Muhoozi mbona mropokaji sana? ana sifa kuwa CDF kweli?

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Posts
5,840
Reaction score
8,202

Uganda: Tutaishambulia Iran kuilinda Israel​

KAMPALA, Uganda

MKUU wa majeshi wa Uganda amesema wako tayari muda wowote kuisaidia Israel endapo itazidiwa nguvu katika vita dhidi ya Iran.

Hata hivyo, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter).

Jenerali Kainerugaba amedai kuwa matarajio yao ni kuona mataifa hayo (Israel na Iran) yanamaliza mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.

“Tunataka kuona vita vya Mashariki ya Kati vikimalizika. Dunia imechoshwa na vita hivyo.

“Lakini, chochote kitakachofanyika kwa ajili ya kuharibu Israel, basi kitatuingiza vitani,” amesema.

Aidha, kauli yake hiyo inaendeleza matamko yake ya utata anayoendelea kuyatoa kiongozi huyo wa jeshi la Uganda.

Wiki chache zilizopita, Jenerali Kainerugaba alizua taharuki baada ya kusema Uganda ina mpango wa kumjengea sanamu Yonatan ‘Yoni’ Netanyahu.

Yoni, ambaye ni kaka wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliuawa akiwa komando wa jeshi la Israel katika vita ya Entebe, Uganda, mwaka 1976.
 
Achilia mbali u CDF, Imagine kesho na keshokutwa anakuwa raisi.
 
Huyo dogo ni mlevi tu wa Pombe na amekuwa akiwapa headache sana Wizara za habari anavyokuwa anatoa izo sentence zake tata ambazo sio msimamo wa serikali
 
Huyu ni wa kuchapa fimbo kama mtoto sababu hana tofauti na litoto lijinga
 
Uganda: Tutaishambulia Iran kuilinda Israel​

KAMPALA, Uganda

MKUU wa majeshi wa Uganda amesema wako tayari muda wowote kuisaidia Israel endapo itazidiwa nguvu katika vita dhidi ya Iran.

Hata hivyo, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, ambaye ni mtoto wa Rais Yoweri Museveni, ameyasema hayo kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter).

Jenerali Kainerugaba amedai kuwa matarajio yao ni kuona mataifa hayo (Israel na Iran) yanamaliza mgogoro huo wa Mashariki ya Kati.

“Tunataka kuona vita vya Mashariki ya Kati vikimalizika. Dunia imechoshwa na vita hivyo.

“Lakini, chochote kitakachofanyika kwa ajili ya kuharibu Israel, basi kitatuingiza vitani,” amesema.

Aidha, kauli yake hiyo inaendeleza matamko yake ya utata anayoendelea kuyatoa kiongozi huyo wa jeshi la Uganda.

Wiki chache zilizopita, Jenerali Kainerugaba alizua taharuki baada ya kusema Uganda ina mpango wa kumjengea sanamu Yonatan ‘Yoni’ Netanyahu.

Yoni, ambaye ni kaka wa Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, aliuawa akiwa komando wa jeshi la Israel katika vita ya Entebe, Uganda, mwaka 1976.
Amefika hapo kwa silver spoon mtoto wa baba ila kwa professional armies hata kikosi hapewi kwa mdomo huo
 
Halafu baba anamuandaa aje kuwa kiongozi mkuu...what a joke!
 
Ila kajibiwa hivi,( Trump )Tunashukuru sana kwa msaada wako ila hivi sio vita vya kitoto ni vita vya wakubwa
 
Nchi ya Baba anaweza kusema lolote,japo juzi kaongea fact kwa wale mnaopiga goti mkiwavisha Pete wachumba zenu😀
 
Back
Top Bottom