Muhimu kufahamika katika wasifu wa Julius Nyerere

Muhimu kufahamika katika wasifu wa Julius Nyerere

Haya umeshayaandika sana, nimeshasoma kitabu chako mwaka 2013 na nilinunua kwa pesa yangu kutoka msikitini nikiwa DSM na nilishakuambia hilo hapahapa...labda wewe huna kumbukumbu

Ninaposema wewe ni mdini Nina uhakika na hilo kutokana na baadhi ya kurasa katika baadhi ya vitabu vyako...ningekuwa nipo karibu navyo ningeviscreeshort nikuoneshe na uongo wako pia.

Pia nimeshasikia mjadala wako ukihojiwa na Azam TV kuna mengi ya uongo uliyoyasema na kusema kuwa ulifanya utafiti.

Uongo ni dhambi na huu mwezi mtukufu kwenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Azarel,
Hilo la wewe kuniita mdini halinisumbui lakini hapa tunajadili Wasifu wa Julius Nyerere.

Ikiwa una ushahidi kuwa mimi muongo eleza huo uongo hapa usomwe nami nijibu.

La unataka tujadili udini mimi niko tayari fungua uzi nitakuja kuchangia.

Kuwa umenunua kitabu changu msikitini wala si jambo la ajabu na sijui kwa nini huoni Cathedral Bookshop hapo St. Joseph's.

Nimenunua vitabu vingi hapo na wala sijafanya kuwa ni kioja cha kuitangazia dunia.

Au sisi haturuhusiwi kuwa na bookshop msikitini?

Kitabu cha Bergen (1981) na Sivalon (2002)vyote nimenunua hapo kwenye bookshop ya kanisa.

Tuendelee na mjadala wa Wasifu wa Julius Nyerere:

CHIEF DAVID KIDAHA MAKWAIA NA DR. WBK MWANJISI KATIKA WASIFU WA JULIUS NYERERE - JamiiForums

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiki kitabu cha Nyerere sina hakika kama utakipenda, sababu hakijawatukuza Abdul Sykes na Hassan Ameir, hakijamtaja Abdul Sykes vile wewe unataka.
 
Hiki kitabu cha Nyerere sina hakika kama utakipenda, sababu hakijawatukuza Abdul Sykes na Hassan Ameir, hakijamtaja Abdul Sykes vile wewe unataka.
Laki...
Kitabu ni kizuri sana kabisa na nimekipenda kwa sababu kubwa mbili kuwa kwanza kitabu cha Abdul Sykes kipo katika bibliography na kimerejewa mara nyingi sana.

Pili kitabu kimenifunza mengi sana ambayo sikuwa nayajua.

Ama kuhusu Abdul Sykes kitabu nimekipenda kwa kuwa kimenipa fursa ya kutembea kwenye mistari yake na kuandika yale ambayo Abdul yamemuhusu lakini hayakuelezwa sawasawa na hili nimefanya kwa wazalendo wengine.

Nadhani umesoma huko nyuma niliposahihisha kuhusu ni nyumba ipi Nyerere aliishi, ni Stanley Street kwa Abdul Sykes au Kipata kwa Ally?

Hapa nikasherehesha sana.

Naamini umeona jinsi nilivyowaadhimisha Chief David Kidaha Makwaia na Dr. Wilbard Mwanjisi ili michango yao ifahamike.

Kitabu nimekipenda kwa kuwa kinanisadikisha katika mengi.

Vipi nisikipende kitabu hiki?

Kuna kitabu cha Shaaban Robert kinaitwa, "Ashiki Kitabu Hiki."

Nami nasema maneno haya haya kwa kitabu hiki "Ashiki wasifu huu wa Julius Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said, kwa nini wapendwa wako wote waliokuwa TANU waligombana na Nyerere? Ally Sykes, Abdul Sykes, Chief Kidaha, Dr. Mwanjisi, Hasan Ameir, Titi Mohamed, kwa hiyo kwako wewe sifa kubwa ya kuwa mzalendo ni kugombana na Nyerere?
 
Abdul Sykes umekosea yeye hakupata kughitilafiana na Nyerere ungesoma kwa utulivu "commentary" yangu ya Chief Kidaha na Dr. Mwanjisi hili nimelieleza.

Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza kwa kirefu mgogoro wa EAMWS na wahusika wake wote pamoja na Nyerere.

