Stuxnet
JF-Expert Member
- Feb 12, 2011
- 13,417
- 23,310
Kiongozi wa waasi, Abu Mohammed al Jolani, ambaye kundi lake lilikuwa kitovu cha mashambulizi ya muda mfupi yaliyomaliza miongo ya udikteta nchini Syria mwishoni mwa wiki hii, ametumia miaka mingi akijaribu kujitenga na uhusiano wake wa zamani na al Qaeda.
Al Jolani ametajwa kama gaidi na Marekani nchi ambayo bado inatoa zawadi ya dola milioni 10 (£7.8m) kwa kichwa chake.
Kiongozi wa Hayat Tahrir al Sham (HTS) anasema ameacha misimamo yake ya zamani kama msimamo mkali wa kijihadi na sasa anakumbatia wa maoni mseto na uvumilivu wa tamaduni nyingine.
Jina halisi la al Jolani ni Ahmad al Sharaa - ndilo alilojulikana nalo kabla ya kujiunga na jihad, na sasa ameanza kulitumia tena, akilitaja alipokuwa akizungumza mjini Damascus Jumapili.
Sasa akiwa na umri wa miaka 42, al Jolani alizaliwa mwaka 1982 nchini Syria katika familia ya tabaka la kati iliyofukuzwa kutoka Uwanda wa Golan unaokaliwa na Israel.
Mitazamo yake ya kisiasa inasemekana kuundwa na Intifada ya Palestina ya mwaka 2000 na mashambulizi ya Septemba 11 mwaka 2001.
Wakati Marekani ilipoivamia Iraq mwaka 2003, al Jolani alikuwa mmoja wa Wasyria wengi waliovuka hadi Iraq kupigana na vikosi vya Marekani, akianzisha uhusiano na al Qaeda huko.
Alikamatwa na jeshi la Marekani nchini Iraq na alifungwa katika gereza la Abu Ghraib ambalo lina sifa mbaya.
Mwanzoni mwa miaka ya 2000, kundi la msimamo mkali la Islamic State of Iraq - lililoongozwa na Abu Bakr al Baghdadi - lilikua kutoka mabaki ya al Qaeda.
Sasa itakuwaje?