Mufti Zubeir amteua Sheikh Ngeruka kuwa Naibu Kadhi Mkuu

Mufti Zubeir amteua Sheikh Ngeruka kuwa Naibu Kadhi Mkuu

BARD AI

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2018
Posts
3,591
Reaction score
8,826
Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu, Abubakari Zubeir amemteua Sheikh Ally Ngeruka kuwa Naibu Kadhi Mkuu wa Tanzania na ustaadh Said Mwenda Anayekuwa Kaimu Naibu Katibu Mkuu wa Utawala na Fedha wa Bakwata.

Taarifa iliyotolewa jana Jmatano Aprili 13, 2023 na Msemaji wa Mufti, Sheikh Khamis Mataka ambaye ni Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Bakwata, amesema Mufti Zubeir kwa mamlaka aliyokuwa nayo ametumia ibara 84:3:5 ya baraza hilo, kufanya uteuzi huo.

Sheikh Mataka amesema Katibu Mkuu wa Bakwata, Sheikh Nuhu Mruma amewateua viongozi mbalimbali akiwemo Twahir Al-Musawaa kuwa mkurugenzi wa mambo ya nje, Bakwata.

“Amemteua Sheikh Othman Kaporo kuwa Mkurugenzi wa Quran na mambo ya dini Bakwata.Pia amemteua Tabu Kawambwa kuwa Mkurugenzi wa habari, mahusiano na usalama wa ndani Bakwata makao makuu,” amesema Sheikh Mataka.

MWANANCHI
 
Back
Top Bottom