Wakuu,
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza mkoani Tanga Februari 27, 2026 limeazimia kwa pamoja kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo kufuatia tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma
Hatua hiyo imekuja siku chache baada ya watumishi 14 wa halmashauri hiyo kusimamishwa kazi kwa tuhuma za ubadhirifu wa fedha katika utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la halmashauri ya Muheza
Akizungumza kwa niaba ya madiwani, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Salimu Sechambo, amesema jumla ya madiwani 50 kati ya 51 wameunga mkono hoja ya kutokuwa na imani na Mkurugenzi Mtendaji, wakieleza uamuzi huo unalenga kulinda rasilimali za umma na kurejesha uwajibikaji ndani ya halmashauri.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Jumaa Muhina amesema Hana Cha kusema Zaidi ya Alhamdulillah.