Kigoma Independent
JF-Expert Member
- Dec 18, 2017
- 3,519
- 2,055
Muhogo ni zao la chakula na biashara lakini siku za hivi karibuni limeonekana kushamiri sana katika uwanda wa biashara kwa kusaidiana na kushirikiana na mashirika mbalimbali ili kupendeleza mnyororo wa thamani hasa kwa wakulima wadogowadogo.
Mashirika ya MVIWATA (Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania) na VECO (Vredeseilanden-Belgium NGO) yanashirikiana katika kuimarisha usalama wa kipato cha chakula miongoni mwa wakulima wadogowadogo. Mashirika haya yameanzisha mnyororo wa thamani kwa uzalishaji wa zao la muhogo.
Uchunguzi wa zao la muhogo kama kipaumbele ulifanywa na wakulima wa muhogo wenyewe. Shughuli muhimu ni pamoja na uimarishaji na uendelezaji wa asasi za biashara za wakulima na kuziunganisha kwenye soko. Pia midahalo mbalimbali imekuwa ikiandaliwa ili kuhakikisha kuna kuwepo na ushiriki wa wadau wengi kwenye mnyororo wa thamani hususani kwenye zao la muhogo kwa wakulima wadogowadogo nchini Tanzania.
Kwahiyo wale wote ambao ni wakulima wadogowadogo wa zao la muhogo na pia ambao wana malengo ya kufanya ukulima wa zao la muhogo mnapenda kushauriwa ili kushirikiana katika kulngaeza ufanisi na mnyororo wa thamani katika zao la muhogo nchini Tanzania kwa kilimo chenye tija na faida kemukemu kupitia ushirikiano ambao utapatikana kutoka mashirika mbalimbali nchini na nje ya nchi.