Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Nikijibu maswali niliyopokea kuhusu kitabu cha wasifu wa Mwalimu Nyerere:
Abdul Katalango kuwa na ustahamilivu kwani kazi yeyote ya mikono ya binadamu haiwezi kukosa kasoro.
Hawa waandishi ni wa ngazi za juu sana katika kiwango chochote kile na jamii itanufaika sana kwa kazi hii yao.
Kuna mengi wameyaeleza ya Mwalimu mimi sikuwa nayajua lakini yapo mengi yamewapita na huu ni ubinadamu.
Nimekuwa narashiarashia Vol. 1 ya kitabu kinamueleza Mwalimu alivyofika Dar es Salaam 1952 aliikuta TAA katika hali gani ya siasa.
Bahati mbaya TAA Political Subcommitee (Kamati Ndogo ya Siasa) iliyoundwa 1950 iliyokuwa inashauriwa na Earle Seaton haikutajwa.
Wajumbe wake walikuwa Dr. Vedasto Kyaruzi, Abdulwahid Sykes, Hamza Mwapachu, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo, Steven Mhando na John Rupia.
Kitabu kinaeleza kuwa Nyerere alipofika Dar es Salaam aliikuta TAA imeshikiliwa na Sykes watatu Abdul na wadogo zake wawili si kuwa ilikuwa chini ya uongozi wa vijana wasomi akina Mwapachu, Kyaruzi na wazee wenye sauti katika wenyeji wa Dar es Salaam kama Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Sheikh Said Chaurembo.
Ukiacha kuunganisha nguvu hizi mbili mengi ya huko mbele hayataeleweka.
Umuhimu wa Kamati hii na wajumbe wake uko katika matayarisho ya kutengeneza mapendekezo ya katiba ya Tanganyika kazi iliyoletwa na Gavana Twining mwaka wa 1949 na baada ya kushindikana kukubaliwa mapendekezo haya ndipo juhudi zikapamba moto kuunda kuitia nguvu TAA majimboni na kuunda TANU.
Sasa huyu Earle Seaton jina lake hapo halipo lakini ndiye aliyekuwa akiwashauri vipi TAA iitambuke serikali ipeleke nguvu zake UNO kwenye Baraza la Udhamini wa Nchi zilizokuwa chini ya utawala wa Waingereza kwa kudai uchaguzi wa "One Man One Vote."
Elewa kuwa hii ni 1950 na Mwalimu hajafika Dar es Salaam.
Moto ulikuwa unafukuta na serikali kujihami ikawa inawaondoa viongozi wa TAA Dar es Salaam kuwapeleka majimboni kuidhoofisha TAA.
Huu ni mfano mmoja tu.
Antar Sangali kuna vitu naviona vinatoa ladha kubwa katika historia ya Mwalimu kwa vipi juu ya ugeni aliokuwanao Dar es Salaam aliweza kwa haraka kuingiliana na watu na katika akautumia uhusiano huu kukubalika na kuijenga TANU kwanza Dar es Salaam kisha nchi nzima.
Kitabu kinasema Nyerere aliishi nyumbani kwa Ally Sykes Mtaa wa Kipata.
Nyerere angeliishi Kipata angejuana na baba yangu hapa kwa kuwa baba yangu alikuwa kapanga nyumba ya Liwali wa Songea Sheikh Abdallah Simba nyumba inayokabiliana na nyumba ya Kleist Sykes ambayo Ally Sykes ndiyo akiishi na mkewe Bi. Zainab.
Ingekuwa hivi baba yangu, Said Salum Abdallah angemjulia Nyerere nyumbani kwa Ally Sykes.
Baba yangu kakutana na Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Kama urafiki Nyerere rafiki yake, mwenzake na msiri wake alikuwa Abdul na kwa kauli yake amesema katika hotuba ya kuaga Ukumbi wa Diamond kuwa Kasella Bantu ndiye aliyempeleka kwa Abdul.
Nini umuhimu wa nyumba hii?
