Dar es Salaam.
Lakini mwaka huo huo alipofika Tabora akaongoza mgomo wa Railway ulioenea nchi nzima na akafanya hivyo mwaka wa 1947, 1949 na tena mwaka wa 1960 miezi michache kabla ya Tanganyika kupata madaraka.
Huu mgomo wa mwaka wa 1960 ulidumu kwa siku 82 na kuweka rekodi kushida mgomo wa Kenya ulioongozwa na Makhan Singh uliodumu kwa siku 62.
Baada ya mgomo huu wa mwaka wa 1960 Nyerere ilimhidhihirikia kuwa mtu huyu atakuja kumpa shida katika Tanganyika huru akawa sasa anamtazama kwa macho mawili.
Picha: Kulia ni Salum Abdallah na anaefuatia ni Kassanga Tumbo na viongozi wa TRAU, Tabora.
View attachment 3043143
Yesu...babu yangu Mzee Mohamed Said, mimi sio mgeni, tumeshabishana mengi sana hapa mimi na wewe directly, ninachopenda kukuambia ni kwamba, kama babu yako alipigania uhuru, babu yako anastahili kuenziwa. na tunashukuru Mungu kwa ajili yake. lakini hatuwezi kusema wewe hapo binafsi unatudai chochote, kwasababu sio babu yako tu aliyepigania. watoto wa nyerere hadi leo masikini, wewe hapo ulipo ni tajiri kuliko watoto wa nyerere. na watoto wa kawawa, na watoto wa wengine wengi tu. tunawashukuru wazee wenu kwa kupigania uhuru, lakini ninyi wajukuu hamtudai kitu.
kwani tangu uanze kulalamika, umeshapata shilingi ngapi? na, shida ni kwamba unalalamika sio kwasababu familia yako walipambania uhuru, bali kwasababu ya udini, unataka waislam kama wapate mgao fulani kwasababu fulani. Hii nchi hadi hapa tulipofika watu wa dini zote hadi wahindu wana mchango wao kwa namna moja ama nyingine, msijione kama ninyi ni special sana. jitahidi basi, kwa umri wako uwe unaandika mambo yanayoendana na umri, unategemewa hapa ndani kulingana na umri wako tupate madini, tumelelewa tukiamini wazee kama wewe ni hazina, wana uzoefu wa maisha na wataleta hoja za kujenga sio tu vijana ila Taifa ili tuendelee kuwa na umoja. tofauti yake wewe naona wazee wenzio walivyokuwa wanachota busara na kuishi nazo, wewe utakuwa ulikuwa unacheza bao. ukapitwa. ndio maana upo hapa unabishana na vitoto vidogo kuhusu mambo ya dini, kila siku dini tuuu unaleta udini, huna maana wala faida kwa taifa hili.
Mkuu msamehe tu huyu mzee,kapata elimu dunia vizuri tu kumbe alikua anazurula tu duniani kwa ufadhili wa wanaotuita makafir alipoishia akili yake ndo hapo.tumelelewa tukiamini wazee kama wewe ni hazina, wana uzoefu wa maisha na wataleta hoja za kujenga sio tu vijana ila Taifa ili tuendelee kuwa na umoja. tofauti yake wewe naona wazee wenzio walivyokuwa wanachota busara na kuishi nazo, wewe utakuwa ulikuwa unacheza bao. ukapitwa. ndio maana upo hapa unabishana na vitoto vidogo kuhusu mambo ya dini, kila siku dini tuuu unaleta udini, huna maana wala faida kwa taifa hili.
Babu...Mkuu msamehe tu huyu mzee,kapata elimu dunia vizuri tu kumbe alikua anazurula tu duniani kwa ufadhili wa wanaotuita makafir alipoishia akili yake ndo hapo.
Fikiria huyu mzee angekulia na kulala madrasa kule msikitini angekua wapi,huyu ni extremister na ana chuki ya wazi kwa wakristo.
Mtu anapindisha mpaka historia ya nchi hii ili Baba wa taifa mmisionari aonekane alidandia treni kwa mbele kwenye kusaka uhuru wa nchi hii.
Bali waislamu ndio walipigania uhuru.
Ni sawa wote walishirikiana km Watanganyika kudai uhuru.
Lakini sijui kwanini anakazania waislam wapewe kipaumbele.
Kupeleka mada ukakasi mpaka kwa mufti Ipo humu.
Sijui anataka nini
City...Nadhani harakati za kusaka uhuru zilikiwa katika misingi ya utaifa na uzalendo. Si udini.
Vyama vilivyopigania uhuru viliundwa na watu wa kila namna, watu wasiofuata dini za wageni, wakristo, waislamu n.k
Watu walipambania nchi ya watanganyika/wazanzibari iwe huru.
Kwanini waislamu wa leo mnaleta ajenda ya kupambania uhuru chini ya mwamvuli wa dini?
Waislamu waliopambani uhuru walijiunga na wenzao kwa upendo..ninyi mnajitenga kwa manung'uniko.. why?
