Mugabe agoma kuwapigia magoti akina Kikwete, UK, US na UN.

Mugabe agoma kuwapigia magoti akina Kikwete, UK, US na UN.

_44778921_mugabe_afp226b.jpg

Muda unahesabika jongwe

Hili Jina la Jongwe sosi yake ni wapi? mbona linanitatiza?....Mwenye ufafanuzi?
 
Mambo ya vita ya kina BUSH,KIKWETE NA ZITTO NA ccm YAMEKWISHA!
WARUDI BUNGENI WADAI EPA,RICHMOND,KAGODA,KAMATI YA MADINI REPORT ETC ETC!
Time is running OUT!

NB:WATANZANIA ACHANENI NA HABARI ZA ZIMBABWE VITA HAKUNA TENA TUMESHINDA WAZALENDO!
PIGANIENI HABARI ZA EPA,RICHMOND,MADINI NK...KAMATENI MAFISADI!
RUDISHENI NCHI NA UHURU!
 
Ninawashangaa wanaosema Morgan ni kibaraka wa magharibi. Ingekuwa vizuri kama wangetupa data kuthibitisha. Magharibi kupinga uongozi wa Mugabe na Morgan kuwa kiongozi wa upinzani haina maana kuwa wana "uhusiano" fulani. Na kama hakuna uhusiano katika hilo, inakuwaje Morgan ni kibaraka? Kumbukeni wanachi wengi Zimbabwe wanampenda Morgani kuliko Mugabe (uchaguzi umethibitisha hili). Je nao ni vibaraka? Jamani pamoja na kutowapenda/kuwachukia Magharibi, tukubali jambo moja, Mugabe kachemsha ni dikteta asiyefaa kuendelea kuongoza nchi. (Refer to his statments)

Kwa upande mmoja nakubaliana na Magharibi kuwa kwa sasa Mugabe hafai, na akiachiwa ataendelea kuua na kuharibu (maana anajua ana siku chache za kuishi). Kwa upande mwingine swali langu kwao ni "why Zimbabwe?" Walikuwa wapi mauaji ya kimbari sehemu kama Burundi na Rwanda? Je hawayaoni ya Darfur na kwingineko? I suppose the reason is clear kuna wazungu Zimbabwe (Double standards) Lakini motives za Magharibi si sababu ya kuhalalisha upuuzi wa Mugabe. HAFAI, AONDOKE.
 
Back
Top Bottom