Muhammed Ali wa Jicho Pevu: A true investigation reporter

Muhammed Ali wa Jicho Pevu: A true investigation reporter

pinno

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2013
Posts
1,213
Reaction score
1,229
Am talking about Jicho pevu's reporter, a hard working guy who does everything and risk all that he has to bring the Kenyan Community the deep side and truth of stories.

Truly ,he is of his own kind, we never had a reporter of this type in any of the East Africa Country.
In Tanzania ,Kubenea of ----------- publishers, emerged but didn't last and he was only political based. Reporting political scandals only.

And back in the days we had Jerry Muro, with his Usiku wa Habari Tv show. But he also didn't last long, I think Tanzania Government is soo good in suppressing the media and turning their faith.

Muhammad Ali of Jicho pevu is our media Muhammad Ali, a true hero just like Muhammad Ali the Boxer.

I have watched some of his reports including:-

Makri ya Injili

Mihadarati.

Report ya ship piracy

Na nyingine kadha wa kadha I have no objection than to agree kuwa Muhammad Ali is the best.
 
Kwa kweli huyo jamaa namkubali kwa jinsi anavyofanya kazi yake. Mungu akulinde Muhammed Ali
 
Jamaa amefanikiwa kwa sababu aliamua kujiweka mbali na rushwa. Ukiachana na rushwa unaweza kufanya kazi yako vizuri na dunia nzima ikakujua.
Kwa wanahabari wengine ni ngumu kuwa kama Moha, kwa sababu ya tabia yao ya kujitegesha kwa vigogo ili wapate rushwa ya pesa, mali au hata vyeo serikalini.

Moha kwa kufanya kazi yake amekuwa kipenzi cha Wakenya kiasi kwamba sio rahisi kumuangamiza kutokana na anachokiandika, wakihofia taharuki ya wananchi. Nakumbuka kuna wakati alitangazwa kafa ili kupima itakuwaje na matokeo yake taharuki ya Wananchi iliwafanya wagundue nguvu ya Moha, wamemwacha.

Wengi walidhani angeangamizwa baada ya kufichua kuhusu vifo vya Saitoti, Mwagatu, Rogo, Chemorei na wengine, lakini bado ameendelea kusimama. Waandishi wengine wajifunze kukataa rushwa ili wafanye kazi.

Muro wala hakuwa mahiri, alikuwa akiwaripoti wanaogoma kuzuia story isirushwe kwa kumpa rushwa, ndio ripoti zake zilikuwa za polisi wa ngazi za chini na Wachina ambao huwa hawatoi rushwa.

Ndio maana alikamatwa akiwa na genge la matapeli na wala rushwa wakubwa kama akina Deo Ngassa ambao maisha yao yanaendeshwa kwa rushwa kubwa za media na utapeli.

Sifa ya Kubenea iko wazi katika kazi yake, ni mtu ambaye unaweza kumfananisha na Moha, kwani licha ya kubanwa na serikali lakini amekuwa akifanya kazi kwa ujasiri. Hajitegeshi apewe rushwa, kajipambanua kuwa hataki rushwa.

Ni kama Moha alipoweka hewani mazungumzo yake na Mhindi mmoja aliyetaka kumpa rushwa ya nyumba ya kifahari ili asirushwe hewani hewani kwenye makala ya mihadarati.

Ova
 
Pamoja na kukataa rushwa ila BAADHI/WENGI ya waandishi tulionao Tanzania ni MAKANJANJA. Kanjanja hawezi kuwa mweledi na kukataa rushwa ni ngumu mno kwake
 
hivi vipindi vyake huwa vinarushwa na tv gani ya kenya na siku gani?
 
Natamani kumjua huyu mtu. Niko vijijini huku hakuna mambo ya tv
 
Mie simkubali Moha...yeye ni mtu ambaye anpenda ktumia half-truths and whole lies. Ndio, anajaribu pahali pengi, lakini yeye anapenda kuwasifu magaidi wa al-shabaab. Hutawahi kumsikia akiwaita al-shabaab "Magaidi." Bali utamsikia akiwaita wapiganaji. Hii ni dalili ya wale wote wanaoabudu al-shabba na umwagaji wa damu. Hata al-jazeera wana huo upuzi.

Jambo lingine pia ni kuwa wao hudanganyika upesi sana. Kuna wakati fulani walichezewa shere (nikidhani na majasusi wa Kenya,) na kudanganywa kuwa felicen Kabuga yupo Kenya. Walipeperusha picha za mwananchi wa Kenya kisha walipopatikana, hawakuomba msamaha. Huu ni unafiki wa hawa watangazaji.
 
Sifa za Mohamed Ali
1. Kutumia lugha sanifu
2. Upangaji bora wa mtiririko wa makala
3. Umahiri katika masimulizi
 
Mie simkubali Moha...yeye ni mtu ambaye anpenda ktumia half-truths and whole lies. Ndio, anajaribu pahali pengi, lakini yeye anapenda kuwasifu magaidi wa al-shabaab. Hutawahi kumsikia akiwaita al-shabaab "Magaidi." Bali utamsikia akiwaita wapiganaji. Hii ni dalili ya wale wote wanaoabudu al-shabba na umwagaji wa damu. Hata al-jazeera wana huo upuzi.

Jambo lingine pia ni kuwa wao hudanganyika upesi sana. Kuna wakati fulani walichezewa shere (nikidhani na majasusi wa Kenya,) na kudanganywa kuwa felicen Kabuga yupo Kenya. Walipeperusha picha za mwananchi wa Kenya kisha walipopatikana, hawakuomba msamaha. Huu ni unafiki wa hawa watangazaji.
Hii ndio maana jf naipendaga..
 
serikala ya Uhuru Kenyatta inataka kummaliza, yuko mafichoni kwa sasa. Ina huzunisha sana kuona mtu anakuwa adui wa nchi kwa kuwa amekataa rushwa na anafanya kazi zake bila ushawishi wa wana siasa.
 
serikala ya Uhuru Kenyatta inataka kummaliza, yuko mafichoni kwa sasa. Ina huzunisha sana kuona mtu anakuwa adui wa nchi kwa kuwa amekataa rushwa na anafanya kazi zake bila ushawishi wa wana siasa.

The new bill is targetting folks like him!...God forbid.
 
Mohammed Ali ni mtu jasiri katika kizazi cha uandishi cha karne hii katika nchi za Afrika Mashariki na pengine Afrika nzima kwa ujumla. Mungu amlinde huyu mja wake.
 
Namkubali sana huyu mwandishi, bado sijaona wa kumfananisha nae Mungu amlinde. Ni tunu ya waKenya
 
What a talented guy
Ukiangalia makala zake kama zile za kifo cha George Saitoti na hata ile ya westgate. Utampenda. Hes detailed sana
 
Back
Top Bottom