Ukisoma utajua nini ilikuwa sababu ya mgogoro ule na utakutana na Sheikh Hassan Bin Ameir, Tewa Said Tewa, Titi Mohamed, Bilal Rehani Waikela, Mussa Kwikima kwa kuwataja wachache.

Tatizo kubwa ilikuwa ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Waislam ndani ya ardhi ya Tanzania.

Ally Sykes na Nyerere walikosana katika mtazamo wa maisha.

Ally Sykes alikuwa mfanyabiashara na alitajirika sana hasa baada ya uhuru.

Hii ilikuwa kinyume ya Leadership Code kama ilivyoelezwa katika Azimio la Arusha la mwaka wa 1967.

Kiongozi hakutakiwa kuwa bepari.

Hapo ndipo walipotofautiana.

Kitabu cha wasifu wa Julius Nyerere kimeeleza hili.

Hii ya "wapendwa wangu," kugombana na Nyerere sijui una maana gani maana ugomvi una pande mbili kwa maana kuwa Nyerere pia akigombana na wenzake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mohamed Said,

..are there any "bomb shells" in the biography.

..mimi huwa sipendi vitabu ambavyo havina mambo ambayo hatukuyajua na hatukutegemea yalitokea.

..unadhani waandishi walikuwa wako wakati wakiandika, au waliandika huku wako "guarded"?
 
JK,
Tatizo ninaloliona ni kuwa wanahangaishwa na legacy yake.

Wanataka awe yeye ndiye muasisi harakati za haki za Waafrika lakini nafasi ilipokuwa wazi yeye badi mtoto na harakati za kuunda TANU kuanzia 1950 hakuwepo pia.

Vipi utawapiku akina Sykes ilhali African Association kaasisi baba yao na watoto wake wakaasisi TANU?

Hapa ndipo lilipo tatizo.

Kubwa zaidi vipi mchango wa Waislam tuupuuze pamoja na wazalendo wake wake kwa waume.

Je wawe kimya kuhusu mchango wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na viongozi wake kama Sheikh Hassan bin Ameir na Ali Mwinyi Tambwe?

Unaweza kuandika historia ya uhuru wa Kenya bila kuwataja Wakikiyu na Mau Mau?

Unaweza kuandika historia ya uhuru wa Kenys bila kuwataja Wakikiyu na Mau Mau?

Sent using Jamii Forums mobile app

..labda kingeandikwa na mtu ambaye hakuwa na mahusiano ya moja kwa moja na Mwalimu ingesaidia.

..Mwalimu ametukuzwa kwa kipindi kirefu. Namheshimu sana Mwalimu, lakini nadhani ametukuzwa kwa kipindi kirefu.

..Sie wengine tumetosheka na sifa kemkem za Mwalimu, sasa tuna hamu ya kusoma habari ambazo zinam-humanize Mwalimu.
 
Zipo za Nyerere kama binadamu mwingine yule na nilishtuka nilipozisoma na kuona source ni mimi.

Kwa kweli niliogopa sana maana sisi kama watoto tuna mipaka yetu ingawa yapo tuliyoyaona kwa macho yetu kwani hatukuwa wadogo hivyo.

Lakini nilifarajika kuona Abbas Sykes yeye kaeleza kila kitu na hapo roho yangu ikatua nikampigia simu rafiki yangu, acha tucheke.

Mimi walioponiuliza niliwagusia tu kuwa chama kikubwa kama kile na hawa wazee wetu wastani wa miaka yao ilikuwa miaka 30 purukushani lazima zitakuwapo.

Hii sehemu itawashangaza wengi na pia itawachekesha sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Laki...
Kitabu ni kizuri sana kabisa na nimekipenda kwa sababu kubwa mbili kuwa kwanza kitabu cha Abdul Sykes kipo katika bibliography na kimerejewa mara nyingi sana.

Pili kitabu kimenifunza mengi sana ambayo sikuwa nayajua.

Ama kuhusu Abdul Sykes kitabu nimekipenda kwa kuwa kimenipa fursa ya kutembea kwenye mistari yake na kuandika yale ambayo Abdul yamemuhusu lakini hayakuelezwa sawasawa na hili nimefanya kwa wazalendo wengine.

Nadhani umesoma huko nyuma niliposahihisha kuhusu ni nyumba ipi Nyerere aliishi, ni Stanley Street kwa Abdul Sykes au Kipata kwa Ally?

