Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Rajesh Ajay Baghwanji amekuja toka Punjab India kuja kusimamia shamba la mikonge Tanga. Alipofika alikuta viranja wa vibarua toka Songea ambao ni Hyera, Mapunda na Komba. Kufuatia ugumu wa majina ya viranja hawa, Rajesh Ajay Baghwanji aka-google majina yao ili ajuwe Kiingereza chao ili awe anawaita kwa Kiingereza kama ifuatavyo:-
- Hyera – japo halina maana katika Kiingereza lakini akawa anamuita Hyena.
- Mapunda – akawa anamuita Donkey.
- Komba – akawa anamuita Bushbaby.
- Baghwanji – taja jina yako moja moja (mmoja mmoja).
- ARARAHANEYE.
- Baghwanji – nini hiyo? Hiyo jina?
- MPOROGOMYI.
- Baghwanji – crazy! Nyie iko serious?
- KAVINABUHIYE.
- Baghwanji – unajuwa takosa kazi hapa nyie bhana! Nyie naleta tani kazini!
- NTAHAMATUYI.
- Baghwanji – I can’t absolutely work with these people. No I can’t!
- URONYOGWAWERURAKUZE.
- Baghwanji – my God! My God! Wewe iko salama upstairs (kichwani) kweli?
- IZUBHADYAWEDYAKIRAMUNYO.
- Baghwanji – mimi tapata kichaa leo hapa, iko mkosi gani? Wewe narogwa au nakula marijuana? Your names are unnecessarily too long to fit in the paper spaces provided!
- NTUNABHONKE.
- Baghwanji – you people, which religion are you? Nyie iko na dini gani? Back home India you can’t play soccer using these names. Mimi tamwambia MD ongeze salary ile Ngoni irudi hapa. Nyie ikalime chumvi Uvinza!