MUGALU: Persona Non Grata

MUGALU: Persona Non Grata

Mchezaji huyu ameonyesha kiwango cha chini kabisa cha uchezaji ambacho hakilingani kabisa na hadhi ya Simba na hasa pale anapokosa magoli ya wazi mechi baada ya mechi.
Waliofanya scouting walifanya makosa makubwa kumleta Simba na badala yake amekuwa akituletea machungu makubwa na pale anapo poteza nafasi nyingi za wazi. Kwa mtazamo wangu mimi naona tija yake kwenye timu ni ndogo sana na nisingependa kumuona akiichezea Simba msimu ujao. Imagine, Simba tungekuwa na Dube leo tungekuwa wapi? Simba wafanye mchakato wa kumpata Dube mchezaji mwenye viwango ambaye anastahili kuchezea Simba na sio Azam. Hapa Simba itabidi wavunje benki ili msimu ujao aje Msimbazi kuziba pengo la striker ambaye ni clinical and tactical ambaye Simba inamkosa sasa hivi. Kwaheri Mugalu, we deserve someone better. Na cocha asipoangalia ataondoka nae kwani sisi wana Simba ameisha tu-boar kupita kiasi.
Ni kweli kabisa. Mugalu hana hadhi ya kuchezea Simba. Ni galasa.
 
Mimi naona tuishie kutoa maoni tu kuwe mchezaji fulani anafaa kama alivyofanya mtoa mada kumtaja Dube lakini kwenye maamuzi tuwaachie Mo, bodi ya Simba na benchi la ufundi kwani wao ndio wanawajibika iwapo mchezaji atachemsha. Kwani kuna suala la kuvunja mkataba wakati mwingine mchezaji ana mkataba wa miaka mitatu halafu yupo mwaka wa kwanza na kashindwa kuingia kwenye mfumo wa timu. Watu wasilazimishe mchezaji wanayemuona wao mzuri basi na wengine wamuone mzuri. Usajili duniani kote ni kamari. Huyo Dube anaweza kusajiliwa Simba halafu akaenda kuwa kituko. Mimi niliwasifu sana viongozi wa Simba kumsajili Chikwende baada ya kumuangalia kwenye mechi mbili za CL dhidi ya Simba lakini sasa hivi nikisikia kaachwa kasajiliwa mchezaji mwingine mwisho mwa msimu sitashangaa.
 
Simba ikishindwa kabisa iwaache wachezaji wawili.
Mugalu na
Chikwende.

Wawachukue
Prince mugelele Dube na
Djuma Tshaabani.

Hapo biashara imeisha.
Beki bado tunazo nzuri.
Wanaweza kurekebishwa tu.

Dube apige namba 9, Djuma namba 10, Wengine kama kawaida.
Kama Kachi Kahata ataondoka basi arudi Fraga.
Hapo Simba hata ubingwa wa dunia wanachukua.
Kagere na Morrison wapewe last warning.

Sio swala la kutumia pesa nyingi ila ni swala la skauti nzuri.
Shabalala atasaidiwa na Djuma. Kapombe atasaidiwa na Duchu.

Mimi ni
mchezaji wa Zamani
 
MO usitumie pesa nyingi ya kusajiri, soma ushauri wangu hapo juu.
Tumezifunga timu nyingi za mabilioni kadhaa.
Kama tulitoka na Sevilla 4:5 tukiwa masikini kabisa.
Basi hatuhitaji pesa nyingi. Ila ni Skauting.
Chukua Dube na Djuma biashara imeisha.
Beki ni nzuri ina
Shabalala
Onyango
Wawa
Kapombe
Duchu
Kennedy ( yuko moto)
Ibrahim Ame
Gadieli.
Erasto Nyoni.
Wanatosha na wako vizuri wote. Aa wahitaji kurekebishwa tu.

Kwako MO
Kwako Mwalimu Kashasha
 
Simba striker zote zimechoka....anatakiwa atafutwe forwad mpya lakini kwa waliopo angalau mugalu na Boko ila mstaafu wa vita vya majimaji babu kagere hapana kwa kweli kachoka.
Kwa muono wangu pale simba,
Ikiwezekana wawa atupishe japo sio lazima na sioni ikitokea.
Kapombe aletewe namba mbili ya nje kama yule djuma anapatikana itafaaa.
Tshabalala atafutiwe mshindani mzawa kwani Gadiel karidhika, yupo busy na duka la nguo la mke wake.
Chikwende sioni akiadopt auzwe nje ikishindikana wampe mda.
Morrison atafutiwe mwanasaikolojia binafsi atatufaa.
Kagere na Nyoni wapewe nishai ya heshima na wastaafishwe wakigoma watupishe.
 
