Mufti Sheikh Abubakar Zubeir Atia Neno Historia ya Waislam Katika Uhuru wa Tanganyika

Mufti Sheikh Abubakar Zubeir Atia Neno Historia ya Waislam Katika Uhuru wa Tanganyika

Nadhani ingekuwa fair kama familia zile tu zilizohusika na mchango wa uhuru zithaminiwe, kwasababu sio waislam wote walipigania uhuru na sio wakristo wote walipigania uhuru. kwahiyo tuseme wakati waislam wanapigania uhuru wakristo walikuwa hawapiganii uhuru? na hata kama ni hivyo, kwanini tusienzi familia hadi wajukuu wa hizo familia kuliko kuwaingiza watu ambao pengine hawakupigania uhuru kabisa?

mfano, mzee wangu mdini kuliko wote Mohamed said, siku zote umetamani kula matunda ya waislam waliopigania uhuru, wewe babu yako alipigania uhuru? baba yako au wewe mwenyewe ulitoa mchango gani? kwanini mnapendaga vya bure sana? pia, kwa shehe zuberi, kama anasema kulikuwa na mchango wa waislam, ni waislam wepi? ndugu zake, baba zake, wajomba zake? kama ana connection nao kifamilia, anastahili yeye na familia yake wakumbukwe. hiyo ni haki. si ukute wakati waislam kadhaa wa DSM wanashirikiana na nyerere kupigania uhuru, baba yake huyu shehe alikuwa huko anafanya yake, hakuna mchango wowote alitoa, lakini kwasababu kuna muislam alishawahi kufanya jambo basi wanataka wachume kupitia muislam huyo.

kwanini shehe leo hii asisimame kwenye jukwaa na kusema, tuenzi utajiri wa waislam kama kina bahresa na mo na wengine, kwasababu huo ni utajiri wa "waislam". hivi jitihada zangu mimi ni jitihada za wakristo wote? jitihada zako wewe ni jitihada za waislam wote hata wale wasiojishughulisha? kwanini huwa mnapenda vya bure na kulalamikalalamika, mnataka mpewe nchi yote muishi peke yenu? huwa hamuoni aibu? mzee Saidi hadi leo umezeeka unataka kufa bado mdomo wako umejaa udini na manung'uniko kwenye vitu ambavyo walifanya wenzio wewe haukutoa mchango wowote. ninyi ndio wale wanaoridhikaga kwa jitihada na utajiri wa jirani, fanyeni kazi, mtanung'unika hadi milele lakini hakuna mtu atakuja kusema chukueni pesa hizi hapa ni mchango wa familia binafsi za kiislam zilizochangia uhuru.

mimi mtu akija na wazo kwamba, waislam kiujumla waenziwe kwa mchango huo, kwasababu tu na yeye ni muislam na anataka kujivika kwenye joho la wale wazee wetu waliopambana, huwa namwona simwelewi.
Yesu....
Umeniuliza kama babu yangu alipigania uhuru.

Jibu ni ndiyo.

Soma hapo chini historia ya babu yangu Salum Abdallah:

MACHACHE KUHUSU BABU YANGU SALUM ABDALLAH

Hiyo picha ya Loco Shed Tabora ndipo akifanyakazi babu yangu Salum Abdallah maarufu Baba Popo kuanzia 1947 had 1964.

Alihamia Tabora kutoka Dar es Salaam baada ya Loco Shed kuhamishwa kutoka Dar es Salaam mwaka huo wa 1947.

1955 yeye na Kassanga Tumbo walianzisha chama Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Salum Abdallah akiwa President na Kassanga Tumbo Secretary.

TRAU ina historia kubwa sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

TRAU ilifanya mgomo mwaka wa 1960 uliodumu siku 82.

Salum Abdallah aliongoza mgomo huo wa wafanyakazi wa Railways uliodumu miezi mitatu.

Kwa miezi mitatu treni, meli na mabasi ya Railway yalisimama hadi Waingereza waliposalimu amri na kuwaita viongozi wa wafanyakazi katika meza ya majadiliano.

Uhuru ulipopatikana babu yangu akapambana kwa fikra na msimamo wa Nyerere kuhusu vyama vya wafanyakazi Nyerere akitaka viwekwe chini ya TANU na viongozi wa vyama vya wafanyakazi pamoja na babu yangu wakipinga wazo hilo.

Yalipotokea maasi ya wanajeshi tarehe 20 Januari 1964 baada ya maasi kuzimwa na jeshi la Waingereza, Nyerere aliwakamata viongozi wote wa vyama vya wafanyakazi na kuwaweka kizuizini.

Babu yangu alifungwa kwenye jela ya Uyui, Tabora na alipotoka kizuizini Tanganyika Railway African Union (TRAU) chama alichokiasisi mwaka wa 1955 kilikuwa kimepigwa marufuku pamoja na vyama vingine vya wafanyakazi na badala yake kimeundwa chama cha National Union of Tanganyika Workers (NUTA) kwa juhudi kubwa za Rashid Kawawa na Michael Kamaliza.

Babu yangu alihama Tabora na kwenda Urambo kupisha shari kwani zilienezwa taarifa za uongo kuwa yeye alikuwa katika kundi pamoja na Victor Mkello (kiongozi wa wafanyakazi wa mashamba ya mkonge) na Kassanga Tumbo walikuwa wamekula njama ya kupindua serikali na kumuua Rais Nyerere.

Babu yangu akajikita katika ukulima wa tumbaku Urambo huku akiendelea na ukulima wake wa miaka yote Kakola na Uyui Tabora.

Fredrick Mchauru aliendelea na utumishi katika serikali ya kikoloni na uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961 alishika nyadhifa mbalimbali katika serikali huru kama zilizvyoelezwa katika makala zilizochapwa na Raia Mwema.

Kama mimi nisingeaandika kitabu cha Abdul Sykes huenda historia hii ya babu yangu na wazalendo wengine isingejulikana na historia ambazo zingesomwa ndiyo hizi za watu kama Fredrick Mchauru na wengineo.

Salum Abdallah alifariki mwaka wa 1974 akiwa na umri kama miaka 80 akiwa mkimya sana kwa kuwa hapakuwa tena pale mjini na barza zilizokuwa zikijadili siasa kama miaka ya 1950 wakati wa kudai uhuru.

Siasa ilikuwa sasa jambo la kutisha watu wakihofu kukamatwa na kuwekwa gerezani.

Babu yangu akiungulia ndani kwa ndani kwa chuki dhidi ya TANU chama alichokiendea mbio na kuhudhuria mikutano yake yote ya siri mwaka wa 1953 pamoja na wazee wenzake akina Maulidi na Abdallah Kivuruga, Rajab Saleh Tambwe, Abubakar Mwilima kuwataja wachache, na kuwa mmoja wa waasisi wake mjini Tabora mwaka wa 1955.

Siku zote yeye baada ya kuona vyama vya wafanyakazi vimekwa chini ya TANU na serikali yake aliwaona viongozi wapya wa vyama hivi vibaraka wa serikali hawataweza kupigania haki za wafanyakazi kwa dhati.

Picha: Kulia ni Christopher Kassanga Tumbo anaefuata ni Salum Abdallah.

1728450105893.jpeg
 
Back
Top Bottom