MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES Best University in Tanzania, 1610th Worlwide

MUHIMBILI UNIVERSITY OF HEALTH AND ALLIED SCIENCES Best University in Tanzania, 1610th Worlwide

Ufundishaji Bongo sio mbaya sana. Nimesoma Bachelor UDSM na Masters UK tena kwenye chuo bora, sijaona tofauti sana kwenye ufundishaji ila matatizo yako kwenye mambo yafuatayo ambayo yanaleta utofauti:


  • Kuchapisha/publication- Tanzania unaweza kukuta mtu eti ni Prof anakitabu kimoja na vi-article vichache wakati kwa wenzetu mtu ni PhD tu maandishi kibao. Wengine ndio baada ya PhD hata kuandika wamesahau. Mtu ni Lecturer hata kutayarisha notes hawezi kazi kupiga copy vitabu vya watu! Huwezi kuona Dr/Prof anagawa copy ya kitabu cha mtu kwa wenzetu.
  • Pesa za research zipo za kumwaga, ni jitihada yako kuziomba na kuzitumia.
  • Wataalamu/waalimu wanafanya consultations na si kufundisha tu. Hii inawafanya wawe na mambo mengi ya kufanyia tafiti, na baada ya hapo wanazichapa, publish.
  • Vipimo vya uelewa hasa kwa UK sio mitihani pekee. Nilishangaa sana hata kwa level ya Bachelor kuna baadhi ya programs mwanafunzi anapimwa kwenye maabala/ mfano computer au kuandika essay kwenye jambo fulani basi. Hivyo wao sio kila somo lazima ulifanyie mtihani wa kukaa kwenye meza masaa matatu mwisho wa semester bali unaweza kuingia library ukafanya kama ka-utafiti na ukaandika paper, basi. Jambo hili linawajenga sana katika uandishi.
  • Collaboration - ukiangalia moja ya vigezo vya vyuo bora ni collaboration. Vyuo vyetu vinapenda kujitenga sana, hasa UDSM. Nakumbuka wakati nasoma tuliwahi kuwaambia chuo pale Faculty of Commerce, (sasa UDBS) waangalie ku-incorporate sylllabus ya NBAA ili wahitimu wa BCom hasa Accounting na Finance wapate exemptions zaidi wakasema wao hawatoi degree ili baadae upate CPA. Kwamba CPA ni jambo lako binafsi hapo baadae. Wakaja na jeuri kwamba, by the way, CPA exams inakuwa moderated na walimu wa UDSM wakasahau kwamba NBAA ni independent institution hivyo inamaamuzi yake. Lakini baada ya mikwaruzano NBAA wakasalimu na kuendelea kutoa exemptions kwa BCom Accounting. Ila walifanya hivi kwa kuwapa uhuru UDSM wafundishe wanavyotaka wakati vyuo vingine vilipewa exemptions baada ya program zao kuwa scrutinized na NBAA.
  • Suala hili hili la ubabe wa kijinga wa UDSM unawafanya wanafunzi wa BAF Mzumbe wapate exemptions 7 kwenye ACCA,UK wakati BCom Accounting na BCom Finance ya UDSM wanapata 4 exemptions. Naongelea sehemu ninayoifahamu, yapo mengi naamini juu ya collaboration ambayo inabidi tubadilike kuendana na wakati na ulimwengu wa taaluma. Niongezee hapa kwa ACCA, Mzumbe kwa kweli kwa hili nawapongeza kwani wanapata exemptions kuliko hata baadhi ya vyuo vya UK. Ni kwamba they enjoy all exemptions, na masomo mawili ambayo hawapati exemptions kwenye ACCA ni Tax, kwa sababu Tax ni muhimu na wengi wanakuwa hawajaisoma, na pia kwa sababu ya different tax regime (Tanzania Vs UK Tax). La pili ni Financial Reporting ambalo katika vyuo haliwi covered vizuri. Baada ya hapo, wanafunzi wa Mzumbe wanaingia kwenye ACCA Professional Stage ambayo kila mtu lazima afanye. Nisiwachoshe na mambo ya BCom.
  • Citation - website hata za vyuo vyetu ziko poor. Ebu angalia website ya chuo chochote hapa nchini. Taarifa mpaka uzifuate ofisini hata mambo ya kawaida sana. Hakuna kazi za waalimu kwenye mitandao, unategemea nini? Website za vyuo vyetu hazipati HIT ( yaani watu hawazitembelei) kwa sababu hazivutiii, hazina taarifa, wakati kuna mengi ya kuweka kwenye mitandao yetu. Si jambo la kushangaza uka-click link fulani ukaambiwa ..under construction..au document unavailble..Usitegemee chuo kikapata rank nzuri.
  • Employability and graduate satisfaction..Wenzetu wanajali sana kuajiriwa kwa wanafunzi wao. Na hii ndio namba moja kwao. Vyuo vina-fight kutafuta waajiri kuja kuajiri hata chuoni kwa wanafunzi wanaomaliza. Kuna Career Centres zinawafundisha wanafunzi employment skills. Hizi centre kuna watu full time wameajiriwa kwa ajiri si ya kufundisha bali kutatua matatizo ya wanafunzi yanayohusiana na kuajiriwa.
Jamani mambo ni mengi..kuna mengi yakubadilisha.

hili lakuajiriwani kweli utakuta kila ikikaribia wanafunzi kumaliza makampuni yanaliikwa kuja kufanya interview. maprof wa wenzetu hawajisikii vzr wanafunzi wao wanapofeli wakati sisi ni sifa
 
Duuh! Enzi hizo za term system, MUHAS enzi hizo MUCHS, Sapu ilikuwa kawaida, Disco haikuwa ajabu, ukipata C, unashangilia na kwenda kunywa bia pale Mashine "BAR" kwa Mzee Njau. Anyway hongereni Ntogwi, Nyambo na marehemu wote mungu awalaze. Siku hizi MMED wanasoma wale waliotoka IMTU, HKMU na vyuo vingine vya magumashi.

siku hizi mmed wanaogopa hata kufundisha wanafunzi wodini kwani wako shallow kuliko undergraduate wenyewe. Duh muhas imepoteza sana kizazi cha watz wenye akili nzuri enzi hizo kwa kuwajazia makalai ya kutosha. Siku hizi kusoma medicine ni hela tu, hukuti mtoto wa maskini kule
 
hongera na machifu waliotujazia makalai mpaka tunaona uvivu kwenda kusoma mmed!

Ni kitu cha ajabu sana hawa machifu wanakupa makarai halafu wanashangaa watu hawaendi kusoma mmed.... Wanakufa wakiongoza vitengo huku wakiongeza mkataba kila siku na hawataki to train juniors kuwa wao siku wasipokuwepo.....
 
Back
Top Bottom