Unamzungumzua Erasto Nyoni, aliyeziba pengo la Lwanga mcheza rafu,
we unamjua Nyoni au unamsoma kwenye gazeti.
Kuna mpiga penati au faulo wa Simba wa kumzidi Nyoni ?
Mechi na Kaizer Chief ya Dar Nyoni na Lwanga nani alicheza vizuri ?
Na Nyoni ni Mzawa wa ndani.

We na ukae Kimya tu
 
Weee nae mbona unaongea utopolo sasa ata uyo kocha akikaa na mchezaji anampima vipi kiwango chake kama sio uwanjani ndani ya hizo dakika 90. Kila mchezaji anapimwa uwanjani ndani ya dakika 90 ambazo mashabiki ndo wanaziona sio mazoezi au kwenye vyumba vya kubadili nguo
Kocha hampimi mchezaji uwanjani, anampima mazoezini. Mugalu anatupia sana mazoezini na kumshawishi kocha. Hata Etiene Ndayiragije alizuru mazoezi ya Simba akiwa kocha wa timu ya Taifa, alikwenda studio kumsifia Mugalu
 
Simba striker zote zimechoka....anatakiwa atafutwe forwad mpya lakini kwa waliopo angalau mugalu na Boko ila mstaafu wa vita vya majimaji babu kagere hapana kwa kweli kachoka.
Kwa muono wangu pale simba,
Ikiwezekana wawa atupishe japo sio lazima na sioni ikitokea.
Kapombe aletewe namba mbili ya nje kama yule djuma anapatikana itafaaa.
Tshabalala atafutiwe mshindani mzawa kwani Gadiel karidhika, yupo busy na duka la nguo la mke wake.
Chikwende sioni akiadopt auzwe nje ikishindikana wampe mda.
Morrison atafutiwe mwanasaikolojia binafsi atatufaa.
Kagere na Nyoni wapewe nishai ya heshima na wastaafishwe wakigoma watupishe.
Nyoni si kuachwa, hapo umepotoka.
 
Unamzungumzua Erasto Nyoni, aliyeziba pengo la Lwanga mcheza rafu,
we unamjua Nyoni au unamsoma kwenye gazeti.
Kuna mpiga penati au faulo wa Simba wa kumzidi Nyoni ?
Mechi na Kaizer Chief ya Dar Nyoni na Lwanga nani alicheza vizuri ?
Na Nyoni ni Mzawa wa ndani.

We na ukae Kimya tu
Nyoni alicheza vizuri au kwa kuwa tulishinda game na kaizer walikuwa hawaji ndio unasahau makosa yake
Alipoteza pasi ngapi za wazi jambo ambalo hutolikuta kwa lwanga.
Unauliza nyoni na lwanga nani alicheza vizuri huku ukijua kabisa lwanga alitoka kwa kuumia.
 
Lwanga alipocheza na Kaizer na Nyoni alipocheza na Kaizer timu ilifanikiwa wapi.?
We hujui mpira.
Kaizer hawaji ndo maelezo gani ? Nani aliwakataza wasije ?
Wa baki kuwa mshabiki tu
 
Lwanga alipocheza na Kaizer na Nyoni alipocheza na Kaizer timu ilifanikiwa wapi.?
We hujui mpira.
Kaizer hawaji ndo maelezo gani ? Nani aliwakataza wasije ?
Wa baki kuwa mshabiki tu
Nasikitika kukuambia kuwa kama ulidhani unaufahamu mpira basi hauujui kabisa au unaangalia magoli tu.
Mtu wa mpira huelewi ukiambiwa kaizer hawaji?
Kwamba huelewi timu pinzani ikipaki basi majukumu ya kiungo wa ulinzi yanapungua?
Yaani mtu wa mpira unamfananisha lwanga na Nyoni, kwamba nyoni ni bora. Huku ukijitapa na kuwaita watu hawaujui mpira.
Unauliza wapi team ilifanikiwa? Total failure ya timu unataka kumpa mzigo lwanga?
Kwamba simba alishinda tatu sababu ya uwepo wa nyoni.
 
Back
Top Bottom