PumbaNadhani ingekuwa fair kama familia zile tu zilizohusika na mchango wa uhuru zithaminiwe, kwasababu sio waislam wote walipigania uhuru na sio wakristo wote walipigania uhuru. kwahiyo tuseme wakati waislam wanapigania uhuru wakristo walikuwa hawapiganii uhuru? na hata kama ni hivyo, kwanini tusienzi familia hadi wajukuu wa hizo familia kuliko kuwaingiza watu ambao pengine hawakupigania uhuru kabisa?
mfano, mzee wangu mdini kuliko wote Mohamed said, siku zote umetamani kula matunda ya waislam waliopigania uhuru, wewe babu yako alipigania uhuru? baba yako au wewe mwenyewe ulitoa mchango gani? kwanini mnapendaga vya bure sana? pia, kwa shehe zuberi, kama anasema kulikuwa na mchango wa waislam, ni waislam wepi? ndugu zake, baba zake, wajomba zake? kama ana connection nao kifamilia, anastahili yeye na familia yake wakumbukwe. hiyo ni haki. si ukute wakati waislam kadhaa wa DSM wanashirikiana na nyerere kupigania uhuru, baba yake huyu shehe alikuwa huko anafanya yake, hakuna mchango wowote alitoa, lakini kwasababu kuna muislam alishawahi kufanya jambo basi wanataka wachume kupitia muislam huyo.
kwanini shehe leo hii asisimame kwenye jukwaa na kusema, tuenzi utajiri wa waislam kama kina bahresa na mo na wengine, kwasababu huo ni utajiri wa "waislam". hivi jitihada zangu mimi ni jitihada za wakristo wote? jitihada zako wewe ni jitihada za waislam wote hata wale wasiojishughulisha? kwanini huwa mnapenda vya bure na kulalamikalalamika, mnataka mpewe nchi yote muishi peke yenu? huwa hamuoni aibu? mzee Saidi hadi leo umezeeka unataka kufa bado mdomo wako umejaa udini na manung'uniko kwenye vitu ambavyo walifanya wenzio wewe haukutoa mchango wowote. ninyi ndio wale wanaoridhikaga kwa jitihada na utajiri wa jirani, fanyeni kazi, mtanung'unika hadi milele lakini hakuna mtu atakuja kusema chukueni pesa hizi hapa ni mchango wa familia binafsi za kiislam zilizochangia uhuru.
mimi mtu akija na wazo kwamba, waislam kiujumla waenziwe kwa mchango huo, kwasababu tu na yeye ni muislam na anataka kujivika kwenye joho la wale wazee wetu waliopambana, huwa namwona simwelewi.
Mzee Said, ninakubali waislamu na wakristu na wengine wasio wa dini hizo mbili walifanya juhudi nyingi kutuletea uhuru.City...
Waasisi wa African Association 1929: Cecil Matola (President), Kleist Abdallah Sykes (Secretary), Mzee bin Sudi, Ibrahim Hamisi, Ali Said Mpima, Suleiman Majisu, Zibe Kidasi, Rawson Watts na Raikes Kusi.
Baada ya kuunda AA Kleist Sykes, Ali Jumbe Kiro na Mzee bin Sudi 1933 wakaunda Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika).
Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika iliunganishwa katika AA kupambana na ukoloni na madhila yake yote.
Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika ndiye alikuwa pia Mweka Hazina wa TANU 1954 na ndiye alikuwa mkusanyaji wa fedha za safari ya Julius Nyerere UNO mwaka wa 1955.
Nyerere dhifa ya kumuaga safari ya UNO ilifanyika katika jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.
Harakati za kudai uhuru zilipopamba moto Mufti Sheikh Hassan bin Ameir alikuwa akiuza kadi za TANU msikitini.
Abdul Sykes akisambaza kadi za TANU ndani ya Soko la Kariakoo yeye akiwa Market Master.
Jiulize kwa nini historia hii ilifutwa?
Angalia hizo picha hapo chini unaona nini?
View attachment 3043991
Baraza la Wazee waTANU
View attachment 3043992
Jengo la Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika lilijengwa 1936
View attachment 3043994
Kulia Haruna Taratibu, Saadan Abdu Kandoro, Julius Nyerere, Sheikh Mohamed Ramia na Iddi Faiz Mafungo
Huyu Ustadhi anafikiri ana akili kumbe bure kabisa.Mkuu msamehe tu huyu mzee,kapata elimu dunia vizuri tu kumbe alikua anazurula tu duniani kwa ufadhili wa wanaotuita makafir alipoishia akili yake ndo hapo.
Fikiria huyu mzee angekulia na kulala madrasa kule msikitini angekua wapi,huyu ni extremister na ana chuki ya wazi kwa wakristo.
Mtu anapindisha mpaka historia ya nchi hii ili Baba wa taifa mmisionari aonekane alidandia treni kwa mbele kwenye kusaka uhuru wa nchi hii.
Bali waislamu ndio walipigania uhuru.
Ni sawa wote walishirikiana km Watanganyika kudai uhuru.
Lakini sijui kwanini anakazania waislam wapewe kipaumbele.
Kupeleka mada ukakasi mpaka kwa mufti Ipo humu.
Sijui anataka nini
DINI NA KABILA TANGANYIKAUdini tu.
Asante kwa bandiko hiliMUFTI SHEIKH ABUBAKAR ZUBEIR ATIA NENO HISTORIA YA WAISLAM NA UHURU WA TANGANYIKA
Kongamano la kuadhimisha mwaka wa Kiislam 1446 lilihitimishwa na Mufti Sheikh Abubakar Zubeir kwa kutia neno kuhusu mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Mufti amesema ni muhimu Waislam waeleze mchango wao katika kupigania uhuru wa Tanganyika ili wasiojua wafahamu.
Sheikh Abubakar Zubeir amesema kuwa kama Waislam hawataieleza historia yao hakuna atakaeieleza kwa niaba yao.