Muhimu kwa wanasimba

Bwana Bima

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2014
Posts
429
Reaction score
929
Kutoka kwa Casto news.

π—‘π—œ π—¦π—œπ—”π—¦π—” π—­π—”π—žπ—˜ 𝗧𝗨 𝗠π—ͺπ—˜π—žπ—˜π—­π—”π—π—œ π—”π— π—žπ—˜π—‘π—œ π— π—”π—žπ—’π—Ÿπ—’

Nimeona posti ya mwekezaji wa makolo analalamika kuwa anakwamishwa na atajitoa,,Okay hapa staki kuongea kishabiki wala kimasihala Bali nataka kuongea Kama mwananchi ambaye napenda kusimama Kwenye ukweli.Ebu tuanzie hapa Tanzania Sheria zipo wazi kabisa haswa kwa wawekazaji ambao wana nia ya kutaka kuwekeza kwenye taasisi za wanachama.

Simba ni klabu ya wanachama na msingi wake mkubwa ni wanachama,Simba walikubali kwenda kwenye mabadiliko na wakampa Mo Dejwi nafasi ya kuwekeza ndani ya klabu yao je zile ada za wanachama ambazo mwekezaji aliwaleta Equit Bank zipo wapi Kuna Mwanachama anakua mrejesho wake hadi leo...?Ukiutazama mfumo wao wa Uwekezaji ni Kama Viongozi walikurupuka tu hawakutaka kutulia kufanya mabadiliko ya kweli,,Ni kiongozi gani ambaye alikubali kuwa thamani ya Simba ni 20B...?Ni kiongozi gani ndani ya Simba alifanya tathimini kwa kuwashirikisha wanachama kufanya tathimini ya Mali za klabu.

Miaka mitatu nyuma tume ya ushindani Tanzania Fcc walitoka hadharani kabisa kupinga mabadiliko ya Simba na kuwarudisha tena mezani kufanya mabadiliko ya Kweli,,Fcc walibaini madudu mengi ndani ya TRANSFORMATION ya simba,Kuna Kampuni Nne zilifunguliwa ambazo zote zilikuwa upande wa mwekezaji je ni kiongozi gani alisaini kupitisha hizo Kampuni za mwekezaji ambazo zilikuwa zinafanya kazi ndani ya klabu kwa kupitia mwekezaji.?

Mo leo hii ana haki kulalamika kuwa anakwamishwa kwasababu,,hadi Sasa hakuna kiongozi ambaye anapambana kutaka kuona mabadiliko yanatimia Try again kila siku anasema mabadiliko yapo hatua nzuri Ila hataki kusema wapo hatua gani,Haya leo mwekezaji anaondoka ni kiongozi gani anaweza Kutoka hadharani kudai 20B za mwekezaji,Na tayari mwekezaji kashatoa zaidi ya 20B ndani ya klabu.Siku zote huwa nawaambiaga amkeni watani daini mabadiliko ya ukweli,,kushangilia usajili au kumfunga Yanga sio mwisho wa klabu yenu.Kinachoendelea kwa Sasa Fcc wanataka ripoti nzima ya mabadiliko na hadi sasa hakuna Viongozi ambacho wamefanya.

Mo leo kakatisha kutoa pesa Ila hakuna kiongozi yoyote ambaye amesimama kuhoji kwa nini mwekezaji hatoi pesa na bado klabu inamtangazia biashara zake,,Mwenyekiti aliyepita kwa kujihuzuru MR MKWABI alisimamia katiba ya klabu ya kuitetea kwa kumuhoji mwekezaji anavyofanya vitu nje ya mkataba, mashabiki wote wa Simba mkamtukana,,Aya huyu wa Sasa kazi yake nini ndani ya klabu kutoa ahadi kumfunga Yanga..?

Muda bado upo simameni daini katiba mpya na mabadiliko ya Kweli Ila hii katiba inawanufaisha tu Viongozi waliopo madarakani. Shida kubwa humu Facebook haswa nzala wenu hawanaga wanachokijua zaidi ya kushangilia Manzonki,,Onana amkeni.
 
Simba nguvuuu moyaaaa
 
Hivi Mo ameshindwa kukaa mezani na viongozi ameona Twitter ndo suluhisho?

Ndio Simba kuna Uswahili lakini nae pia ni miongoni mwao, kafanya mambo mengi ya ajabu mitandaoni badala ya kutafuta njia nzuri.
 
Hivi Mo ameshindwa kukaa mezani na viongozi ameona Twitter ndo suluhisho?

Ndio Simba kuna Uswahili lakini nae pia ni miongoni mwao, kafanya mambo mengi ya ajabu mitandaoni badala ya kutafuta njia nzuri.
Mo anataka uungwaji mkono kwa mashabiki viongozi wengi pale simba wapigaji
 
Mo anataka uungwaji mkono kwa mashabiki viongozi wengi pale simba wapigaji
Mbona kama viongozi wote wa Sasa ni Pro-Mo? Ameshindwa nini kuwashinikiza wapeleke mbele Mchakato Kwa manufaa yake na ya klabu badala ya kuzusha taharuki na kuaibisha timu mitandaoni? Nani wa kumpinga Mo pale? Mangungu? Au Abdalla Jaribu tena? Hao ni watu wake kawaweka mwenyewe.
 
Watu wanataka wazione B 20 kweli zimewekwa na pili umiliki wa ile 51 ni kama jamaa ana watu ambao anataka kuwapa sasa akaja kubanwa kwenyw wadhamini ambao hawapaswi kuteuliwa na raisi. Na mwisho jamaa naona anatakaga kik tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…