Alloyce PR
JF-Expert Member
- Nov 15, 2020
- 817
- 881
"Serikali ya awamu ijayo (2025–2030) ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haina budi kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri, na kurekebisha sheria za kodi ziwe jumuishi kwa kila mmoja. Zaidi ya yote, ni lazima kuwe na uwazi wa mali za viongozi.
Kwa kuongezea, sheria ya kuwawajibisha wala rushwa na watakatishaji fedha (money launderers) unapaswa kuimarishwa kupitia sheria mpya yenye mkazo zaidi bila kuyumba, pia kutoa adhabu ya kunyongwa hadi kufa kwa watakaobainika kutoa na kupokea rushwa au kutakatisha fedha.
Tukifanya hivyo, tutaona maendeleo ya kasi kiasi kwamba hata mabeberu watashangaa kuona hatuombi misaada kwao, wala kuingia kwenye mikopo ya kudhalilisha utu wetu kwa masharti yanayokwenda kinyume na maadili yetu ikiwemo Sheria za LGBTQ." — Alloyce, P.R.