Muheza: Baraza la Madiwani lapiga kura ya kutokuwa na imani Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Juma Mhina

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Februari 27, 2026 limeazimia kwa pamoja kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya watumishi 14 wa halmashauri hiyo kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya Muheza

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salimu Sechambo, amesema jumla ya madiwani 50 kati ya 51 wameunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji, wakieleza uamuzi huo unalenga kulinda rasilimali za umma na kurejesha uwajibikaji ndani ya halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Jumaa Muhina amesema Hana Cha kusema Zaidi ya Alhamdulillah.

Huyu mwamba kweli achunguzwe anaviashiria vyote vya upigaji!
Alikuwaga Longido nadhani alitolewa kisa upigaji na uajibikaji mbovu sn, akapewa Ngorongoro then Muheza
 
Wakuu,

Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Februari 27, 2026 limeazimia kwa pamoja kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma

Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya watumishi 14 wa halmashauri hiyo kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya Muheza

Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salimu Sechambo, amesema jumla ya madiwani 50 kati ya 51 wameunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji, wakieleza uamuzi huo unalenga kulinda rasilimali za umma na kurejesha uwajibikaji ndani ya halmashauri.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Jumaa Muhina amesema Hana Cha kusema Zaidi ya Alhamdulillah.

Nzega na Muheza wapi na wapi?
 
Hana cha kusema zaidi ya "alhamdudulahi" 😄

Ova
 
Back
Top Bottom