Muha vs Baniani

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2021
Posts
3,211
Reaction score
3,611
Rajesh Ajay Baghwanji amekuja toka Punjab India kuja kusimamia shamba la mikonge Tanga. Alipofika alikuta viranja wa vibarua toka Songea ambao ni Hyera, Mapunda na Komba. Kufuatia ugumu wa majina ya viranja hawa, Rajesh Ajay Baghwanji aka-google majina yao ili ajuwe Kiingereza chao ili awe anawaita kwa Kiingereza kama ifuatavyo:-
  • Hyera – japo halina maana katika Kiingereza lakini akawa anamuita Hyena.
  • Mapunda – akawa anamuita Donkey.
  • Komba – akawa anamuita Bushbaby.
Wangoni hawa hawakusoma hivyo hawakujuwa tafsiri ya majina yao kwa Kiingereza. Baadaye huko, kufuatia mgomo wao wa mishahara midogo, Wangoni hawa walifukuzwa kazi na wakaletwa Manamba saba wa Ki-ha toka Kigoma. Bagwanji akawa anaandika majina yao kama ifuatavyo:-
  • Baghwanji – taja jina yako moja moja (mmoja mmoja).
  • ARARAHANEYE.
  • Baghwanji – nini hiyo? Hiyo jina?
  • MPOROGOMYI.
  • Baghwanji – crazy! Nyie iko serious?
  • KAVINABUHIYE.
  • Baghwanji – unajuwa takosa kazi hapa nyie bhana! Nyie naleta tani kazini!
  • NTAHAMATUYI.
  • Baghwanji – I can’t absolutely work with these people. No I can’t!
  • URONYOGWAWERURAKUZE.
  • Baghwanji – my God! My God! Wewe iko salama upstairs (kichwani) kweli?
  • IZUBHADYAWEDYAKIRAMUNYO.
  • Baghwanji – mimi tapata kichaa leo hapa, iko mkosi gani? Wewe narogwa au nakula marijuana? Your names are unnecessarily too long to fit in the paper spaces provided!
  • NTUNABHONKE.
  • Baghwanji – you people, which religion are you? Nyie iko na dini gani? Back home India you can’t play soccer using these names. Mimi tamwambia MD ongeze salary ile Ngoni irudi hapa. Nyie ikalime chumvi Uvinza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…