Mufti Simba aagiza Waislamu waikatae CCM

wewe mkristo inakuhusu nini?
Unajuaje walichokosa kwenye mahakama mama?
wapeni haki zao what is the issue here?


Ndg Tumain embu tupeni basi hayo wanayokosa ktka mahakama mama nasi tujue mana tupo gizani tuu!
 
Namuunga mkono mzee Simba kwa hoja yake ya kuwataka waislamu wasiipigie kura ccm kwa sababu ninatamani sana kuiona ccm ikifa kifo cha mende!

Nawaomba viongozi wa dini za kikristo nao waanzishe hoja kama hiyo kwa waumini wao ya kutoipigia kura ccm 2010! Hapo ukombozi wa watz utakuwa umepatikana kiurainiiiiiiii...!
 
Haya matatizo siyo ya waislamu wa kulaumiwa ni CCM.Ikumbukwe viongozi wakristo wa CCM ndiyo walioandaa ilani hiyo akiwemo Benjamin Mkapa,Philip Mangula na KIngunge Ngombale Mwiru.Na vilevile ni mkristo mwingine Bernard Membe akachokoza OIC.Kwa kuangalia mwenendo wa viongozi hawa ni vyema kabla ya kulaumu viongozi wa BAKWATA wahojiwe kwa nini waliingiza vitu controversial kinyume cha katiba waliyoapa kuilinda?
 
ndio mnajua leo kuwa CCM ni matapeli? mnalo
 


Nimesoma post zako mbili tu...upo very Intellectual ! Upo juu sana upstairs!
 
.
Kama noma naiwe noma potelea mbali na ivunjike amani.
.
MUFTI UKO SAWA
.
Katika hili umewaunganisha waislam. Hii ndio bakwata
Inayo hitajiwa na waislam.

Ndg embu pitia kidogo kuna post 2 kazitupa Bw.Mkandara
Hayo nayosema sio solution na yanaonyesha upeo duni kabisa
 
Mimi Namwamini sana Mkandara kwa comments zake, He is very really cool guy.
 
Mambo yanadizidi kuwa mambo safi sana Mufti kuwakweli kama simba

maana kadinali pengo akionge siri kali kimyaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!1
 
Serikali lazima iangalie hili suala ni mgogoro mkubwa sana unafukuta.
 



Duuh!!
natungoje tuyaone haya yakitokea,kwani siku si nyingi huko bukoba kuna uchaguzi...!!!
 
naamini ya kwamba mtu mzima akisema hana budi kusikilizwa, Jamaa wana hoja wapewe tu mahakama zao Ila nani atakuwa anawalipa mishahara dini husika au Serikali? Kama serikali basi inabidi hao makadhi basi wawe wa dini yeyote isije ikawa chombo cha kujitengenezea ajira kwa dini fulani.
 
Nafikiri njia ya mwongo ni fupi na pia za mwizi ni arobaini. Kwa muda mrefu sisiemu walikuwa wakiendesha siasa za ulaghai, sasa yamefika mwisho. Si waislamu pekee walioathirika na uongo huo, na wengine si mnawaona? wa kutoa laana haya!!!!!!!! wa kutishia kujitoa kwenye sisiemu haya!!!!!!!!!!! Nafikiri soon tutapata mbivu na mbichi.
Usanii umefika mwisho. Nakumbuka niliuliza kama kuna kipimo cha kupima uwezo wa kufikiri wa hawa jamaa wanaoitwa wasirikali, sikupata jibu. Naomba nikumbushie!
 
kama kipi?
 
Tusikubali kuyumbishwa na watu kama hawa na pia mimi nasema kuwa udini ni suala la mtu mmoja na sio kama hivi leo
 
Wanaopinga mahakama ya kadhi wanapinga kitu wasichokijua, hii ni dangerous, na kwa kweli wamekurupuka kupinga.

Mahakama hii ilikuwapo hapa (Tanganyika) wakati wa ukoloni na baada ya uhuru, lakini ilifutwa wakati wa awamu ya kwanza ya uongozi wa nchi hii bila sababu wala maelezo. Zanzibar bado ipo. Mahakama hizi zipo pia mahala pengi duniani tena ktk nchi nyingine ambazo siyo za kiislamu e.g. Kenya, Uganda, U.K. etc..hivi huko mahakama hizi zimeleta maafa gani au wakristo wa huko siyo wakristo kama wa Tanzania?

Tuache jazba na uchochezi wa kidini na tufanye utafiti kabla ya kupinga kitu tusichokijua halafu kikatuletea balaa katika taifa letu. Wapeni wanachotaka waislamu na wengine pia wapewe wakitaka ili tuishi salama, there is no big deal here.
 
There are two things in our job. Criticism i accept with respect. Disrespect i dont accept and dont respect" - Arsene Wenger.

Ndugu yangu Mkandara,
Kweli Maadili yetu yashakwisha, hata Waungwanga mmechanganyikiwa. Sisi Wakristu na Waislamu (hata wapagani - indigenous faiths) wa Tanzania ni ndugu halafu tunaelewana kabisa; hata mila zetu zinachanganya kabisa, kuna mliosilimishwa na wale tusio-silimishwa (I cannot go into details). Kama kweli mie ningekuwa Mufti Simba ningefunga safari kumfuata Kardinali Pengo na kumwomba aniambie nia yake ya hizo Nyaraka na mwendendo mzima wa misimamo yetu kuhusu dini na serikali yetu. Haya mambo ya viongozi wa dini na kukurupuka kama wahuni inaleta uchungu sana. Religions are here for uniting the people for their common goals. From the office of "Mufti Juma" to Mr. Pengo is just a walking distance. I am sure these people if they were talking to each other and having discussions they will find that they are preaching the same; the common goal for the "discrimated peolpe of Tanzania".

I think Mufti Juma and Pengo (or any body behind this); is not wishing us well. Waislam ilibidi waende moja kwa moja wawaone wakristu kuongea.

If I have a friend Mkandara who is a good muslim and I enjoy with him; Why Mufti Juma cannot have Pengo as a friend?

I think something is missing!!
 
Mkuu, mimi nimeuliza maswali machache tu mpaka sasa sijajibiwa. Napenda kujua kwanini serikali iwajibike katika suala la mahakama ya kadhi. Kwanini waislam wenyewe wasiianzishe ili iwasaidie kutimiza lengo la kiibada? Kwanini lihusishwe na maisha ya wasio waislam (katiba)?


Vile vile, kama mahakama hii ilifutwa, kwanini inatakiwa kuanzishwa upya sasa? Je, sababu gani zilizotumiwa kuifuta? Kwanini sababu hizo zinajitokeza kipindi hiki?

Naamini kuwa si lazima kuiga kila tunaloliona au kulisikia kutoka sehemu nyingine. Ni vyema tukaangalia mazingira yetu na kujiundia taasisi na ustaarabu unaotufaa sisi kwa sababu zetu. Tunaweza kuiga mambo bila kuyaelewa yakatuletea matatizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…