Nyumba hii ndipo kulipokuwa na kituo cha harakati zote za Waafrika Dar es Salaam dhidi ya ukoloni toka wakati Kleist Sykes yu hai.
Nyerere kajuana na watu wengi nyumba hii wanachama wa kawaida wa TAA na viongozi.
Ukimtoa Nyerere nyumba hii ya Mtaa wa Aggrey ukampeleka Kipata kwa Ally Sykes unapoteza historia kubwa ya Mwalimu.
Nyerere hakupata kuishi nyumba moja na Ally Sykes Mtaa wa Kipata.
Nyumba ya Ally Sykes umaarufu wake ni kuwa pale ndipo ilipokuwa, "printing press," ya kuchapa mikaratasi ya "uchochezi,"dhidi ya serikali kazi hiyo akiifanya kwa siri yeye mwenyewe Ally Sykes.
Kwa wakati ule nyumba ya Abdul ilikuwa nyumba ya kisasa yenye vikorombwezo vyote.
Ilikuwa nyumba mbili katika moja.
Nyumba kubwa mlango mkubwa unaelekea Mtaa wa Stanley na nyumba ndogo Mtaa wa Sikukuu.
Hii nyumba ndogo ndiyo akiishi Abbas Sykes na ndiyo akaondolewa pale na kaka yake kumpisha Nyerere mwaka wa 1955 baada ya Mwalimu kuacha kazi.
Mipango yote ya TANU ikifanyika nyumba hii.
Katika nyumba hii ndipo Mama Maria alipojuana na Bi. Mwamvua bint Mrisho mke wa Abdul Sykes na wakawa mashoga wakubwa.
Antar Sangali Ni muhimu mno mchango wa Earle Seaton ukafahamika toka mwanzo ili itakapokuja kuelezwa ilikuwaje Japhet Kirilo akawa mmoja kati ya watu 17 waliounda TANU ijulikane kuwa yeye ndiyo Mtanganyika wa kwanza kuzungumza UNO mwaka wa 1952 kufuatilia kwa Wameru kupeleka madai ya kudhulumiwa ardhi yao na Wazungu na Earle Seaton ndiye aliyetayarisha ile "petition," kupitia Meru Citizens Union.
Hapa utamuona Seaton akitoka kuisaidia TAA Makao Makao Makuu kuandika waraka kwa Gavana Edward Twining anakuja kuwasaidia Wameru kutengeneza "petition," kudai haki yao UNO.
Hili la kwanza.
Pili utakuja kujua nafasi ya Mzanzibar, Sheikh Hassan bin Ameir ambae alikuwa sheikh na mwanasiasa pia pale patakapozuka mgongano baina yake na Julius Nyerere mara tu baada ya uhuru kupatikana ikabidi Sheikh Hassan bin Ameir akamatwe na kufukuzwa Tanganyika akarudishwa kwao Zanzibar.
Sheikh Hassan bin Ameir ana historia kubwa kwa Nyerere binafsi, TANU na katika historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
Huyu kushoto ni Earle Seaton yuko na Mwalimu Nyerere hapa ni baada ya uhuru.
Seaton alikuwa Wakili kutoka Bermuda akifanya shughuli zake Moshi na alikuwa rafiki wa Abdul Sykes.
Abdul ndiye aliyemtia TAA 1950 kwa mlango wa nyuma kama mshauri kuhusu Mandate Territories.
Pucha:Ally Sykes na Julius Nyerere
Kulia Lawi Sijaona, Abdul Sykes, Julius Nyerere na Dossa Aziz tafrija ya kumuaga Nyerere safari ya pili Ukumbi wa Arnautoglo UNO 1957. Picha hii alinipa Kleist Sykes.
Kulia Abdulwahid Sykes na mkewe Bi. Mwamvua bint Mrisho kwenye Garden Party Government House sasa Ikulu, 1950s. Hawa ndiyo walimpokea Julius Nyerere 1952 na 1955 alipoacha kazi wakamkaribisha nyumbani kwao yeye na Mama Maria.
Sent using Jamii Forums mobile app