A
Anonymous
Guest
Nimeenda mara kadhaa kwenye haya matawi mawili ya Hospitali ya Taifa Muhimbili (Upanga & Mloganzila), chanjo ya Tetanus haipo kwa zaidi ya mwaka sasa.
Mara ya kwanza nilienda Upanga kama miezi 8 iliyopita baada ya mwanangu kung'atwa na mbwa, wakamchoma tu chanjo ya kichaa cha mbwa, chanjo ya Tetanus nikaambiwa kwa sasa hawana labda niende vituo vya afya au nikajaribu Mloganzila. Kule Mloganzila nako nilipewa jibu lilelile kwamba hiyo chanjo kwa sasa hawana.
Juzi tena nilipata ajali, nikapata michubuko mwilini, nikatibiwa hapo emergency ya Upanga, ila kwa mshangao tena wakawa hawana chanjo ya Tetanus na jibu lao ni lilelile kwamba kachome vituo vya afya. Nimeenda tena Mloganzila napo hawana.
Sasa najiuliza inakuwaje kwa hospitali ya level ya juu kabisa kama National Hospital inakosa chanjo ya muhimu kama hii. Kwa siku wanapokea majeruhi wangapi, hawaoni ni usumbufu kwa wateja kwenda kuhangaika huko kwingine kutafuta chanjo ya Tetanus ambayo kuiweka hapo kwao ni jambo dogo tu kwani ni bure.