MUHAS:- Tafiti zinaonesha tiba asili za UVIKO 19 zilikuwa na matokeo chanya.

MUHAS:- Tafiti zinaonesha tiba asili za UVIKO 19 zilikuwa na matokeo chanya.

Mpinzire

JF-Expert Member
Joined
Jan 18, 2013
Posts
7,503
Reaction score
13,463

Mfuko wa Utafiti wa UVIKO-19 wa Amne Salim:​

Jumla ya tafiti nane zimeweza kuzalishwa na watafiti mbalimbali kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili (MUHAS) kufuatia ufadhili uliotolewa na familia ya aliyekuwa Waziri Mkuu Salim Ahmed Salim uliolenga kuenzi kifo cha mke wake, Amne Salim, aliyefariki kwa ugonjwa wa UVIKO-19 hapo Oktoba 20, 2020. Ukipewa jina la Mfuko wa Utafiti wa UVIKO-19 wa Amne Salim, familia ya Dk Salim ilitoa Shilingi milioni 100 kwa ajili ya kufadhili tafiti mbalimbali juu ya janga la UVIKO-19, kwa lengo la kuwawezesha watunga sera na wafanya maamuzi kulifahamu janga hilo vizuri na kama Tanzania inaweza kutumia uzoefu wa UVIKO-19 kukabiliana na majanga mengine. The Chanzo imezungumza na watafiti watatu walionufaika na ufadhili huo kwa lengo la kufahamu tafiti zao zilihusu nini na matokeo gani waliweza kupata, ikiwa ni sehemu ya kueneza matokeo hayo kwa jamii.

Matokeo ya utafiti huo yalibaini kuwa tiba asili kama vile kujifukiza, kunywa tangawizi iliyochanganywa na malimao kulileta matokeo chanya kwa wale waliokajihisi wanadalili za Uviko 19. Ata hivo Muhas imeiomba Serikali kutumia matokeo hayo kuweza kujindaa na magonjwa mengine ambayo yanaweza kuja huko mbele na kutotegemea wafadhili wa nje pekeake.

 
Back
Top Bottom