Hapa nikasherehesha sana.

Naamini umeona jinsi nilivyowaadhimisha Chief David Kidaha Makwaia na Dr. Wilbard Mwanjisi ili michango yao ifahamike.

Kitabu nimekipenda kwa kuwa kinanisadikisha katika mengi.

Vipi nisikipende kitabu hiki?

Kuna kitabu cha Shaaban Robert kinaitwa, "Ashiki Kitabu Hiki."

Nami nasema maneno haya haya kwa kitabu hiki "Ashiki wasifu huu wa Julius Nyerere.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mzee wangu una uwezo mkubwa sana kichwani, hasa kukabiliana na hoja na matusi ya vijana wasio na adabu. Nadhani namna unavyowajibu wabajiona wapumbavu sana.

Nikuombe mzee wangu Kama itakupendeza nami nipate kusoma huo wasifu wa Mwalimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
JK,
Tatizo ninaloliona ni kuwa wanahangaishwa na legacy yake.

Wanataka awe yeye ndiye muasisi harakati za haki za Waafrika lakini nafasi ilipokuwa wazi yeye badi mtoto na harakati za kuunda TANU kuanzia 1950 hakuwepo pia.

Vipi utawapiku akina Sykes ilhali African Association kaasisi baba yao na watoto wake wakaasisi TANU?

Hapa ndipo lilipo tatizo.

Kubwa zaidi vipi mchango wa Waislam tuupuuze pamoja na wazalendo wake wake kwa waume.

Je wawe kimya kuhusu mchango wa Al Jamiatul Islammiya fi Tanganyika na viongozi wake kama Sheikh Hassan bin Ameir na Ali Mwinyi Tambwe?

Unaweza kuandika historia ya uhuru wa Kenya bila kuwataja Wakikiyu na Mau Mau?

Sent using Jamii Forums mobile app
Haiwezekani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nsharighe,
Haya ndiyo matatizo yanayowakabili si waandishi wa habari zozote za Nyerere hata watangazaji ambao wamepata kunihoji kuhusu Mwalimu wana mambo yamo kichwani mwao mfano kuwa yeye peke yake ndiye alikuwa mjuzi wa kila kitu.

Kuna suala la katiba ya TANU kuwa Nyerere ndiye aliyeiandika na katika Wasifu hivyo ndivyo ilivyoandikwa.

Ukweli ni kuwa katiba ya TANU ilinakiliwa neno kwa neno kutoka kwa katiba ya Convention People's Party (CPP)ya Kwame Nkrumah wa Ghana na sababu yake ni kuwa ikiwa ilipitishwa Ghana na Waingereza haitakataliwa Tanganyika.

Hiki kipande cha katiba bado sijakutananacho.

Hotuba ya Nyerere UNO 1955.

Abdul Sykes alikuwanayo hotuba hiyo toka 1950 na ni kazi ya TAA Political Subcommittee, kamati ya akina Abdul Sykes, Hamza Mwapachu, Steven Mhando, Dr. Vedasto Kyaruzi, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Said Chaurembo na John Rupia.

Muongeze na Mwanasheria Earle Seaton kwenye hilo kundi humuoni popote lakini alikuwapo rafiki wa Abdul Sykes.

Seaton ndiye aliyeandika "petition" ya Meru Citizens Union na ikasomwa UNO na Japhet Kirilo mwaka wa 1952 mkalimani akiwa yeye mwenyewe Seaton.

Yako mengi hawataweza kuyajua na kujifunza hadi wajifungue hiyo minyororo waliyojifunga na watoke ndani ya hilo dema.

Lazima ikubalike kuwa wakati haya yanafanyika Nyerere hakuwako na ni muhimu tutambue kuwa Nyerere kakipokea chama kutoka kwa Abdul Sykes.

Kijarubu kumkwepa Abdul Sykes katika historia ya TANU na Julius Nyerere ni kujitafutia matatizo bure.

Sasa inawezekana Nyerere hakuijua historia hii labda kwa kuwa Abdul hakumweleza kwa hiyo ikawa yeye kayaona yale tu aliyoyaona nyumbani kwa Abdul nyuma ya hapo hayajui.

Kama Abdul alimweleza na Nyerere hakuyapenda hili sasa ni shauri lingine kabisa.

Hapa yapo mengi ya kueleza lakini tusubiri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom